[wanabidii] Mkapa yupo sahihi hakukosea

Monday, August 24, 2015
Watu tunakuwa wasahaulifu sana. Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(SUGU) kwa kumtaja jina, alimuita Waziri Mkuu MPUMBAVU bila ya kuwa na sababu yoyote ya msingi. Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akamtukana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumtaja jina kuwa ni DHAIFU.
Inasikitisha sana kuona kauli ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Willium Mkapa kuwa baadhi ya wapinzni wanaosema wanataka kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa kutafsiriwa kuwa ni matusi kwa Wapinzani. Hivi ni mtanzania gani hajui Tanzania ilishatoka mikononi mwa Wakoloni?(Ilishakombolewa?)

Mzee Mkapa alitumia maneno sahihi kabisa kwa mtu ambaye anajitoa ufahamu wa ukweli wa jambo. Ni sifa gani ambayo inastahili kwa mtu anayetaka kulikomboa Taifa ambalo tayari lilishakombolewa? Anashindwa kweli kutumia hata maneno kama MABADILIKO na siyo UKOMBOZI?

wapinzani nawaonya msije mkakomalia kauli ya MKAPA na mkaacha kujikita kwenye agenda za msingi. Alichokisema Mkapa ni sahihi kabisa, Tanzania ilishakombolewa na kinachotakiwa ni MABADILIKO ambayo siyo lazima yaletwe na Wapinzani bali chamamchochote chenye MGOMBEA MWADILIFU na anayetokana chama chenye Sera safi na siyo UKOMBOZI.

wote tunaoamini Tanzania ni Taifa huru lazima tuungane na kauli ya MKAPA na pengine kauli hii iwe fundisho kwa wanasiasa wanaotumia maneno yanayowapotosha watanzania.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments