[wanabidii] Kuna Vitatu Muhimu Kwenye Chaguzi, Kura Ya Maoni Ni Kimojawapo..!

Wednesday, September 23, 2015


Ndugu zangu,

Matokeo ya kura ya maoni ya Twaweza yaliyotangazwa jana ni gumzo kubwa.
Ni kawaida kabisa kwenye Sayansi ya siasa. 
Maana, kwenye chaguzi, watu huwa na shauku ya kufuatilia habari zenye vitu vitatu;
1. Kashfa, na hasa inapowahusu wagombea.
2. Kauli za ' Utumbo' napo pia ni pale mgombea anapoongea jambo ambalo hakupaswa kulisema hadharani.
3. Kura za maoni. Hili nalo huvutia sana watu.

Kwa hilo la kura ya maoni limekaa kisaikolojia sana. Ndugu yangu Profesa Kitila Mkumbo ameliweka vizuri kwenye makala yake ya The Citizen leo Jumatano; "Should politicians worry about opinion polls?" Kwamba je, wanasiasa wanapaswa kuwa na wasiwasi juu ya kura za maoni? Ameuliza Profesa Kitila Mkumbo na kujaribu kulifafanua hilo.

Kwangu mimi, jibu la swali hilo ni la dhahiri, ni NDIYO.

Mwanasiasa anayepuuzia kura za maoni huyo si mwanasiasa. Unaweza kupuuzia utabiri wa wanajimu lakini si kura ya maoni iliyotokana na utafiti wa Kisayansi.

Naamini, kabisa, kuwa UKAWA kuna watu makini ambao kwa sasa hawawezi kulala wakijitahidi kutafuta namna ya kupunguza madhara ya kura ya maoni iliyoendeshwa na TWAWEZA. Ni kwa vile, kisaikolojia, maamuzi ya wapiga kura huathiriwa kwa kiwango kikubwa na kura za maoni. Kuna ambao hukatishwa tamaa, na kuna ambao huongezewa imani juu ya wagombea wao.

Katika muda uliobaki, matokeo ya kura nyingine ya maoni yiliyoendeshwa kisayansi yakitolewa kabla uchaguzi mkuu, na yakiipa Ukawa na mgombea wao Urais alama za juu, basi, yatatakuwa na athari chanya kwa wagombea wa UKAWA, yatawaathiri pia kisaikolojia wapiga kura kwa faida ya UKAWA.

Kwa hali ilivyo sasa, walio UKAWA makini, wanahitaji kusikia ripoti nyingine ya kura ya maoni ikitolewa na taasisi nyingine inayoaminika, na yenye kuonyesha picha tofauti na ripoti ya TWAWEZA.

Na tusubiri tuone.

Maggid.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments