Kuna jambo ambalo watu wanataka kulizoea hapa mjini, hasa linapopita gari la wagonjwa (ambulance) watu wasiohusika hujiunga na msafara wa gari hilo au kama ni msafara wa viongozi utaona baadhi ya madereva wasiokuwamo kwenye huo msafara wanaunga na wao kwenye msafara. Jamani hii ni hatari waweza kujikuta kwenye matatizo ya kuvamia msafara au kusababisha ajali pale msafara unapoingia njia ambayo wewe huelekei.
Leo asubuhi nimeshuhudia katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi pikipki ya polisi ilipita ikisafisha njia halafu yakapita magari kama 3 hivi na baadaye magari yasiohusika yakajiunga. Msafara ulipofika pale St. Peter ukaelekea Oysterbay sasa wale waungaji walikuwa wanenda mjini pale walibabaika sana karibu wagongane wao kwa wao. Wito tuache kujiunga kwenye misafari isiyotuhusu itakuja kutugharimu.
0 Comments