[wanabidii] EDWARD LOWASA AOKOLEWA NA MWANZILISHI WA TANU

Wednesday, January 14, 2015
EDWARD LOWASA AOKOLEWA NA MWANZILISHI WA TANU
MWANASIASA mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema suala la matumizi ya fedha kwa viongozi wa kitaifa na kimataifa lilikuwapo katika karne nyingi zilizopita. Kutokana na hali hiyo, amesema anashangazwa na baadhi ya viongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kulishupalia suala hilo na hata kuwanyooshea vidole wanachama wengine
Kingunge amefunguka na kusema kuwa hakuna aliye msafi katika makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliojitokeza kutaka kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuwa wote wanatumia fedha na kufanya faulo mbalimbali katika kusaka nafasi hiyo nyeti katika uongozi wa nchi, kinyume cha maadili hivyo hakuna wa kunyooshea mwingine kidole.
i.Kingunge alisema ni wazi pamoja na kuwapo kwa suala hilo, lakini halipaswi kuwa ajenda kwa sasa ila kinachotakiwa ni kuangalia namna gani ya kushughulika nalo bila kuwapo mapambano dhidi ya mtu mmoja.
Habari imekuwa ni pigo kwa vigogo wengine wa chama hicho walioanza kumsonda kidole ndugu Lowasa kwamba anatumia pesa nyingi kwenye kinyanganyiro hicho kiasi cha habari kusambaa kuwa amefunguwa uanachana wa CCM kwa miaka 11. Iwapo Kingunge ameweza kutetea uhalali wa kutumia mapesa ndani ya chama hicho basi Ndugu Lowasa itakuwa njia nyeupe kwenda ikulu kwa sababu UKAWA bado wanakigugumizi atakayetoa mwakilishi wao au awe Slaa, mbowe, Lema, ama Lissu ambapo kwa upande mwingine wanaona mbatia ndiyo chaguo pekee zaidi ya Lipumba ambaye amegombea zaidi ya mara tano kwa nunge.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments