[Mabadiliko] LIPUMBA AMEHONGWA, SLAA AMENUNULIWA... UKAWA WAMETEKWA!

Wednesday, September 09, 2015
LIPUMBA AMEHONGWA, SLAA AMENUNULIWA... UKAWA WAMETEKWA!

TAFSIRI ya haraka ya neno 'Propaganda' ni taarifa, mawazo au uvumi unaosambazwa kwa makusudi kumsaidia au kumharibia mtu, kundi la watu, harakati, taasisi, taifa na kadhalika.
Propaganda pia inatafsiriwa kama namna ya mawasiliano yanayolenga kuwashawishi baadhi ya watu waunge mkono jambo fulani.
Lakini tafsiri nyingine ya Propaganda ni taarifa ambazo siyo sahihi zinazotumika kwa msingi wa kushawishi hadhira na kuchochea agenda, mara nyingi kwa kuwasilisha taarifa zilizopangwa ama kutengenezwa (pengine kudanganya hapa na pale) ili kuhamasisha kundi linalolengwa liamini kinachoelezwa na liunge mkono.
Neno hili kwa sasa limebebeshwa mtazamo hasi kwa kulihusisha na harakati za kurubuni kwa maslahi ya kundi linaloendesha harakati hizo na kwamba wanaofanya propaganda wanaweza kuwaaminisha watu kwamba ile rangi 'nyeusi' ni 'nyeupe' na kinyume chake.
Hata hivyo, asili yake ilikuwa ni ya usawa na ilikuwa na malengo chanya, kama kuhamasisha masuala ya afya ya jamii, mabango kuhamasisha jamii ishiriki kwenye sensa na uchaguzi, ama ujumbe kuwahamasisha wanajamii kuripoti matukio ya uhalifu.
Pengine hakuna mtu katika historia aliyetumia nguvu ya propaganda kwa mafanikio ya kutisha kama alivyofanya Paul Joseph Goebbels, ambaye alikuwa Waziri wa Propaganda wa chama cha Nazi cha Ujerumani kati ya mwaka 1933 hadi 1945 wakati wa Hitler. Wakati wote wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, yeye ndiye aliyedhibiti mawasiliano yote nchini Ujerumani na kufanikiwa kulibadilisha taifa lote kuwa kakamavu na la kijeshi.
Inaelezwa kwamba, isingekuwa mbinu za Goebbels, chama cha Nazi kisingeweza kutawala Ujerumani kwani licha ya kuhamasisha magwaride ya kijeshi, ndiye aliyewafanya Wajerumani wawe makatili hata wakati wa vita kiasi cha kufanya mauaji ya kutisha, ikiwa ni pamoja na kuwateketeza Wayahudi.
Goebbels ndiye aliyehamasisha hadi kuanzishwa kwa somo la propaganda shuleni, ambapo watoto walianza kuaminishwa mambo mbalimbali tangu wakiwa wadogo, hata kama yalikuwa ya uongo.
Watoto walifundishwa na kulishwa uzalendo kwamba Ujerumani ilikuwa ni ya Wajerumani tu, hivyo Wayahudi na watu wengine hawakutakiwa kuishi humo!

Propaganda za Ukawa
Kiongozi wa chama cha National Socialism (au kwa Kijerumani: Nationalsozialismus), ambacho ni maarufu zaidi kama Nazi, Adolf Hitler, alitenga sura tatu za kitabu chake cha Mein Kampf kilichochapishwa 1925/26, ambacho chenyewe ni silaha ya propaganda, katika somo na mafundisho ya propaganda. Alidai alijifunza faida za propaganda wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kwamba propaganda za Waingereza zilikuwa na nguvu kuliko za Wajerumani. Mjadala kwamba Ujerumani ilipoteza vita hivyo kwa sababu ya nguvu za propaganda za Waingereza umeelezwa kwa kina kwenye kitabu cha Mein Kampf, na ndio ulioakisi harakati za Ujerumani kupigania utaifa wao. Ingawa madai hayo ni ya uongo – propaganda za Wajerumani zilikuwa na nguvu sana kwenye vita hivyo kuliko za Waingereza – mjadala huyo ukawa ndio ukweli wa chama cha Nazi na kupandikiza 'imani' kwa Wajerumani kwa msaada wa Hitler.
Hitler anasema katika kitabu cha Mein Kampf Sura ya VI (nanukuu kwa tafsiri ya Kiswahili): "Daima propaganda lazima ijidhihirishe kwa watu wengi. (...) Propaganda zote lazima ziwasilishwe katika mfumo maalumu na lazima zijikite kwanza kwa wasomi ili zisiwe juu ya vichwa vya watu wenye uelewa mdogo ambao ndio walengwa. (...) Sanaa ya propaganda hasa inahusisha uwezo wa kuamsha matamanio ya watu kwa ushawishi wa kutumia hisia zao, ili kutafuta mfumo mzuri wa kisaikolojia ambao unaweza kuteka umakini na kuchochea msukumo mioyoni mwa wananchi wengi. Makundi makubwa ya wananchi hayaundwi na wanadiplomasia au maprofesa wala hayahusishi watu wenye uwezo wa kufanya maamuzi sahihi baada ya tafakuri katika kadhia husika, bali ni makundi ya vijana ambao wanayumbishwa na wazo moja baada ya jingine. (...) Kundi kubwa la wananchi katika taifa lina tabia za kike na mtazamo ambao mawazo na mwitikio wao unatawaliwa na huruma badala ya tafakuri makini. Halitofautiani sana, lakini lina mtazamo hasi na chanya wa kupenda na kuchukia, sahihi na isiyo sahihi, ukweli na uongo." Mwisho wa kunukuu.
Hapa Tanzania, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) –
...
http://www.brotherdanny.com/2015/09/lipumba-amehongwa-slaa-amenunuliwa.html

--
DANIEL MBEGA
INVESTIGATIVE JOURNALIST, BLOGGER, RESEARCHER & PUBLISHER
CELL: +255 767 939 319/ +255 715 070 109
WHAT'S APP: +255 656 331 974
BLOGS: www.kilimohai.wordpress.com
               www.brotherdanny5.blogspot.com

"Kama hawatuwekei mgombea mzuri, kwanini watutawale?" Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, 1995

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAE93EM_yDa8pUO-HNbNgEGUKPqgVvZf-8bDSfCZyn_W%2BzHWyYw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments