Rais Obama amoenyesha kuelewa anachokisema na kumaanisha anachokifanya.
Aliahidi kumaliza vita ya Iraki amefanya hivyo, aliahidi kuondoa askari wake afganistani amefanya hivyo, aliahidi kumtafuta Osama na amefanya hivyo.
Romney alijaribu kutoa taarifa za uongo kuhusu Obama jinsi alivyo shughulikia suala la kuuwawa kwa wanadiplomasia wa Marekani huko Libya na Obama aliweka taarifa hiyo sahihi na kumuumbua Romney.
Pia Romney alijaribu kutoa taarifa ambazo sio sahihi kuhusu uzalishaji wa mafutoa n.k , Rais Obama aleweka taarifa hiyo sahihi.
Kwa ujamla Obama amefanya vizuri zaidi katika mdahalo huu kuliko mdahalo uliopita na ameamsha hamasa na kuonyesha uwezo wake wa kuongoza.
Tunajifunza kuwa ni muhimu kuwa na taarifa sahihi kuhusu mambo muhimu na sio kukurupuka kuzungumza mambo bila kufanya utafiti.
Pili tunajifunza umuhimu wa vyombo vya habari na wadau wake kuwa makini na kufikisha ujumbe kwa jamii, maana muongozaji mdahalo nae alikuwa anajua kuhusu mambo yanayojadiliwa na pale alipoona kuna upotofu alikuwa anaweka usahihi.
Tatu tunajifunza umuhimu wa midahalo katika kusaidia wananchi kufanya maamuzi kuhusu wagombea wa nafasi za kisiasa.
Phares Magesa.
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments