[wanabidii] Mshindi Jana Ni Anna Wa ACT..!

Monday, October 19, 2015


Ndugu zangu,
Jana kulifanyika kilichoitwa mdahalo wa wagombea urais, ingawa, kwa tafsiri sahihi ya mdahalo ule haukuwa mdahalo kama mdahalo tunamaanisha debate.
Nilichokiona mimi kwa uzoefu wangu nilioukusanya japo kwa uchache, ni mahojiano maalum ya jopo la wasomi na wagombea urais- Special Party Leaders Interviews. Hakukuwa na debate miongoni mwao. Kimsingi, maswali walioulizwa akina Anna Mghwira na Chifu Yemba yangeweza pia kutumwa kwa wagombea ambao hawakufika ili wayajibu kwa wakati wao.
Hata hivyo, kama ilivyo kwenye debate, hata kwenye mahojiano ya viongozi wa vyama wapiga kura hutaka kujua ni nani aliyeibuka na alama za juu.
Kwa jana mimi nampa Anna Mghwira 80% Hata kama kuna nyakati alilazimika kusoma majibu yake lakini alijieleza vizuri sana.
Na pengine Anna mwenyewe hajui, lakini kwa performance yake ya jana amechangia kutoa picha kuwa ACT kinaelekea kuwa Third Major Party kwa Tanzania. Naamini, jana kuna kura nyingi amezitumbukiza kwenye kapu la ACT. Ni kura za wana-ccm na Wana-chadema wasiomkubali John na wasiomkubali Edward. Wapiga kura hao jana wameliona kapu la kutumbukiza kura zao. Na tafsiri yake ni kuwa, tusije kushangaa kuona matokeo yatakayompa Anna kura zisizo za aibu, kura zenye kuanzia laki tano ..hata kama hatapata urais..
Ni mtazamo wangu.
Maggid.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments