[wanabidii] TAFAKARI NA CHUKUA HATUA

Friday, September 18, 2015
CCM wangekuwa wametawala vizuri muda huu
kazi yao ingekuwa rahisi sana wangekuwa
wanazunguka kwa wananchi na kuwaambia;

ONENI mahakama ya rushwa inavyofanya
kazi.


ONENI reli ya kati ilivyoimara na usafiri wa
treni kwa ujumla.

ONENI elimu bora tuliyoianzisha.

ONENI elimu bure tunayowapatia.

ONENI sekta ya viwanda inavyoshamiri.


ONENI walimu walivyo na maisha bora.

ONENI wanafunzi wote wana mikopo na
mabumu hayachelewi.


ONENI zahanati katika kila kata.


ONENI uzalishaji ulivyokuwa.

ONENI tumekuwa tukitoa milioni hamsini kila
kijiji.

ONENI kilimo cha kisasa.

ONENI bandari zetu zilivyobora.

ONENI sarafu ya Tanzania ulivyopanda
thamani.


ONENI maisha bora kwa kila mtanzania
tulivyofanikiwa.


ONENI flyovers dar es salaam

ONENI madini yetu yanavyonufaisha
watanzania.

ONENI hakuna fisadi anayezunguka mtaani
wote wapo jela

ONENI kilimo cha mkonge kilivyokuwa.

ONENI wakulima wa pamba walivyo na
maisha bora.


ONENI wakulima na wavuvi walivyo na maisha
bora

ONENI hiki ONENI kile, hii ndiyo ingelikuwa
kazi ya CCM kila sentensi wangeanza na
ONENI halafu ndiyo wanafuata na ilani mpya
lakini kutokana na utawala wao mbaya kila
kitu hapo juu wanaanza na TUTAFANYA kana
kwamba nchi hii miaka yote ilikuwa
ikiongozwa na nyani vitu vyote alivyovianzisha
Nyerere ikiwamo viwanda elimu bure nk
wamevivuruga sasa wanataka kuvirudisha
mliviharibu kwanini kama si kupotezeana
muda?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments