[Mabadiliko] Uchambuzi Wa Habari: UKAWA Wametishia ' Chui' Mara Nyingi...!

Thursday, November 19, 2015


Ndugu zangu,

Kwenye magazeti ya leo moja ya habari kubwa ni UKAWA kutishia kumzuia Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano asihutubie kesho Ijumaa.

Kuna kisa cha kijana aliyekwenda kuchunga ng'ombe porini. Akaamua kufanya masihara na waliobaki kijijini. Akapiga kelele kuashiria kuna hatari. Watu wakaacha kazi zao, wakabeba silaha kwenda porini, walipofika kijana akaonekana yuko juu ya mti akidai kuwa amemwona chui.

Watu wazima wakashindwa hata kuanza msako wa chui kwa vile hawakuona hata nyayo za chui. Kijana yule akarudia mchezo ule mara kadhaa. Mwisho watu wakaamua kumpuuzia. Lakini,ikafika siku chui wa ukweli alitokea, na kelele za kijana yule hazikusaidia, watu wazima walimpuuzia. Akaliwa na chui.

Kisa hicho chapaswa kiwe somo kwa UKAWA. Kwenye jambo kubwa la kitaifa kama linalotarajiwa kutoea kesho, viongozi wa UKAWA walipaswa kutambua kuwa macho na masikio ya Watanzania kwa mamilioni, wakiwamo Watanzania waliowapigia kura UKAWA, yanaelekezwa Dodoma.

Maana, Watanzania wana uelewa pia, kuwa hii ni Jamhuri, na Rais na Amiri Jeshi Mkuu anasubiriwa kwa hamu hiyo kesho kwenda kuongea na Watanzania wote kuonyesha mwelekeo wa Serikali yake. Hakuna kwenye Jamhuri anayeweza kulizuia hilo, na viongozi wa UKAWA wanalifahamu hilo.

UKAWA walipaswa kuzuia mchakato uliopelekea Rais wa Jamhuri kuapishwa. Kama wameshindwa kufanya hivyo, kutishia leo kumzuia Rais kuhutubia Bunge ni sawa na kisa kile cha kijana aliyetishia chui mara nyingi, maana, UKAWA sasa wako kwenye mtihani wa imani, tayari kuna wananchi wanaokosa imani nao kwa hulka ya baadhi ya viongozi wakuu wa UKAWA kutoa matamko yasiyotekelezaka, ikiwamo kutangaza mgomo na maandamano nchi nzima.

Na mwisho wa yote; Hii ni Nchi Yetu Sote. Katika yote tuyafanyayo, ni vema na ni busara kutanguliza maslahi mapana ya nchi. Kujaribu kumzuia au kumfanyia fujo Rais wa Jamhuri asitekeleze yaliyo katika wajibu wake si jambo lililo na maslahi mapana kwa nchi. Na hilo linapaswa lisemwe, hata siku ile, Rais wa Jamhuri atakapotoka UKAWA na wapinzani wakafanya jaribio kama hilo, kumzuia na kumfanyia fujo asitekeleze yaliyo katika wajibu wake, Rais wa Jamhuri aliyetokana na UKAWA.

Maggid.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye6HQhnZkfrXP8yOYUwuzek3k0KaezMzrdfAQ3K-wf27MA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments