Ngoja nimkumbushe kidogo mzee Kingunge CCM ya mwaka 1995 wakati akiwa katibu wa itikadi na uenezi wa ccm Taifa, kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma walikwenda wawili na Mzee Rashidi Kawawa, kumpokea Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa ccm Mwalimu Julias Nyerere.
Wakiwa hapo Uwanja wa ndege Mwalimu aliwauliza, Rashidi kwenye orodha ya wagombea John yumo (akimaanisha John Samwel Malecela). Kawawa akamjibu ndiyo yupo, Nyerere akamwambia Mwambie Ally aje achukue kadi yake akimaanisha Mwenyekiti wa Taifa CCM na Rais wa CCM na Alhaji Ally Hassan Mwinyi. Ilibidi yeye mwenyewe Kawawa na Mzee Job Lusinde waende kumsihi Malecela aondoe jina lake kwenye orodha ya urais.
Naye John Malecela wakati akijitoa kwenye kinyanganyiro cha urais alisema ' nimeamua kujiondoa kwenye orodha ya wagombea uris, nimeondoa jina langu kwa manufaa ya chama changu' Namuuliza mzee wangu Kingunge. Je kwa wakati huo Nyerere alikuwa nani?
Je Hakushinikizwa Malecela ajitoe akiwa hana wadhifa wowote wala hakutumia cheo chochote isipokuwa uamuzi wake tu binafsi? Je Katiba ya CCM haikuvunjwa.
Yeye akishirikiana na Mwalimu Nyerere alimshinikiza Malecela ajitoe kwa sababu hakumpenda. Leo (Kingunge) anaishutumu kamati ya maadili kwa madai ya kuwa haina mamlaka wala uwezo wa kikatiba wa kukata jina la mtu. Amedai kwenye kamati kuu wakiwa na majina yao mifukoni.
Kingunge hataki kukubaliana kwamba chama cha siasa lazima kiendeshwe kwa utaratibu, vinginevyo akiri kwamba hata wao mwaka 1995 hawakufata katiba wakati wanaliondoa jina la Malecela pasipo kutoa sababu wala kumpa nafasi ya kujitetea.
Kama Malecela ameenguliwa mwaka 1995 kwanini iwe nogwa kwa Lowassa kuenguliwa na kamati ya maadili kwa sababu zilizowazi? Kingunge akubali kwamba alikuwa mmoja wao wakati wa kumsulubu
Malecel kwa sababu za binafsi na kwa hiyo ubinafsishaji wa ccm haujaanza leo.
Kingunge huyu amabaye leo anasema ccm haina demokras alikuwa bega kwa bega na Mwalimu mwaka 1995 walipopiga panga jina la Lowassa hadi kusababisha wanuniane na yeye (Kingunge) na Lowassa.
Ilifikia hatua ya Lowassa kumtolea maneno makali Mzee kingunge hadi kufikia hatua ya kumshitaki kwa Mwalimu, akaonywa.
Kingunge hasemi ukweli lakini kama angekuwa mkweli sababu ya utajiri ambao mwaka 1995 ulitumika kumfanya Lowassa akose sifa kutokana na kuonekana ana mali nyingi amabazo hawezi kuthisibitisha kwamaba alizipata kihalali, kwa Lowassa amekuwa tajiri zaidi ya mwka 1995 ila kwa bahati mbaya sababu ya utajiri haikuhesabiwa katika kumuengua.
Kamati iliangalia kuhusika kwakwe na mkataba wa Richmond, ikaona Lowassa hawezi kujinasua na kwa hivyo chama hakina sababu ya kumkumbatia mtu ambaye wakati wa kumuombea kura inabidi kuanza na maneno ya kusafishe.
Hichi ndicho wanachofanya Frederick Sumaye na wapiga debe wa Chadema.
Kingunge anaishambulia serikali nya Kikwete kwamba imesababisha uchumi kudorora, angekuwa mkweli angesema yote kwamba tatizo la ufisadi na mafisadi ambao wamekimbi CCM na kujificha kwenye upinzani ndio walioshiriki kuufanya uchumi udorore.
Kwa mfano ufisadi wa mkataba wa Richimond ulisababisha nchi kwenda katika mgawo mkali wa umeme kwa miezi 18, hiki ni kipindi kirefu sana, kinatosha kuhujumu uchumi kwani viwnda vingi vilisimama, shughuli nyinginezo za uzalishji (na huduma zilisimama kuufanya uchumi udumae).
Niliposikia Kingunge kaachana na ccm nikakumbuka matukio mawili, la kwanza siku moja nilimtembelea ofisini kwakwe Lowassa, na katika mazungumzo alinimbia, Mapunda Mhe Rais anaacha kuufuata ushauri wa mzee Ngombale anafuata ushauri wa waziri mmoja maarufu katika serikali ya awamu ya nne kutoka mikoa ya kusini, pamoja na taasisi moja nyeti.
Siku nyingine nilikwenda kwake mzee kingunge, mzee wangu ambaye nilikuwa na mazoea ya kumtembelea, akanidokeza habari kuna ujumbe ambao Rostam alimpa kumpeleke Rais Kikwete, Rais akamrudishia majibu kwamba mwambie Rostam, Mwenyekiti anasema jiuzulu ujumbe NEC.
Hii ni ishara kwamba wa walimweka kingunge kwa manufaa yao na walitaka kuutumia urafiki wao na Rais kufanya mambo watakavyo na si kufanya kwa misingi ya uongozi na uadilifu inavyotakiwa katika kutumikia wananchi.
Tangu ulipokamilika mchujo wa wagombea 38 na wa ccm na kupatikana kwa Dk. Magufuli, Kingunge amekuwa akilalamika kuoinyesha jinsi ambavyo matokeo hayakumfurahisha lakini maneno yake yanaonyesha amtetea mtu mmoja Lowassa na si wagombea wengine 37 walioshindwa na Magufuli.
Hii inamaana kwamba katika mchakato huo kama Lowassa angeshinda Kingunge asingelalamika kwamba taratibu zimekiukwa. Kingunge anamtetea mtu, anampigania mtu badala ya kupigania chama, amependa sana hadi anafikia chongo kuita kengeza.
Utashi wake binafsi unamfanya asahau kwamba ccm ni taasisi siyo mali ya kundi dogo. Kingunge akumbuke kwa nafasi yake aliyokuwanayo na muda aliokuwa ccm anafanana na mpishi aliyekuwa jikoni, ameshiriki mengi na kufanya mengi yaliyosababisha matokeo anayoyalaani sasa.
Kingunge anapolaumu serikali ya JK kutofanya vizuri kiuchumi, Je wakati wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere uchumi ulikuwa haukuyumba? Watanzania hawakupata taabu na adha nyingi za kukosa bidhaa muhimu? Mbona hakujitoa CCM kuthibitisha kwamba anawapenda watanzania kuliko chama.
Nimalize kwa kumshauri mzee Kingunge kwamba kama alivyoamua kupumzika iwe hivyo na apumzishe pia mdomo wake akiamua kuwa mpinzani binafsi watanzania hawatamuelewa.
Chanzo Tazama
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments