1. Serikali yazidi kuiongezea mzigo benki ya Stanbic kashfa ya mabilioni
Hii ni habari inayopewa nafasi ya kwanza kwa uzito na mtandao waMjengwablog.com . Inahusu uchumi wa nchi na inatokana na hukumu ya mahakama ya Uingereza iliyotamka kuwa Tanzania ilipwe dola milioni saba ikiwa ni asilimia moja ya riba iliyoongezwa na tozo ya shilingi bilioni moja. Benki ya Stanbic ikaiingiza kinyemela kampuni ya EGMA kama mtu wa kati ' Dalali' na kuongeza asilimia moja. Katika kashfa aliyepata kuwa Miss Tanzania 1996, Shose Sinare naye jina lake linahusishwa.
2. Gazeti Mawio lafutwa kwenye orodha ya magazeti
Hii ni habari iliyotawala kwenye magazeti mengi. Mtandao waMjengwablog.com inaipa nafasi ya pili kwa ukubwa. Wengi wanajiuliza sababu za Mawio kufutwa. Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali na maelezo ya waziri mwenye dhamana, Nape Nnauye, Mawio limefutwa kwenye orodha ya msajili wa magazeti kutokana na kuandika habari za uchochezi. Kwa mujibu wa Waziri Nape, kati ya habari hizo ni ; " Machafuko yaja Zanzibar" na " Seif Rais Zanzibar, maandalizi ya kumtangaza yaiva".
3. " Zanzibar ikiwaka, Bara haitapona"
Hii ni kauli iliyotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Askofu Jude Ruwa'ichi. Ni habari inayopewa uzito wa tatu kwa siku ya leo na mtandao huu wa Mjengwablog.com
Kimsingi Askofu ametimiza wajibu wake wa kiroho katika kuwaasa wenye dhamana kufanya maamuzi magumu yatakayopelekea uwepo wa amani, akisema, " Zanzibar pakiwaka na Bara hapatakuwa shwari." Inahusu amani ya nchi. Ni kauli ya kuzingatiwa kwa pande husika zilizo kwenye mgogoro.
Soma habari nyingine na katuni bora ya leo. Ni kwenyehttp://mjengwablg.com
Maggid Mjengwa
Mhariri/Mchambuzi
Habari za mtandaoni/Mjengwablog.com/KwanzaJamii
0754 678 252
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at https://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye5_X1%2BnR7LrgxKvhSB9vGN4Z3fZzwA3PDvUbthVm0iStg%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments