[wanabidii] TUNATAKA JESHI LA POLISI LA AINA GANI ?

Tuesday, October 30, 2012
Ndugu zangu

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kumetokea mambo kadhaa
yanayolihusu jeshi la polisi kama taasisi muhimu ya kulinda mali na
usalama wa wananchi wa Tanzania , mambo yenyewe ni mengi siwezi kuanza
kutaja moja moja ila kwa ufupi mambo hayo yameonyesha Jeshi letu la
polisi kushindwa kuwa na muelekeo sahihi katika kukabiliana na
changamoto kadhaa zinazoendelea kwa sasa hivi .

Pia muda huu tuko katika mchakato wa kutoa maoni yetu kuhusu katiba
mpya.
Napenda kuleta mada hii kwa ajili ya kuchangia na tuone tunahitaji
jeshi la polisi la Aina gani katika Tanzania .
Hapa chini naweka Muongozo wangu tu .

MUUNDO WA JESHI LA POLISI
Hapa tunaona kule mwanza kamanda wa polisi ameuwawa lakini wapelelezi
na vigogo wengine wanatoka DSM kushugulikia suala hilo kitu ambacho
kinatumia gharama kubwa , matukio kama haya yanaweza kutokea 5 kwa
wakati mmoja ina maana jeshi la polisi makao makuu wataacha ?

JESHI LA POLISI NA TAALUMA ( Mafunzo )
Vipi kuhusu taaluma je tunajeshi la polisi linalokusanya wanataaluma
wa fani mbalimbali na ambao wanaweza kufanya kazi zao bila kusumbuliwa
na bila kuhitaji msaada kutoka nje ?

RUSHWA NDANI YA JESHI LA POLISI

VYUO VYA MAFUNZO VYA POLISI

USHIRIKIANO WA POLISI NA VYOMBO VINGINE VYA DOLA

USHIRIKIANO WA JESHI LA POLISI NA WANANCHI

TABIA ZA BAADHI YA POLISI NJE YA JESHI HILO YAANI URAIANI

VYAMA VYA KITAALUMA NDANI YA JESHI LA POLISI

MUHIMU : Mimi sio mfanyakazi wa Wizara ya mambo ya ndani ni mdau wa
sekta hii tu kama walivyo Watanzania wengine .

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments