[wanabidii] Je diwani na mtendaji wa kijiji n a Kata wana mamlaka ya kumwondoa Mwenyekiti wa kijiji aliyechaguliwa na wananchi?

Thursday, April 14, 2016

Inasikitisha sana kuona eti watendaji wamekuwa na mamlaka ya kumnyanganya Madaraka Mwenyekiti wa kijiji cha Shighatini Kata ya Shighatini Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro bila hata ya kufuata sheria na meongozo wa serikali ya mitaa mamlaka ya Wilaya.
Najiuliza INA maanani wiote hawasomi hizi sheria au kwanini wawashinikize halmashauri na wananchi kupiga kura ya kukosa imani na Mwenyekiti wao kwa siri kinyume na taratibu za kisheria .Na kumdhililisha Mwenyekiti kama Mwizi au Muuaji wakati viongozi wapi na wamekaa kimya huku wananchi wakizidi kushangaa kuna tatizo gani. watu wamekuwa miungu mtu kijijini na Rais haoni.

Diwani ndiye aliyekuwa anasimamia na kushinikiza mama huyu atolewe nje kwa chuki za kisiasa.
Mama huyu Mara nyingi amelalamika kwao lakini hakuna kinachoendelea had I tarehe 22/03/2016 Halmashauri ilipotaka meza ipatane au watajiuzulu.
Mwenyekiti alipomweza kaimu katibu Kata na diwani ndio tatizo lilipoibuka. Mara nyingi wamekalishwa chini lakini KATIBU huyu wa kijiji amejas dharau amekuwa habadiliki.

Sakata hili limeanza Mara baada ya Mwenyekiti huyu ambaye ni mwanamke kudai mapato na matumizi ya kijiji na kukemea baadhi ya wajumbe kwa kushirikiana na katibu Hutu wakijiji kutumia fedha za wananchi kinyume na taratibu zilizowekwa na pia fedha za Tasaf na pango la  vyumba mbalinbali vya kijiji kutumiwa vibaya pamoja na fedha za mradi wa maji ya world bank kushinikiza kuwa zigawanywe na kijiji ambacho zamani nilikuwa chini ya kijiji hiki cha Shighatini kukataa kushiriki ugawaji huko kwani fedha za miradi zina taratibu zake.
Migogoro mingi Kila Siku kati ya Mwenyekiti na katibu kwani kaimu katibu Kata na diwani wana Mahusiano ya karibu na ni ndugu  na wanatoka  sehemu moja

KATIBU bhuyu anashika mihuri yote Kila kitu anasfanya yeye ni migogoro anasuluhisha yeye haonyeshi barua vitabu jambo lolote ni had I Mwenyekiti amjie juu kama  atasikia kutokana kijiji vingine
Hakuna kamati iliyochaguliwa ni zile zile za zamani na hataki huyu Mwenyekiti ahudhurie kikao chochote anamwambia yeye hahusiki wenyviti wa vitongoji hawajawahi kufanya kikao chochote na wananchi wao yeye hasimamii shughuli za maendeleo anadai hataki kugombana na wananchi shughuli hakuna kinachoenda kazi yake anatafuta mahali penye hela kama Tasaf kugawa vyandarua nk yaani ni shida

Tunaomba jambo hili litupiwemcho na watendaji wenye dhamana  kwani wananchi wanaumia pasipo msaada huyu Mwenyekiti anasema hajawahi kulipwa posho yoyote ya uongozi wake tangia achaguliwe lakini anasikia wenzake wanalipwa she hamsini nk
Nami amsaidie mama huyu wana sheria wanawake
Unasemaje ananilea Nkya upo?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments