[wanabidii] MUNGU ATUSAIDIE 'WENGI NI WAPENDA MADARAKA NA SI VIONGOZI'

Saturday, October 06, 2012
Inasikitisha kuona Wapenda Madaraka wakiwadanganya wananchi kwamba wakipewa 
Nafasi Wataifanya nchi kutoa Mabomba ya Maziwa..

Ni jinsi gani tutawasaidia wananchi waache ushabiki wa kisiasa nakuona tatizo au mfumo fulani
ambao umeingiza nchi kwenye matatizo.

Tunahitaji Viongozi na si Wapenda Madaraka.  Wananchi wengi wanajua asilimia kubwa ya matatizo yetu, yamechangiwa zaidi na 
wanasiasa wetu na mfumo wa ndani na wakidunia .

Wanasiasa Acheni kuwadanganya wananchi badala yake tuwape wananchi nguvu ya sheria na mshikamano...na 
Sisi wananchi tubadilike tuondokane na kutoa Rushwa miongoni Mwetu nk...

Inakuawje Mwanasiasa anaingia kwenye siasa ndani ya miaka kadhaaa ana Mali na Pesa kuliko hiyo mishahara ya ubunge au Uwaziri..

Chadema na CCM wengi wao ni wezi tu....Majina Makubwa na Ufisadi na hata Wakipewa nchi zaidi wanataka kuandika Historia, Nilikua Raisi, Waziri, Mbunge etc
na si kumkomboa Mwananchi.

Wanasiasa Msitumie advantage ya Matatizo ya Wananchi kujipatia nafasi za kisiasa huku mkijua matatizo tulio nayo hawezi kubadilka ndani ya Muda mfupi sababu ya Mfumo wa kidunia ambao unatukandamiza nchi masikini

Mungu walinde Watanzania na Uwaokoe na Mafisadi na Hali Ngumu ya Maisha (Tayari Mungu alishaibariki Tanzania Mafisadi wanaifaidi)
Mungu Ibariki Africa




--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments