Ndugu zangu,
Hata mchana wa leo nilipokuwa kijijini Melela Kololo, kule Mvomero, Morogoro, sikuwa na taarifa za matokeo ya utafiti wa Twaweza kuhusu Uchaguzi Mkuu.
Nimefika Mjini Dar Es Salaam nimeukuta mjadala juu ya utafiti huo. Na kwenye TV usiku huu hata wasomi wetu nimewasikia wakitoa 'maoni' , sio ya kitafiti , juu ya utafiti uliotolewa.
Mwalimu wangu Chuo Kikuu aliniambia; tafiti hupingwa kwa tafiti. Ni matumaini yangu yatakuja matokeo ya tafiti nyingine iliyofanywa na wengine. Tafiti itakayoungana au kupingana na ya Twaweza.
Nao watueleze njia za kisayansi walizotumia katika kufikia matokeo yao. Ndivyo Sayansi inavyotutaka tuyapime mambo ya kisayansi. Nje ya hapo yatabaki kuwa ni maoni tu. Kila mmoja anayo haki ya kutoa maoni yake.
Swali, tafiti bora ni ipi?
Nikijitahidi kukumbuka nilivyofundishwa, ni kuwa, njia ya kuelekea kwenye tafiti bora inajengwa kwanza na hamu ya kutaka kujua jambo. Kisha unatengeneza maswali ambao tafiti yako ikusaidie kuyajibu.
Ukitoka hapo unachagua njia ya kuifanya tafiti hiyo': Qualitative/Quantitative, au zote mbili.
Baada ya hapo ndipo huanza kazi ya kukusanya taarifa ( Data). Ukishakusanya taarifa, unakuwa na empiri, kwa maana ya mzigo wa taarifa unaotakiwa uchambuliwe. Kuna makapi ya kuayaacha na mchele wa kuchukua.Ndipo baadae unapopata matokeo ya tafiti.
Na tafiti bora ni ile ambayo, matokeo yake yanaweza kupelekea kufanyika tafiti nyingine ambayo matokeo yake yanaweza kutofautiana na tafiti iliyofanyika. Nadharia hii inatokana na mwanafalsafa wa Kisayansi Karl Popper ( Falsifiability au refutability)
Kwa mfano, kama Taasisi ya Tahea imekuja na matokeo ya utafiti yenye kusema kuwa Iringa ni ya tatu kitaifa kwa utapia mlo, sababu za Tahea zaweza kusemwa kuwa ni kutokana na gharama za juu za pembejeo za kilimo.
Lakini, mwingine anaweza kufanya utafiti mpya akagundua, kuwa akina mama wa Iringa, ambao ndio wenye majukumu makubwa ya malezi, kwamba idadi ya akina mama hao wenye kushiriki ulevi wa pombe inaongezeka.
Hivyo, wanapoamka asubuhi, huona uvivu kuchuma mbogamboga kwa chakula cha watoto. Huona uvivu pia kupika chakula maana lazima pia waende shambani pia. Kwamba wengine hufikia hata kuwanywisha pombe watoto wao mapema asubuhi, na ukawa ndio mlo wa mtoto.
Hayo ni maoni ya Mwenyekiti wenu yanayotokana na niliyojifunza yenye kutokana na tafiti za Kisayansi...
Maggid,
Dar es Salaam.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments