[wanabidii] Rais Kikwete afanya uteuzi wa makamishna wa Magereza

Monday, October 01, 2012
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Magereza na maafisa wengine.

Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo amesema Rais amemteua Bwana John Casmir Minja kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza na kuwateua wengine kuwa maofisa kama ifuatavyo:

  • Dkt. Juma Ally Malewa ameteuliwa kuwa Kamishna, Divisheni ya Sheria na Uendelezaji wa Magereza.
  • Bwana Deonice Lwamahe Chamulesile ameteuliwa kuwa Kamishna, Huduma za Urekebishaji.
  • Bwana Gaston Sanga ameteuliwa kuwa Kamishna, Divisheni ya Utawala na Fedha.

Wengine ni:

  • Bwana Fidelis M. Mboya ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani, ambapo kabla ya uteuzi huu Bw. Mboya alikuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria na Uendeshaji wa Magereza na;
  • Bwana James B. Celestine, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, amepandishwa cheo na kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ambapo atarejea Magereza na kupangiwa kazi nyingine.

Kulingana na taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Oktoba 1, 2012 mjini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huu umeanza tangu tarehe 25 Septemba, 2012.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2012

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments