Ndugu zangu,
Bandari ni sehemu muhimu na nyeti katika kukusanya mapato ya kuendesha nchi na hata ikakua kiuchumi.
Inashangaza, hizi zinazoitwa bandari kavu, na zinazomilikiwa na makampuni ya Watanzania wenzetu wafanyabiashara zimeachwa ziruhusu panya wachimbe mashimo na kufanya kazi ya kutafuna mapato ya nchi.
Ni jambo jema kuwa sasa tunaonyeshwa hadharani wahusika wenye kuwafuga panya hawa wenye kuhujumu uchumi wa nchi ili hali wahusika wenyewe wakineemeka kwa kujikwapulia mapato yasiyolipiwa kodi.
Unashangaa kuwa hawa ndio wenye kujiita Wafanyabiashara wakati hawana hata aibu ya kufanya hujuma hizi zenye kuwaumiza wanyonge wengi raia wa nchi. Umefika wakati kwa Serikali, kuhakikisha, zinafukia na kupiga zege juu ya mashimo ya panya ya zinazoitwa Bandari Kavu.
Kamwe Jamhuri haipaswi kushindwa vita dhidi ya wenye kufuga panya watafuna mapato ya Jamhuri. Kwa Kiongozi Mkuu wa Jamhuri kusalimu amri kwenye vita hivyo, ni sawa na kukubali kuiweka rehani Jamhuri na raia wake
Viva Republic!
Maggid Mjengwa,
0754 678 252
Iringa.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments