[wanabidii] Watanzania: TBC ni mali ya nani? - Mwanzo

Sunday, October 28, 2012

Imeandikwa na Egbert Mkoko, Grahamstown, Afrika Kusini — NAOMBA nianze makala haya kwa kuelezea kisa kilichotokea hapa Afrika Kusini mwaka 2006 kikiihusisha shirika la utangazaji nchini humu SABC, na kutawala vyombo vya habari kwa muda wa karibu nusu mwaka, kuanzia Juni mwaka huo hadi mwezi wa Desemba.

SABC iliingia katika msukosuko mkali baada ya gazeti moja maarufu liitwalo Sowetan kuvujisha habari za Mkuu wa Kitengo cha Habari ndani ya SABC, Dk. Snuki Zikalala, kuwapiga marufuku wanaharakati kadhaa kushiriki katika vipindi mbalimbali vya redio na televisheni.

Habari hiyo iliandikwa katika gazeti la Sowetan Juni 20 mwaka 2006, na iliwashtua raia wengi wa Afrika Kusini, kutokana na demokrasia iliyoanza kuota mizizi nchini humu, na hasa pale chombo cha habari cha umma kinapochukua hatua ya aina hiyo.

Kabla sijaendelea na kisa hiki, naomba tuwekane sawa kwamba SABC si chombo cha habari cha Serikali (state or government owned broadcasting) hapa Afrika Kusini, bali ni chombo cha habari cha umma (public broadcasting service) ambacho kimeanzishwa kwa mujibu wa sheria ya utangazaji namba Nne ya mwaka 1999.

Kutokana na hali hiyo, chombo hiki si mdomo wa Serikali na hilo limewekwa bayana katika sheria ya utangazaji na sera ya SABC.


http://wotepamoja.com/archives/9817#.UI1GaCyJttY.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments