[wanabidii] KWA WAISLAMU KESHO NI ARAFA-IFAHAMU

Wednesday, October 24, 2012
               ASSALAMU ALAIKUM YA HAYYU ALLADHINA AMANUU

kwa wale waislamu napenda kuwakumbusha na pia kuwasisitiza kuwa kesho ni moja ya masiku matukufu, ni siku ya ARAFA,
ARAFA-ni mwezi tisa ya kila mfungo tatu, asili ya arafa kwa uchache ni eneo ambalo kwa mara ya kwanza  adamu na hawa walionana for the first time, baada ya kutupwa duniani,ni pale walipo ondolewa kwenye bustani walizokuwa wakikaa,...pana historia nyingi na maelezo mengi, lakini kwa uchache ni hivo, kwa mantiki hiyo kesho mahujaji wataenda kushinda kwenye viwanja hivo vya arafa, therefore kwa wale ambalo hatukupata nafasi ya kwenda hijja tuna paswa ingawa ni sunna, kufunga hiyo kesho even though tulipaswa tufunge kwa masiku yote tisa mara baada ya kuingia mfungo tatu....kuna fadhila nyingi sana kwa atakae funga hiyo kesho, moja ya fadhila hizo ni kusamehewa dhambi mwaka mmoja kabla na mwaka mmoja baadae  kama ALLAH akitaka au akipenda na kama ukikamilisha masharti ya toba, masharti ambayo nahakika mnayasikia kwa viongozi mbalimbali wa dini ikiwa ni masheikh, maimamu nk
kwa wale mnaopenda kuwabeza waislamu natoa ombi la kutowabeza katika thread hii niliyo iposti kwani ni mambo yao ya kuabudu.....
nawatakia nia ya kufunga kama afya ipo
wabilah taufiki
IDD MUBARAKK

Share this :

Related Posts

0 Comments