[wanabidii] JAKAYA anaondoka, TANZANIA tabaki, ukimshambulia na kumchonganisha na wananchi ni UVIVU WA KUFIKIRI

Wednesday, October 28, 2015
Watanzania wengi wanapenda sana kumnukuu Mwl. Nyere katika majimbo mengi lakini hawapendi hata kidogo nukuu muhimu sana ya kuonya WATU WASIWE WAVIVU WA KUFIKRI.

Tabia hii kujaribu kumchonganisha rais Kikwete na Wananchi imechukua muda mrefu sana. Hata juzi Jumamosi wakati wa kufunga kampeni nadhani kila mtu aliwashuhudia Mbowe, Maarif Seif Sharrif, Hamad, Duni na Mbatia wakitumia muda mwingi Kupambana na Kikwete bdala ya kuawaambia wapiga kura uboira wa mgombea wao na udhaifu wa CCM.

Tumemshuhudia Dk. Magufuli akitembea nchi nzima isipokuwa majimbo matano tu, kueleza mikakati yake na at least kuonekana. Lowassa aliweza kufika mijini na wiki mbili za mwisho ndipo alijaribu kidogo kufika zaidi ya hapo.

Mimi ni miongoni mwa waliosema mapema kwamba Dr. Magufuli atachaguliwa kwa kura nyingi zaidi kwa sababu hiuyo baadhi ya watu wakakasirika kutokana na Kauli hiyo.

Ukawa walitumia muda wao zaidi kwa maeneo ambayo yenye watu wanaotoka ukanda ukanda mmoja wan chi na kuacha maeneo mengi ya nchi amabayo ni makubwa sana.

Ushindi kamwe usingepatiakana kwa kutegemea maeneo hayo. Tanzania ni Kubwa mno tusisahau jiografia ya nchi yetu, Jakaya anaondoka, Tanzania itabaki, ukimshambulia na kutafuta kumchonganishisha na wananchi ni UVIVU WA KUFIKIRI, ambao ni udhaifu wa watu wengi

Share this :

Related Posts

0 Comments