wa UVCCM mkoa wa Iringa angalau kwa nia moja tu kujua namna wapiga
kura wanavyofanya maamuzi yao ya kisiasa.
Kwa kuwa nimeweza kushuhudia siasa za iringa angalau tangu mwaka
1995 wakati huo nikiwa kijana mdogo sekondari lakini niliweza kuona
mtazamo wangu wa siasa na hamasa za Wakazi wa iringa juu uchaguzi.
Kwa hakika Uchaguzi huo kwa bahati nzuri UVCCM taifa ilirudisha
majina 3 ambayo kwa hakika majina mawili ni ya makada wa CCM na
UVCCM tangu siasa za vyuo za UVCCM na ndani ya Chama makada hao
ni Abba Ngwilangwa na Ramadhani Baraza.
Nilitegemea sana makada wa UVCCM na wajumbe waliokuwa na haki ya
kumchagua mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa basi kura zao
zingeangukia katikaRamadhani Baraza ambaye kwa hakika wasifu wake
kisiasa ni mkubwa au akipata ushindi Abba Ngwilangwa ambaye yeye
nae wasifu wake kwa Chama hauna mashaka.
Kwa hakika mimi binafsi sina imani na Tumaini Msowoya kama anauwezo
wa kuiimarisha CCM na UVCCM Iringa ili kuweza kupambana na CHADEMA
katika mkoa wa Iringa na wilaya zake.Nadhani hapa Chama cha
Mapinduzi kimepotea njia bila ya kujua.
Kama CCM Mkoa wa Iringa wasipokuwa makini basi kuna dalili zote
jimbo mla Iringa Mjini kubaki upinzani na majimbo k uongezeka kwa
CHADEMA kupata majimbo zaidi.
Wajumbe na wenye nafasi ya kupiga kura siku zote wanatakiwa kuwa
makini mno katika uchaguzi kwani uchaguzi ni uhai wa Chama na
vinginevyo uchaguzi unaweza kuwa umauti kwa chama.
Kama hali hii itaendelea Iringa mjini kubaki kwa CHADEMA kwa miaka
10 zaidi.Ninasema haya kwa kuwa UVCCM ndipo moyo wa chama ulipo
kama moyo ni dhaifu basi na mwili mzima wa chama utakuwa dhaifu
kabisa.
Wasalaam Adeladius Makwega
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments