[wanabidii] Nimeshangazwa Sana Na Kauli Za Mbowe Na Anna Mghwira..Ni Za Kumfagilia Njia John Magufuli..!

Friday, October 16, 2015


Ndugu zangu,

Kwenye ITV usiku huu nimesikia kauli za ajabu kutoka kwa viongozi waandamizi wa vyama viwili vya kisiasa, Chadema na ACT.

Ndugu yangu Freeman Mbowe akiwa Mwanza amesikika akiwahimiza wafuasi wa chama chake baada ya kupiga kura wabaki wakilinda kura kwa kusimama mita mia mbili. Na dada yangu Anna Mghwira vivyo vivyo, akiwa Singida amesema yenye kufanana na Freeman Mbowe.

Nina bahati ya kufuatilia chaguzi za vyama vingi tangu zianze katika nchi hii ukiacha za nyuma ya mwaka 1964 ambazo nimezisoma tu vitabuni. Kuna mambo ya msingi kwenye demokrasia ya vyama vingi ambayo Freeman Mbowe na Anna Mghwira wanapaswa kuyajua, lakini, huenda kwa makusudi wanajitia ujinga wakidhani kwa kufanya hivyo yatawasaidia kisiasa.

Watanzania wa leo sio wale wa mwaka 1995. Ni waelewa zaidi. Vyama kuhimiza wafuasi wao wabaki kwenye vituo vya kupigia kura mita mia mbili na hata kwa siku nzima tu ni kukaribisha hali ya vurugu na uvunjivu wa amani. Kama vyama havina imani na mchakato mzima ni vema na ni busara vikasusia uchaguzi kabla kuliko kushiriki katika mazingira hayo.

Na kwa walivyo wapiga kura wa Tanzania, walio wengi hutafsiri tabia ya chama kuanza kulalamika na hata kuchukua hatua zinazoweza kuvunja amani kuwa ni dalili za chama husika kuelekea kushindwa.

Freeman na Anna, kama viongozi wa vyama na mmoja ni mgombea urais, wanapaswa kuwa makini zaidi. Siku tisa kabla Uchaguzi Mkuu, kauli za Freeman Mbowe na Anna Mghwira, bila wao kujua, zaweza kuwa zimetuma ujumbe huo kwa wapiga kura wengi, hivyo, kujiharakishia wenyewe anguko lao na kumsafishia njia ya Ikulu mpinzani wao mkuu, John Pombe Magufuli.

Ni mtazamo wangu.

Maggid

Iringa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments