[wanabidii] Masikini Lowassa

Tuesday, April 12, 2016
Ndugu zangu nimeamua kuandiaka makala yangu haya leo kutokana na matamshi ya Lowassa, ya hivi karibuni mbele ya wageni wake waliomtembelea nyumbani kwakwe Masaki, Jijini D are Es Salaam, waliotajwa kuwa ni wanazuoni kutoka ndani na nje ya nchi, walioongozwa na mwanazuoni mwenzao, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dare Es Salaam (UDSM) Professor Rwekeza Mkandala.

Professor Mkandala amekaririwa na vyombo vya habari nchini akisema kwenda nyumbani kwa Lowassa, kulilenga kufanya utafiti wao wa kitaaluma na kwamba watafanya hivyo kwa wanasiasa wengine walioshiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Kama kweli Professor Mkandala anasema kweli, nimejaribu kurejea taarifa mbalimbali zilizomkariri Lowassa akisema hayo aliyosema, sikuona lolote linaloweza kuingizwa kwenye utafiti wowote ule wa kitaaluma kwa maana halisi ya taaluma. Sifahamu taaluma ya usanii na sanaa, lakini naamini yenyewe ina misingi na kanuni zake. Mtu huwezi kukusanya porojo, halafu ukaziita tafiti.

"Uchgauzi ule (wa October 25) tulishinda na kila mtu anajua hivyo hata Magufuli anajua hilo lakini walitumia vyombo vya dola kupora ushindi wetu. Zilinunuliwa pingu nyingi sana kwa lengo la kuwafunga waleta mabadiliko… kwa sasa tumejipanga kuhakikisha hatuporwi tena ushindi wetu katika uchaguzi ujao kwa sababu joto la kutaka mabadiliko ni kubwa na watanzania bado wameichoka CCM.

Masikini Lowassa hana washauri? Au anao, lakini hawamwambii ukweli? Kila kona ya nchi vijana waliompa kura katika uchaguzi wa October 2015, wanajutia kura zao walizopoteza kwa kumpa yeye, leo Lowassa anasimama mbele ya kina Prof. Mkandala anasema anajiandaa kushinda uchaguzi ujao.Kweli? Kwanza kwa chama gani, Chadema? Aataisikia Redioni 2020.

Mwaka 2020, Lowasa atakuwa na umri wa miaka 67 wakati Magufuli atakuwa na miaka 61, tena akiwa na rekodi iliyotukuka ya kuwashughulikia mafisadi na kuirudisha nchi katika mstari ikiwemo nidhamu na uwajibikaji serikalini na uzalendo kwa wananchi wote Watanzania, na hili la mafisadi ndilo lililokuwa chukizo kuu la vijana wa Tanzania. Je kijana gani atakayemnyima kura Rais Maguful na kumpa Lowassa?

Kwa dili gani tena la kifisadi kama Richmond atakalopiga tena Lowassa na washirika wake katika utawala huu wa Magufuli kwa lengo la kupata fedha za kunyweshea vijana viroba wamuunge mkono katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Lowasa huyu anasema: "Bandarini (Dar es salama) kwa sasa nasikia uingizaji wa mizigo umeshuka kwa asilimia 50, kampuni nyingi za mizigo zimefungwa shughuli zao, na pale kulikuwa na vijana wetu wengi wana ajira sasa hivi wako mitaani, maisha ya mwananchi yanazidi kuwa magumu" Kama kunashuka kwa idadi ya mizigo ya wakwepa kodi katika bandari hiyo, bora hata hiyo asilimia 50 anayosema ipotee kabisa ili bandari ibaki tupu kuliko nchi kuruhusu bandari zetu kuwa uchochoro wa wafilisi uchumi wa taifa hili.

Falsafa iliyochaguliwa na wengi October 25, mwaka jana. Ni hapa kazi tu, na kazi hiyo iwe ya halali, na si ile iliyotangazwa na Lowassa akiwa mikoani kwenye kampeni zake zake, kuruhusu kahawa na ndizi kuuzwa kwa njia ya magendo nchini Uganda.

Falsafa hiyo ya Rais Magufuli na CCM yake inahimiza kazi halali, kwa hiyo kama vijana hao wa Lowassa walizoea kuishi maisha ya kiujanja ujanja ukweli ni kwamba hawana nafasi tena. Busara ya Lowassa ingewahimiza kutafuta kazi ya halali na si vinginevyo.

Lowassa anasema: "Kugawa fedha pesa si kazi ya Rais, kuna mamlaka amabayo ina mamlaka ya kidhinisha bajeti, ambayo ni bunge". Ebo Anachofanya Rais Magufuli ni kubadilisha matumizi kutoka eneo Fulani kwenda eneo Fulani lenye kipaumbele zaidi kwa wananchi na fedha hizo zilishaidhinishwa na bunge kupitia Bajeti ya mwaka 2015/2016.

Fedha za uzinduzi wa bunge zilipelekwakununua vitanda Muhimbili, zilishapitishwa na Bunge la bajeti iliyopita, Rais akasema haiwezekani wabunge kula na kunywa bilioni 2 zote wakati wazazi na watoto wao Mhuhimbili wanalala chini.

Fedha za Decemba 9,2015 siku ya uhuru zilipitishwa na Bunge la bajeti iliyopita, Rais Kasema kuna kero ya foleni katika barabara ya Morocco hadi Mwenge hivyo ipanuliwe, Leo magari akiwemo Lowassa mwenyewe anaserereka tu pale. Ni fedha ganianayogawa Rais Magufuli anayogawa kinyume na taratibu?

Kwa hakika Lowassa amenikumbusha kamati yake ya Maadhimisho ya Uhuru ya miaka 45, tuliambiwa kuwa imetumia Sh. Bilioni 50 wakati nchi ikiwa gizani kwa kukosa umeme, huku akiwa ameikumbatia bado Richmond yake kwenye mifuko ya sauti yake, kumbe nayo ilikuwa sherehe ya dili.

Kilichonishangaza zaidi na kunikatisha tama kwa Lowassa ni kauli yake hii: " Kitendo cha nchi wahisani wakiongozwa na na Marekani kukata misaada yao, ni pigo kwa mustakabali wa uchumi wa nchi yetu…….halafu tunasema tunataka nchi ya viwanda, pesa tutatoa wapi kama si hawa wafadhili wa ndani nan je kusaidia katika hili? Hwa wafadhili si wakubeza….wataturudisha nyuma".

Hapa nalazimika kukubaliana na wale waliokuwa wakidai wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka wa jana kwamba Lowassa keshaipiga bei Tanzania yetu kwa Mataifa Makubwa ya nje.

Rais Magufuli anapambana kuhakikisha Taifa linaondoka kuwa tegemezi pamoja na kutembea na bakuli la ombaomba nje, Halafu Lowassa anatuambia tusiwabeze wafadhili wan je. Kweli? Anataka tuwanyebyekee na kuwapigia magoti kana kwamba hatuko huru

Lowasa anazungumza haya akijua fika kwamba misaada MCC kwa Tanzania ni sawa na tone la maji kwenye bahari ikilinganishwa na misaada amabayo Taifa hili inapatakutoka Marekani kupitia mipango mbali mbali.

Watu gani wanafadhili mapambano dhidi ya Maralia na Ukimw, si Marekani kupitia Shirika lake la misaada la kimataifa la (USAID)? Trilioni moja kwa miaka mitano ambayo nisawa na bilioni 200 kwa mwaka?

Mbona mfuko wa Bill na Melinda Gate pamoja na mfuko wa George W. Bush wanaendelea kumwaga mamilioni ya shilingi kwa Tanzania? Hao si Wamarekani? Pigo linatoka wapi kama Lowassa hana dhamira mbaya kujenga taswira hasi juu ya uhusiano wetu na Marekani?

Kweli hata Lowassa hafahamu kwamba shilingi trilioni moja ukiigawanya kwa miaka mitano ni sawa na bilioni 200 tu kwa mwaka? Serikali ya Rais Magufuli ikiziba mianya yote ya wizi na ufisadi, Tanzania itashindwa kupata Shilingi Bilioni 200 kwa mwaka ili kuziba pengo la MCC? Vipi kuhusu misaada ya USAID kupitia mpango wake wa Partership for Growth? Loawassa halijui hili? Namuhurumia Lowassa, Nahitimisha

Chanzo Tazama
12 April,2016

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments