VIJANA NA USHIRIKI KATIKA KULETA MABADILIKO YA KWELI KATIKA TAIFA LETU.
Habari za muda huu wanabidii.
Ninatumaini kuwa mu-wazima wa afya, na sote tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai aliotupatia. Zaidi ya yote taifa letu limekuwa likipitia nyakati nyingi sana za ukuaji wa kijamii, kiuchumi, kijeshi, na medania ya kisiasa.
Siwezi kataa kuwa mwaka huu utakuwa ni miongoni wa miaka ambayo historia imetokea na sisi tukiwa tunatazama, ndiyo maana nikasema kwa tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai aliotupatia.
Mwaka huu nilishiriki katika mchakato wa kutafuta kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kukiwakilisha katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kupitia jimbo la Maswa Mashariki. Binafsi kwangu ulikuwa ni ukomavu mkubwa kisiasa, na hata kufanya maamuzi.
Kama kijana, niliona kuwa ni vyema kabisa kushiriki katika uandikaji wa historia hii. Sehemu yangu ilikuwa ni ndogo sana, katika siasa za Tanzania baada ya kuwa nimeishia kwenye kura za maoni, lakini kwa watu Maswa Mashariki lilikuwa ni tukio la ushujaa, ushupavu, na kuvutia kwamba Chama Cha Mapinduzi kina vijana wanaoweza "Kusema Mambo kama Yaliyo!"
Vijana mwaka huu tumeshiriki kwa kiasi kikubwa sana katika siasa za Tanzania kuliko kipindi chochote kila. Mambo makubwa ninayoyaona, ili tuweza kuwa kichocheo kikubwa cha mabadiliko halisia, Vijana, pamoja na watu wengine wote, lazima tukubali kuwa UADILIFU, UCHAPAKAZI ULIOTUKUKA, UZALENDO, UTAIFA, na UMOJA ni mambo ambayo hayawezi kuwekwa rehani kwasababu ya maslahi ya wanasiasa.
Leo hii, niemamua kuwa weka pembeni ndugu zangu wengine ambao hamuangukii katika kundi la vijana, ila pia ninafahamu kuwa tupo ambao bado damu zetu zinachemka kama za vijana, hivyo hatutakuwa tumeachana sana.
Mie kama kijana, nimekataa kutumia na wanasiasa, kwa sababu moja kubwa...wanasiasa walio wengi wana-umri unaanzia miaka hamsini (50) kwenda mbele... maamuzi mengi ambayo wakuwa wakiyafanya, au watakayo yafanya yanamadhara ya zaidi ya miaka 15 katika maisha ya kila mtanzania. Hivyo ninatoa rai kwa viongozi wetu kuwa ili vijana tuwezi kuwa sehemu ya mabadiliko, ni lazima VIONGOZI WETU watuone sisi kama WASHIRIKA KATIKA KULETA MABADILIKO YALETAYO MAENDELEO KWA VIZAZI VYA SASA NA VIJAVYO. Si vinginevyo.
Kwa sasa wanasisa, na nyakati za nyuma watutumia vijana kwa kutuletea hoja nyepesi nyepesi ambazo hazina lengo la kumkombo kijana, mama, baba, babu au mtoto wa Tanzania. Kuhusu vijana, ninatamani kuona tunakuwa sehemu ya MABADILIKO kwa kuwa na viongozi, au serikali zinazohakikisha kuwa MAZINGIRA YA KUFANYA UJASIRIAMALI ni RAFIKI WA VIJANA WOTE...KUONA SERIKALI INAAZISHA BUSINESS INCUBATION CENTRES NYINGI NCHI NZIMA..
Mabadiliko ya kweli si kutoa serikali moja na kuingiza serikali yingine madarakani. MABADILIKO YA KWELI, ni kuhakikisha kuwa maisha ya MTANZANIA, Mkazi wa Tanzania, au mwekezaji anakuwa na uwezo wa kufanya shughuli zake katika mazingira rafiki, na kuona njozi zake za mafanikio zinafikiwa...ina tamani kuwa na ile AMERICAN DREAM HAPA TANZANIA... KUWA NCHI AMBAYO NJOZI KUWA KITU HALISI KUTOKANA NA FURSA ZA NDANI NA NJE.
KIONGOZI ATAKAYE FANIKIWA KUNIFANYIKA MAMBO HAYA NDIYIE MWANA-MABADILIKO WA KWELI.
ILA KIONGOZI AMBAYE ANAPIGIA CHAPUA KUONDOA CHAMA FULANI MADARAKANI, AU KUHAKIKISHA KUWA CHAMA FULANI HAKISHIKI MADARAKA KWA SABABU YA CHUKI KIONGOZI HUYO AU CHAMA HICHO HAKIFAI HATA KUWA KATIKA ORODHA YA VYAMA, AU VIONGOZI WANAOTAKIWA KUKUMBUKWA KATIKA HISTORIA ZA NCHI YETU.
SASA, kwa sababu hapo juu nimekwisha onyesha kuwa mimi ni mwanachama wa Chama gani, ninaomba kumbukumbu zionye kuwa, ninaamini MAGUFULI, JOHN POMBE, anaweza, ana udhati, uadilifu, uzalendo, wa kuweza kufanya njozi za vijana wengi wa tanzania zinatima.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
Share this :
0 Comments