Sikubaliani na baadhi maaskofu wa aina ya Kajima kwa kuwa baadhi yao wameshiriki kuvunja ndoa nyingi na kuzifilisi baadhi ya familia huku wao wakijitajirisha kwa kutumia migongo ya ujinga wa baadhi ya waumini wao.
Sikubaliani nao kwa kiasi kikubwa watu waliojipachika uaskofu na unabii wakati nasfi zao zimejaa mambo machafu. Pia nawachukuia watu waojipachika majina ya uaskofu kwa lengo la kuwaghilibu watanzania wenzao, ambao wamekumbwa na misongo ya maisha, shida za kila aina ambao hujikuta wakiangukia mikononi mwa hawa matapeli wanaojifanya wana uwezo wa kuwaondolea shida zao.
Wanajiita Maaskofu, manabii, mitume, mitume wa fedha, nk ni kejeli na fedheha kwa Mungu! Wanajifanya watumishi wa Mungu lakini kumbe wamejaa roho ya kutumikiwa. wanasema wao ndio wafuasi wa Kristo lakini hawafuati mafundisho na maisha ya Kristo.
Wanasema wanachunga kondoo wa Bwana wakati wao ndio mbwa mwitu wakali wanaotafuna kondoo za Bwana na kuwalazimisha watu kutoa kila kitu walichonacho hadi wanafilisika lakini kumbe wao wanaishi ufahari mkubwa! Wanalaumu serikali kwa ufisadi kumbe wao ndio mafisasi wa mali za kanisa na waumini wao. Hawana huruma hata kidogo nia yao ni kula na kushibisha matumbo yao kwa vijisenti vya maskini!
Umewahi kuwasikia hata siku moja wakiweka mikakati makanisani mwao ya jinsi ya kuwasaidia maelfu ya maskini na yatima tuliono? Kati ya vitu wasivyopenda kusikia watu hawa ni huduma kwa watoto yatima, wajane na walemavu.
Kwa tabia hiyo ya maaskofu hao hujipatia fedha nyingi kwa njia ya sadaka, mavumo makubwa kutoka waumini wao ambayo huwapa kiburi na kujiona miungu watu na kutoona haya kuwasema maaskofu wa ukweli, walioupata uaskofu wao darasani na kwa uwezo wa mungu muumba mbingu na ardhi.
Sikublini na maakofu hawa matapeli kwa sababau baadhi yao tunafahamu vizuri historia zao na maisha yao kwa ujumla, histori ya maisha machafu na tabia za kishetani ndio maana wanakimbilia katika ulokole ili kusafisha historia zao ndani ya jamii, huku baadhi yao wakifanikiwa kuanzisha hata makanisa lakini ukiangali kwa ukweli hayana hata hadhi ya kuitwa makanisa.
Naamini makanisa kama haya ya kina kajima na maaskofu wengine kama kina kajima ndio yale ya manabii wa uongo walioelezwa na yesu kristo, mbele ya wanafunzi wake kwamaba watatokea mwisho wa dunia na wengi watajifanya wana uwezo wa kuponya. Makanisa haya yanayoibuka kama uyoga hayana tofauti na yale yaliyotokea Uganda amabo Kibwetere aliwafungia ndani waumini wake na kuwateketeza kwa moto.
Rai yangu kwa serikali upo umuhimu mkubwa sasa, pamoja na uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa katiba yetu lakini mamaraka ya usajili wa makanisa na misikiti iwe makinia kwa watu wanaojianzishia madhebu kila kukicha kwani mengine yamekuwa yakiwatia umasikini wa Tanzania na kuleta uchochezi hapa nchini.
0 Comments