Ninaendelea kumsikiliza Mheshimiwa James Mbatia akiongea na waandishi wa habari. Yako mambo ya ajabu ambayo nimemsikia akiyaongea.
1) Midahalo:
Mbatia anasema midahalo inabidi ifanywe baina ya viongozi wa vyama vya siasa na si wagombea. Mtu ukijiuliza haya: Vyama vimeandaa ilani za Uchaguzi. baadaye Ilani hizo zikakabidhiwa kwa wagombea ili wainadi. Hawa ndio wasemaji wakuu na ndio wanajiandaa kutekeleza ilani hizo. Watu wanataka kujua kama wanafanana na ilani hizo. Watu wanataka kuwapima uwezo wao na tabia zao. ndiyo hasa maana ya midahalo. Lakini tunajua wote kuwa kama ni kuiga hata midahalo hii tukiifanya tutakuwa tunaiga. Tunaweza kuanzia Kenya katika uchaguzi waliomaliza karibuni. Walikuwa na midahalo na walishiriki wagombea. Tunaweza kuangalia marekani wakati huu. Wagombea wanajitahidi kujinadi na wanapimwa. Iweje badala ya kuwakutanisha wagombea Tanzania tuwakutanishe wengine? Mwaka 2005 nakumbuka CCM walimzuia Mgombea wake asishiriki midahalo. Tulijua kuwa alikuwa mdhaifu wa hoja na hii ni kweli. kweli kabisa. lakini bado CCM haikutaka kuleta watu wasiohusika na utekelezaji wa ilani.
Sasa mbatia anaweza kutweleza mgombea wa UKAWA ana shida gani? kama ana shida kwanini walimuweka? Lakini najiuliza Mbatia akiisoma Katiba yetu anaona Chama kina nafasi gani kumuingilia Rais katika utekelezaji wa majukumu yake? nafasi pekee waliyo nayo ni kumnyang'anya kadi ya chama napo sijui inaweza ikawaje mtu mwenye vyombo vya mabavu.
2) Hoja ua UDINI:
Mgombea lowasa anasemekana kuingia Kanisani na kusema maneno mawili a) naomba mniombee 2) Mnichague mimi ili zamu hii tuwe na Rais Mlutheri
Mbatia katika kurusha shutuma anaishutumu CCM kwa kutumia a) hapo juu tu na kuiacha pembeni hoja hasa ya ULUTHERI. najiuliza anafikiri watanzania hawakumbuki kilichosemwa au kasahau yeye? Hajui kuwa bila kujibu hoja anakuwa amebakiza maswali ambayo wapiga kura ndiyo watakayotumia kule chumbani na kutoka wakinyosha vidole kumbe wamepigia wa kidole?
3) Ukanda/ukabila:
Ni kweli watu wanaongelea CHADEMA kuwa chama kinachokumbatia ukanda. Wanaosema hivyo wanazingatia kinachoonekana yaani nguvu kubwa wanayoikusanya kwa kuwaweka pamoja watu wa kaskazini yaani Mbatia, Mbowe, Sumaye lowasa na wengine. Hata humu mtandaoni utakuta wanaounga mkono kila kinachopendelea UKAWA na kutukana kila kinachoipinga utaunusa ukanda. Badala ya kujibu hoja ili kujisafisha anawashambulia wanaosema bila kusema wanasema nini. Niliwahi kuandika kuhusu udini tanzania na kubaini uko wa namna mbili 1) Kuna wanaotenda udini. 2) Kuna wanaokemea udini. Wale wanaotenda udini wanakuwa wepesi kuwakemea wanaosema udini kuwa ni wadini. mfano kiongozi anateua wanadini wake kwa wingi. Wakimsema anasema acha udini. Sasa mbatia haoni kuwa wanaosema wanasema ukanda huo bali anakurupuka kuwasema wanaomwonyesha tatizo.
4) Kuhatarisha amani:
Mbatia kwa maelezo yake unaweza kusema labda matokeo ya uchaguzi yameishatangazwa na watanzania wameishaamua UKAWA iongoze ila CCM inakataa kukabidhi madaraka. Anaonyesha jinsi watanzania walivyokwishaamua kufanya mabadiliko kupitia UKAWA. Hajaona kuwa kuna wanaoona mabadiliko kupitia CCM. na kuwa tunasubiri Watanzania waamue wanataka mabadiliko kutokea wapi kati ya CDM, CCM ACT etc. Haonyeshi kuamini kuwa jambo tofauti linaweza kutokea. Naamini mkutano huu aliokuwa nao haukuwa mkutano wa kampein. maana yake alistahili kuwa lialistic. Mimi nikaanza kuwa na wasiwasi kuwa ikitokea matokeo yakawa kinyume mbatia anaweza kuwa mmoja wa watakaoongoza ghasia. Hapa ndipo ninapoona hatari. Hatari ya kuiyumbisha amani.
Wakati fulani humu niliwahi kumtaja Mbatia kama mmoja wa viongozi wanaoweza kuliongoza taifa hili. Kuna wakati niliwahi kumsikia akisema '----- vyama hivi vinavyojiita vilipigania uhuru' Neno hili lilinishtua nikasema huenda lilimponyoka (tongue slip). Mtu asiyekili kuwa TANU na ASP (CCM) vilipigania uhuru wa taifa letu watu wa namna hii wanakuwa wamenunuliwa. mifano ipo mmoja wapo ni Tshangilai wa Zimbabwe. Watu hawa ni wa hatari. mara zote wananchi waliamua kuendela na vyama vyao mpaka viaminike hivi wasijeingiza watawala toka nje. Mkutano wa leo na waandishi wa habari umenifanya nijiulize kama nilikuwa namfahamu au sasa ndio naanza kumfahamu
Elisa Muhingo
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments