Na Ananilea Nkya
Nimeisikiliza hotuba Dr Slaa kwenye youtube--nimeungana na wananchi ambao wamesema Dr Slaa kwa kujua au kwa kutokujua amekubali kutumika kuyumbisha maelfu ya wananchi wanaotaka mabadiliko nchini na kwa hiyo amejichafua mbele ya Watanzania.
Dr Slaa anapaswa kujua kwamba mabadiliko ni lazima kwa sasa na hayazuiliki tena maana nchi ilipofikia sasa Septemba 2015, wenye ari kubwa ya kuleta mabadiliko ni wananchi wenyewe kupitia sanduku la kura hapo tarehe 25 Oktoba.
Pengine Dr Slaa hakujua kuwa wananchi wanaotaka mabadiliko ya uongozi nchini walikuwa wameshamsahau maana tangu alipoacha kuonekana hadharani hasa wakati wa kumtambulisha Edward Lowassa kama mgombea Urais wa UKAWA--muungano wa vyama vinavyopigania kuingia madarakani vikiwa na ajenda ya kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi, wengi walishajua kuwa Dr Slaa hayupo tena upande wa wananchi.
Alichokisema Dr Slaa kwenye hotuba yake ya kile alichokiita 'kuachana na siasa za vyama' ni kajichafua yeye mwenyewe na kuharibu heshima aliyojijengea kwenye jamii.
Kwa mfano Dr Slaa alisema eti aliweka msingi kwamba angemkubali Edward Lowassa kugombea Urais iwapo angeondoka CCM na mtaji wa wabunge 50 kuhamia UKAWA ili wagombee ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na NLD- vyama vinavyounda UKAWA.
Hivi Dr Slaa aliona vijana wanaochakarika kwenye vyama vinavyounda UKAWA wao hawataki kuwa wabunge? Hawastahili nao kufaidi mshahara wa shilingi milioni 10 kila mwezi na kiinua mgongo cha zaidi ya shilingi milioni 200 baada ya miaka mitano ?
Hebu fikiria wabunge wa CCM ambao wengi wamekuwa bungeni miaka kumi, ishirini wengine miaka thelathini na zaidi. Ni matajiri kiasi gani leo hii? Hivi watu wa aina hiyo kweli wanaweza kuondoka kwenye chama chao kwa wingi kiasi hicho na kuamua sasa kupigania kuondoa mfumo unaowatajirisha wao ili wananchi wengi masikini nao watajirike?
Watakuwa na shida gani wakati kwenye chama chao hata kama mtu umekosa kuteuliwa kugombea ubunge malofa wakishaichagua CCM serikali ya CCM inawagawia kazi za ulaji watu waliokosa ubunge? Kwani wewe hujamsikia Mgombea Urais wa CCM Dr Magufuli akiwatangazia wale walioanguka kwenye kuwa za maoni ubunge CCM kwamba wasijali anazo kazi tele za kuwapa akichaguliwa Rais?
Kwa mtazamo wangu--walioamua kuondoka CCM na kujiunga na UKAWA kama kweli dhamira yao ni kushirikina na UKAWA kupigania kuingiza serikali ya UKAWA madarakani ili kuandika Katiba Mpya ya wananchi--watu hao wanastahili pongezi maana watakuwa wamefanya maamuzi magumu na muhimu ya kuwezesha wananchi wengi kuondoka kwenye umaskini unaosababishwa na serikali ya CCM.
Hivi Dr Slaa kweli anadhani mabadiliko ya kuchagua serikali itakayoandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi yatatokea nchini kwa wabunge wengi wa CCM kuondoka CCM –kujiunga UKAWA--wabunge ambao waliizika Rasimu ya Katiba ya wananchi pale Dodoma 2014 huku wakiwa wanalipw akila mmoja shilingi laki tatu kila siku kwa takriban miezi mitatu?
Hivi Dr Slaa hajui kwamba wanaotaka mabadiliko ni mamilioni ya Watanzania wakiwepo wanachama wa CCM wanaoumizwa na umaskini ambao chimbuko lake ni mifumo iliyowekwa na serikali ya CCM--mifumo inayotajirisha watawala wachache huku mamilioni ya wananchi wakiwa mafukara?
Kwa mtazamo wangu, wananchi wengi wakitafakari hatua aliyochukua Dr Slaa na maneno aliyoyazungumza hadharani watabaini kuwa Dr Slaa amejidhihirisha kuwa ni mtu mbinafsi.
Zaidi watabaini kuwa Dr Slaa pengine aliingia kwenye upinzani akidhani siasa ni kama kazi nyingine. Kumbe siasa hasa kuwa kwenye chama cha upinzania ni kujitoa hata kama kuna kuumia kiasi gani –hadi lengo la ukombozi wa pili wa taifa hili--ukombozi wa kuondoa mifumo inayowafukarisha wananchi ing'olewe.
Kwa maoni yangu, kama Dr Slaa angekuwa ameingia kwenye siasa kupigania ukombozi wa wananchi--kamwe asingekubali kukaa pembeni sasa--tena baada ya yeye mwenyewe kukubali Lowassa aingie UKAWA mradi awe ni mtaji na si hasara. Kibaya zaidi asingekuwa upande wa watawala wanaofukarisha wananchi eti kwa sababu Lowassa alishindwa kuleta UKAWA mtaji wa watu wa kugombea ubunge.
Pengine Dr Slaa amekuwa na tafsiri finyu kuhusu mtaji wa siasa. Siamini kuwa vyama vinavyounda UKAWA vina uhaba wa watu wenye uwezo wa kuwa wabunge. Hivyo mtaji muhimu ambao Dr Slaa angeutaka kwa Lowassa ni wapiga kura. Angejiuliza je huyu Lowassa anakubalika kwa wapiga kura?
Jibu kama Lowassa anakubalika kwa wapiga kura au la Watanzania wenyewe wanalo jibu na hadanganyiki mtu hapo. Watanzania wanaomuona Lowassa anafaa kuongoza Tanzania mafuriko. Huyo mtaji wa wapiga kura ambao Lowassa ameongeza UKAWA ndicho kinachowasumbua watawala.
Tena Watanzania wanaomuunga mkono Lowassa hawajakosea maana hata Mwalimu Nyerere alitamka hadharani mwaka 1995 kwamba Lowassa ni mtu mwenye dhamira na uwezo wa kuiongoza Tanzania.
Isitoshe wananchi wanamuona Lowassa kuwa ni mtaji muhimu maana kwa kuhama CCM amehamasisha nguvu kubwa ya umma katika kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa wananchi.
Dr Slaa alisema eti kwenye familia yake wanakula mhogo na maharage. Hivi familia inayokula mhogo na maharage (yaani kwa sababu ya umaskini wa kikwelikweli) inaweza kumruhusu baba ambaye alijibainisha kuwa ni kamanda wa mapambano ya wanyonge awageuke mamilioni ya Watanzania ambao hata mhogo na maharage hawapati na hivyo siku nyingine hulazimika kulala njaa?
Kama Lowassa angeingia CHADEMA na asigombee Urais badala yake CHADEMA na UKAWA wangemteua Dr Slaa kugombea Urais, je Dr Slaa angetamka maneno aliyoyatamka? Hata kama Dr Slaa angekuwa na uadilifu kama malaika angetoa kauli zinazofanana na zile wanazotoa watalawa wa CCM dhidi ya mamilioni ya Watanzania wanaotaabika kwa umaskini?
Hivi Dr Slaa ameamua kuungana na serikali ya CCM kudanganya wananchi kwamba tatizo la umaskini unaosumbua mamilioni ya Watanzania chanzo chake siyo serikali ya CCM bali ni Lowassa na hivyo Lowassa akiingia madarakani uma ufisadi utaongezeka nchini?
Kimsingi Watanzania wa leo HATUDANGANYIKI. Zaidi sana Mungu wa wanyonge ni mnyofu sana hatawaacha Watanzania mwaka huu—mwaka wa mabadiliko.
Ninawatia moyo Watanzania wote mkiwepo wana CCM mnaoumizwa na hali ya umaskini miongoni mwa wananchi wengi nchini kwetu msikate tamaa wala kuogopa kama akitokea kiongozi mwingine wa UKAWA akageuka wananchi kama Dr Slaa na Prof Lipumba kabla ya uchaguzi mkuu tarehe 25 Oktoba 2015 ninyi songeni mbele, mabadiliko yanawezekana.
Kimsingi ni kila mtu kutambua kuwa kuna njama nyingi zinazofanyika kwa lengo la kuvuruga wananchi ili waogope au wapuuze kufanya mabadiliko.
Sote tuwe macho, hakuna kuchoka, hakuna kuogopa .Mabadiliko ni lazima hayazuiliki. Mungu ibariki Tanzania.
Narudia kusema mimi sina chama chochote cha siasa ninachofungamana nacho. Ninachopigania ni maslahi ya mamilioni ya Watanzania masikini (malofa) kwa utawala mbovu wa serikali ya CCM.
Ninaruhusu mwenye kutaka kuchapisha makala hii afanye hivyo maana historia itatuhukumu mmoja mmoja na kama kundi linalopigania mabadiliko Tanzania.
Kwa maswali niandikie: ananilea_nkya@yahoo.com
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Wed, 9/2/15, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Mtikisiko
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, September 2, 2015, 2:29 PM
Mtikisiko
Waandishi Wetu
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema),
Dk. Wilbrod Slaa, amevunja ukimya kwa kueleza kile
kilichomsukuma
kujiuzulu wadhifa huo, sambamba na kujivua uanachama wa
chama hicho.
Katika kuvunja kwake ukimya huo, Dk. Slaa aliweka hadharani
namna
viongozi wenzake ndani ya Chadema, akiwamo mwenyekiti wao,
Freeman
Mbowe, Makamu Mwenyekiti Profesa Abdallah Safari
walivyoyumbisha
kusimamia misingi ya namna ya kumpokea Waziri Mkuu
aliyejiuzulu kwa
kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond, Edward
Lowassa.
Mbali na hayo, mengine aliyoweka wazi ni namna Lowassa
alivyoratibu
mipango yake ya kuhamia Chadema akiwa bado CCM, akifanya
hivyo kwa
kumtumia Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
Gwajima.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Gwajima ndiye "mshenga" wa
Lowassa kwa Chadema
na kati ya hoja alizozitumia kumshawishi Dk. Slaa kumkubali
Lowassa ni
kwamba, mwanasiasa huyo aliyeokosa urais CCM, anaungwa mkono
na Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na ndani ya Kanisa
Katoliki,
maaskofu 30 kati ya 34, wamehongwa na wamemkubali
Lowassa.
Ilivyokuwa na Kama ambavyo wahenga wanasema kimya kingi
kina mshindo,
ndivyo ilivyokuwa kwa kimya cha Dk. Slaa. Mshindo wa kimya
hicho ulianza
kujidhihirisha mapema, katika Hoteli ya Serena, jijini Dar
es Salaam,
alikofanyia mkutano huo, ambapo mpaka saa saba mchana idadi
kubwa ya
waandishi wa habari walikuwa tayari wamefika katika eneo
hilo, kushiria
kuwa tukio hilo litakuwa na ukubwa wa aina yake.
Dk. Slaa aliyewasili ukumbi wa mkutano saa 8:05 mchana,
jana, Jumanne,
aliweka bayana uamuzi wake wa kuzungumza na waandishi wa
habari,
akisema, kwa kuwa ikifika mahali ukweli unatakiwa kusemwa ni
lazima
usemwe, kutokana na upotoshwaji uliofanywa na watu
mbalimbali wakiwamo
baadhi ya viongozi wakuu wa Chadema, kwamba alikuwa
amepumzishwa
(likizo) na viongozi wa chama hicho.
"Nataka nianze na kusema mimi sikuwa likizo, sikupewa na
mtu yeyote,
niliamua kuachana na siasa Julai 18, 2015 usiku saa tatu,
baada ya kuona
yanayofanyika ndani ya chama changu sikubaliani nayo,"
alisema Dk.
Slaa.
Alisema alishiriki katika majadiliano ya kumakribisha
Lowassa ndani ya
Chadema lakini kwa kuweka misingi ambayo chama kilitakiwa
kwanza
kuizingatia kabla ya kufikia uamuzi wa kumkaribisha, baada
ya kukatwa
katika mbio za kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
"Baada ya tarehe 11 Julai, Lowassa alipokatwa mshenga wa
Lowassa,
Askofu Josephat Gwajima alinipigia simu kuniambia sasa kule
Dodoma mambo
yameisha, nikamwambia awasiliane na Mwenyekiti (Mbowe),
tukawasiliana
na naye baadaye tukakutana naye, nikawaeleza msimamo wangu
kwamba ni
lazima kusikia mtu ana nini, tukakutana na vijana wake ili
tujue ana
nini," alisema na kuongeza; "Nikasema msingi wa kwanza
ni lazima
atangaze kutoka CCM, akijiondoa aseme anakwenda chama gani,
na atumie
nafasi hiyo kujisafisha na tuhuma zote zinazomkabili katika
nchi hii,
kwa sababu Chadema kimeaminika, ukipokea mtu ambaye
hajajisafisha
unakuwa unapokea na uchafu wake. Hilo halikufanyika mpaka
alipopokewa
Julai 28. Siwezi kumsafisha mtu ninayekaa naye meza
moja."
Dk. Slaa anasema msingi wa pili aliokipa chama chake kabla
ya kumpokea
ni kupima kama Lowassa ni rasilimali (asset) au mzigo
(liability) kwa
chama hicho, kwa kuwa walikuwa wameambiwa kwamba angekuja na
viongozi
wengi kutoka CCM. "Nikawauliza anakuja na nani, yeye peke
yake au na
wafuasi, na kama wafuasi ni wa aina gani, vijana wa boda
boda
wanaoshabikia tu au ni viongozi serious (makini). Nikaambiwa
anakuja na
wabunge 50, wenyeviti wa CCM mikoa 22 na wenyeviti wa wilaya
88,
nikakiri hili litakuwa tetemeko, nikahitaji kupewa majina,
Katibu Mkuu
makini hawezi kupokea idadi tu, na tulikuwa tunakwenda
kwenye uchaguzi
wa kura za maoni, ilikuwa lazima nijue nani anagombea wapi,
vinginevyo
uta – destabilize (utayumbisha) chama," alisema na
kuongeza kwamba;
mpaka chama hicho kinampokea Lowassa hakuna hata moja kati
ya misingi
hiyo iliyotekelezwa.
Kuhusu ushiriki wake katika kikao cha kumpokea Lowassa,
alisema aliombwa
kuitisha kikao cha Kamati Kuu ya dharura, lakini akaeleza
msimamo wake
kwamba hajapata jibu la upembuzi kama Lowassa ni mtaji au
mzigo.
"Asubuhi ya Julai 27, Mwenyekiti alinipigia simu
kunieleza sijaridhika
akaomba tukutane asubuhi tuzungumze ili tusije
tukatofautiana na
Mwenyekiti, kwangu mimi tangu mwaka 2004 sijawahi
kutofautiana na
mwenyekiti, tulifika pale akiwepo Tundu Lissu, na mshenga
wake Gwajima,
tukabishana tangu saa 3 asubuhi mpaka saa 9 alasiri, wapo
hapa waseme
kweli, mimi sikukubaliana nao tangu mwanzo, nawaomba
viongozi wangu wawe
wanyoofu na wenye hofu ya Mungu," alisema.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, baadaye walitakiwa kwenda nyumbani
kwa Lowassa
lakini alikataa akisema hawezi kwenda nyumbani kwa mtu wa
CCM katika
mazingira ya u-Katibu Mkuu wa Chadema. Aliongeza kwamba
baada ya hapo,
iliundwa kamati ya watu wachache kumshawishi (Slaa), ambayo
ilikaa tangu
saa 9 mpaka saa 12 jioni lakini akawapa masharti yale
yale.
"Tuliporudi kwenye kikao taarifa ya kikao kile
haikutolewa. Nikaandika
barua ya kujiuzulu nikampa Makamu Mwenyekiti Profesa Safari
akaichana,
nikaandika nyingine nikampa Makamu Mwenyekiti Zanzibar,
akaniambia Dokta
usihangaike mambo haya yamepangwa," alisema.
Akizungumzia watu waliokuja Chadema, alisema wote wamekuja
wakiwa
makapi baada ya kuwa wameshindwa kwanza kwenye mchakato wa
awali wa CCM
(kura za maoni) na hata huko walikotoka si wasafi. "Watu
kama Sumaye
hawakuwa safi, mimi mwenyewe nilimwita fisadi bungeni,
alichukua Shamba
la Magereza Kibaigwa, na yeye mwenyewe alifikia hatua ya
kusema CCM
wakimteua Lowassa yeye atahama chama, sasa yuko naye, najua
dhambi
haihalalishiwi na dhambi nyingine, lakini maneno hayo
yalitamkwa na
nani, Watanzania walimwita Sumaye ziro," alisema.
Aliendelea kuwaponda wana CCM waliohamia kuwa ni kama makapi
ambao
hawataongeza thamani yoyote kwa chama hicho akiwataja Mgana
Msindai na
Matson Chizii kuwa ni sehemu ya makapi ambayo hayataongeza
thamani
yoyote kwa Chadema. "Kuna watu wanasema ondoa CCM kwanza
hata
ikiwezekana kuweka mkataba na shetani, mimi ni Padri
Mkatoliki, hata
kama nimestaafu, nikubali kuweka mkataba na shetani mradi tu
niondoe
CCM. Unaondoa CCM kwa program serious na watu makini au
unaondoa na watu
wale wale?" alihoja Dk. Slaa.
Chadema na tuhuma za ufisadi Mbali na kuhoji endapo
waliohamia Chadema
kutoka CCM wameongeza thamani yoyote kisiasa; Dk. Slaa
aliyesimama imara
akizungumza kwa saa 1.32 alisema; "Chadema iliaminika
miongoni mwa
Watanzania kwa kutoyumbishwa na kusimamia uadilifu. Sasa leo
Chadema
wanathubutu kusema etu usimtuhumu mtu? Upuuzi mtupu! Kama
tusingemtuhumu
Mramba (Waziri wa Fedha wa zamani, Basil Mramba) leo
angekuwa Segerea?
"Kama tusingemtuhumu Yona (Waziri wa Viwanda wa Nishati na
Madini,
Daniel Yona) leo angekuwa Segerea? Ni lazima tuhuma zitolewe
ndipo
serikali iwajibike. Kwa kawaida binadamu lazima kwanza awe
na
'reasonable doubt' sio 'absolute doubt'," alisema
Dk. Slaa. Alinukuu
kifungu kimoja cha Biblia kinachosisitiza kuwa ni makosa na
dhambi
kupotosha watu huku akiitupia lawama Serikali ya CCM kwa
kumlea Lowassa
kwa miaka mingi bila kumshughulikia akisema: "CCM ni waoga
na ndio maana
wamlea mtu huyu na leo wanatuletea matatizo."
Dk. Slaa ambaye alisema hajawahi kutofautiana na Mwenyekiti
wa Chadema,
Mbowe, vikaoni tangu mwaka 2004, aliwashangaa viongozi wa
Chadema kwa
majaribio yao ya kuwapotosha Watanzania kwa kutaka waamini
kuwa kwa
Lowassa na watu wake kuhamia Chadema, wamekuwa watu
wasafi.
"Ni kama vile choo; kwetu Watanzania choo ni sehemu
chafu ingawa kwa
wenzetu ukiingia chooni unakuta kuna glasi ya 'wine'.
Samahani kwa mfano
huo lakini sina mfano mwingine. Sasa leo mtu aende chooni
achote kile
kilichomo ndani ya choo na kukihamishia chumani anakolala,
utasemaje? Ni
kwamba choo kimehamia chumbani. "Na kwa kuwa ili aweze
kuchota kinyesi
kilichomo chooni atalazimika kwanza kukikoroga, basi kile
kilichomo
chumbani kitakuwa kinanuka zaidi ya hata choo chenyewe,"
alisema Dk.
Slaa.
Suala la kashfa ya Richmond
Kuhusu kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond,
kashfa ambayo
aghalabu Lowassa na wapambe wake hawapendi kuisikia hata
kidogo, Mbunge
huyo wa zamani wa Karatu alisema yeye na wabunge wengine wa
Bunge la
Tisa wanalifahamu zaidi kwa kuwa waliiishi kashfa hiyo.
Dk. Slaa aliwatupia lawama wabunge wa CCM kwa kutopenda
kusoma nyaraka
mbalimbali huku pia akiwalaumu waandishi wa habari kwa
kutokufanya
utafiti na kuandika habari za kina.
"Hebu mwambieni Lowassa aache kulalamika. Ajitokeza
hadharani na
kusema Richmond ni ya nani? Amtaje hadharani huyo mkubwa
anayedai kuwa
alimzuia kuvunja mkataba, ni nani. Juu ya Waziri Mkuu kuna
Makamu wa
Rais na Rais, sasa ni nani kati ya hao,
"Juzi juzi hata leo walikuwa wakinitisha eti nisizungumzie
masuala haya
wakidai kuwa nitapotea kisiasa; nini kupotea kisiasa, niko
tayari
kupotea katika siasa za Tanzania hata nipotee kabisa duniani
kuliko
kuikana dhamira yangu.
"Msingi wa Richmond ukitaka kuujua ni ripoti ya Kamati
ya Mwakyembe
(Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Dk. Harrison
Mwakyembe)," alisema
Dk. Slaa Alisema kamati hiyo iliomba ridhaa ya Rais iweze
kupitia
nyaraka za Baraza la Mawaziri na kufahamu kwamba katika
Kikao cha Baraza
la Mawaziri kilichoketi Februari 2, 2006 (takriban mwezi
mmoja na nusu
tangu Lowassa ateuliwe kuwa Waziri Mkuu), kilitoa
mapendekezo ya namna
ya kushughulikia kwa dharuala tatizo la umeme lililokuwa
limeikumba
Tanzania.
Alisema suala hilo lilianzia tangu wakati wa Rais Benjamin
Mkapa ambapo
Baraza la Mawaziri lilielekeza namna ya kulitatua, kisha
suala hilo
likarithishwa kwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.
"Kwa mujibu wa kifungu cha 112 cha Katiba, Waziri Mkuu
ndiye mwenye
nguvu katika utendaji wa serikali na baada ya kikao cha
Februari 2,
2006, saaa 10 jioni ya siku hiyo hiyo, Ibrahim Msabaha
(aliyekuwa Waziri
wa Nishati na Madini wakati huo), akafuta mchakato
ulioanzia kwenye
Serikali ya Mkapa na kubarikiwa na Baraza la Mawaziri.
"Tujiulize Msabaha alipata wapi nguvu ya kufanya hivyo
kama si kwa
bosi wake (Waziri Mkuu)? Mimi mwenyewe, Februari 5 au 6
mwaka 2008
wakati wa kashfa ya Richmond, nililetewa rushwa hotelini
kwangu saa 12
asubuhi. Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu Februari 8,
2008.
"Nililetewa Sh. milioni 500 ili ripoti isipitishwe.
Nikamuuliza
aliyeniletea, kama mimi unanipa Sh. milioni 500, wewe una
shilingi
ngapi?" alisema huku akihoji Dk. Slaa na kumtaka Lowassa
ajitokeze na
kueleza jinsi ripoti ile ilivyoibiwa, ingawa hakufafanua
zaidi akisema
hizo 'ni silaha za akiba'. Alisema amewahi kuwaambia
wote wawili,
Lowassa na Sumaye kwamba rushwa huanzia kichwani, moyoni
kabla ya
kutolewa mikononi na kwamba katika sakata la Richmond,
Lowassa
aliingilia mchakato kwa kumtumia msaidizi wake binafsi
kupeleka
maelekezo kwa Msabaha.
"Leo anasema mwenye ushahidi apeleke mahakamani la sivyo
afunge mdomo
wake; mimi ninasema Lowassa anatafuta urais wa nchi hii
nafasi ambayo
hawezi kupewa mtu mwongo; mwongo hakubaliki kuwa Rais,"
alisema.
Dk. Slaa alikumbushia pia ufisadi wa Kampuni ya Meremeta
iliyodaiwa
kuwa ni mali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kabla
wajanja
'hawajaidaka' na kuitumia kuibia fedha za umma akisema
Lowassa alimuonya
akimwambia nyaraka anazoziandika na kuziwasilisha bungeni
zinaiaibisha
serikali.
"Nikamjibu, nikasema hapana. Tuwatafute kwanza wanaoiba
Meremeta hapo
itatusaidia hata kufahamu nani alisababisha mradi wa magari
wa Nyumbu
ukafilisika. "Baadaye akaniita kule Speaker's Lounge
bungeni, tukawa
wawili, akaja na mtu mwingine ambaye leo sitamtaja, wakaanza
kunitishatisha na nikawaona na wale vijana wao, nikaogopa.
Nikawaambia
nyie ni mafisadi vichwani, moyoni na ndani ya nafsi zenu.
"Baada ya hapo
nikafungua mlango nikakimbia kuokoa maisha yangu. Nani
anaweza
kumwambia Lowassa wewe ni fisadi? Ni watu wachache sana
wenye ujasiri
huo lakini mimi nilimwambia," alisema.
Dk. Slaa aliwashangaa wananchi wanaoshabikia ujio wa
Lowassa kutaka
urais kupitia Chadema akidai kuwa atawasaidia kutatua shida
mbalimbali,
akisema: "Nendeni Monduli (Jimbo la Lowassa), hakuna maji
kule! Sasa
atawaletea vipi maji Watanzania wote? Nendeni Karatu (Jimbo
ambalo Slaa
alikuwa Mbunge kwa miaka 15) mfananishe na Monduli ."Watu
wa Karatu
watakwambia ukweli kuwa akiwa Waziri Mkuu, alibadili hata
mpaka wa
Monduli na Karatu na hadi leo kuna ugomvi. Mtu kama huyo
atawezaji
kutatua matatizo ya wakulima na wafugaji kama yeye mwenyewe
ni chanzo?"
Dk. Slaa pia liponda ujenzi wa shule za kata ambao wapambe
wa Lowassa
huutumia kama kete ya mafanikio yake kiuendaji, akisema
mpango huo
ulibuniwa mwaka 1990 nchini Thailand naye akiwa ni mmoja wa
wajumbe
walioshiriki wakati huo ukiitwa Education For All (EFA).
Urafiki wa
Lowassa na Lawrence Masha Kuhusu uhusiano uliopo kati ya
Lowassa na
aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha,
ambaye naye kwa
sasa yupo Chadema, Dk. Slaa alisema ulianzia wakati wa
mchakato wa
kuhalalisha zabuni ya Richmond.
Alisema Lowassa, Msabaha na Masha walishiriki kikamilifu
kusimamia
mchakato uliorudiwa zaidi ya mara tatu kuiwezesha Richmond
kupata zabuni
ya kufua umeme wa dharura nchini kinyume cha sheria ya
ununuzi. Alisema
kampuni nane zilizoomba zabuni hiyo zote hazikuwa na sifa
lakini
wakubwa hao wakalazimisha Richmond kupewa mkataba ndani ya
siku 10
badala ya siku 45, kwa mujibu wa sheria na kwamba uetetezi
wa Lowassa
kwamba alichukua hatua, si kweli na mtu mwongo hafai kuwa
Rais.
Alisema hata baada ya kashfa ya Richmond kujulikana,
Lowassa na Rostam
Aziz walishinikiza kampuni hiyo irithiwe na Dowans, kampuni
nyingine
feki kutoka Costa Rica. "Kamati ya Mwakyembe ilipotaka
kuifahamu Dowans
ya Costa Rica, iliambiwa kuwa Mkurugenzi wake aitwaye Zamora
aliisajiri
siku moja pamoja na kampuni zake nyingine 99 huku pia akiwa
ni
mwenyekiti wa kampuni nyingine 52 tofauti. "Hadi leo
Dowans wanalipwa
Sh. milioni 153 kila siku. Lowassa aje kutuambia ni nani
anayepokea
fedha hizo. Ninafahamu kuwa hata fedha za kampeni sasa
zinatolewa na
Rostam Azizi, mtu aliyewahi kunipigia simu akiniambia;
'dokta, omba
Mungu ndani ya dakika tano hautakuwapo duniani'.
"Lowassa aje atuambie kwa nini Scotland Yard wanamtafuta
kwa utoroshaji
wa Pauni milioni 400. Mtu huyu leo anataka kuwa Rais!
Haikubaliki na
niseme wazi kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote lakini
ni
Mtanzania na nitapiga kelele watu hawa wajulikane.
"Lowassa aje hadharani aseme ana hisa kiasi gani kwenye
kampuni
mbalimbali nchini ambazo hakuziandikisha kwenye Sekretarieti
ya Maadili
ya Viongozi wa Umma," alisema. Alihoji uadilifu wa Sumaye
aliyepora eneo
la ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Mvomero huko Morogoro
na kuihodhi
ardhi ambayo hadi leo haitumiki na sasa makao hayo makuu
yamejengwa
pembebi ya Barabara ya Dodoma – Morogoro.
Ahitimisha hoja zake
Katika kuhitimisha hotuba yake hiyo ya saa moja na nusu,
Dk. Slaa
aliwasihi vijana aliowaimarisha ndani ya Chadema kutopiga
kura kwa
ushabiki bali watafakari na kufanya uamuzi sahihi huku
akiponda hoja za
kufunguliwa kwa babu Seya na watuhumiwa wa ugaidi Zanzibar,
akisema si
za msingi kwa Watanzania wa sasa.
"Nilisema tangu awali kuwa nimestaafu siasa. Kwa sasa sina
chama, bali
nina nchi. Nimeombwa na vyama vitano tofauti nijiunge
nigombee uraisa,
lakini nikasema hapana, tatizo la Watanzania si urais wa Dk.
Slaa; ni
uadilifu wa viongozi.
"Ndio maana nitaendelea kupiga kelele nje ya vyama vya
siasa kwa kuwa
kuna viongozi ambao si waadilifu wanataka kuchukua taifa
letu. Kwa mfano
mshenda wa Lowassa (Askofu Gwajima) alikuja kwangu,
akaniambia
ninapaswa kumuunga mkono Lowassa kwa sababu anaungwa mkono
na wengi.
"Nikamuuliza akina nani hao? Akanijibu kuwa kuna fedha
kutoka kwa Rostam
Aziz, anaungwa mkono na KKKT na kwamba kati ya maaskofu 34
wa Katoliki,
30 wamehongwa!
"Nikamwambia akili yake imepumbazwa. Nikawasikitikia
maaskofu wangu
kwamba kama ni kweli wamehongwa, basi taifa letu
linaangamia. Mshenga
(Gwajima) akaniambia kuna askofu alitaka gari zuri la
kiaaskofu, ndani
ya dakika 20, akapewa. "Nikajiuliza hawa watu wanatoa wapi
fedha?
Inamaana hata hawaziweke benki kwa sababu huwezi ndani ya
dakika 20
ukanunua gari la Sh. milioni 60," alimaliza Dk. Slaa
hotuba hiyo huku
akisisitiza kuwa zipo silaha nyingine za akiba atazitumia
mara baada ya
Lowassa na Sumaye kujibu hoja hizo.
Dk. Slaa alisema huenda maneno yake yakaonekana kuegemea
upande fulani
kwa sasa, lakini hiyo ni kutokana na ukweli kuwa ukweli
lazima utakuwa
upande tofauti na uongo.
Chanzo Raia Mwema
Toleo la 421, 2 Sep 2015
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments