[wanabidii] Mkuu Chuo cha GTI, Bi. Zuki Mihyo Afungua Mafunzo ya Jinsia, Demokrasia na Katiba

Wednesday, March 26, 2014

[caption id="attachment_44352" align="aligncenter" width="640"] Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (kulia, aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI.[/caption][caption id="attachment_44348" align="aligncenter" width="640"] Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI.[/caption][caption id="attachment_44350" align="aligncenter" width="640"] Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya. [/caption][caption id="attachment_44351" align="aligncenter" width="640"] Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI.[/caption][caption id="attachment_44349" align="aligncenter" width="640"] Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya. [/caption]
MKUU wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo leo jijini Dar es Salaam amefungua mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yaliyowashirikishwa washiriki kutoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Pwani na Morogoro.

Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Jinsia kilichopo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, Bi. Zuki Mihyo alisema kutokuwepo na misingi imara ya kutetea, kulinda na kudumisha demokrasia iliyojengwa kwenye misingi ya usawa wa kijinsia inayo tambulika Kikatiba kumechangia uwepo wa tatizo la unyanyasaji wa kijinsia nchini.

Alisema tatizo la unyanyasaji wa kijinsia licha ya kuwapata watu wa jinsia zote, limekuwa likiwaathiri zaidi wanawake na watoto wa kike tofauti na ilivyo kwa wanaume na watoto wa kiume katika jamii, hivyo kushauri kuna kila sababu ya kupambana na mifumo kandamizi inayochangia hali hiyo.

"...Wanawake na watoto wa kike mara nyingi wamekuwa wakifanyiwa ukatili huu na wanaume au wavulana ambao wanaweza kuwa ndugu zao wa karibu, marafiki na hata wenzi wao," alisema Mkuu huyo wa chuo cha GTI kilichopo chini ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)
[caption id="attachment_44347" align="aligncenter" width="640"] Mmoja wa watoa mada wa mafunzo hayo, Geoffrey Chambua (aliyesimama katikati) akizungumza na washiriki wa mafunzo.
[/caption]
Alisema suala la ukekelezaji wa mila na desturi kama vile ukeketaji, kurithi wajane na mila nyingine nyingi zinazowagandamiza  wanawake na makundi ya pembezoni na kuwafanya kutokuwa na sauti wala kushiriki katika kutoa uamuzi kuanzia ngazi ya familia hadi taifa vimekuwa vikichangia ukatili wa jinsia kwa wasichana, wanawake na makundi mengine ya pembezoni.

"...Tunaelewa kuwa wakati wa zamani mila nyingi zilikuwa na maana lakini kwa wakati huu mila hizo zimepitwa na wakati hivyo ziachwe ili kukomesha dhuluma, manyanyaso, ukandamizaji n.k, ili kuwa na usawa kwa watu wote," alisema.

Aidha alifafanua kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa washiriki kuweza kushiriki katika kuchambua masuala ya jinsia, demokrasia na katiba mpya ili waweze kuyasimamia na kuyatetea katika mikakati mbalimbali ya maendeleo. Aliongeza kuwa malengo mahususi ni pamoja na kukuza uelewa na utambuzi wa uhusiano baina ya dhana za jinsia, demokrasia na katiba, kuchochea ushiriki na uwajibikaji wa asasi za kiraia na makundi maalumu yaliopo pembezoni na mchakato wa kidemokrasia na kutambua changamoto na fursa zilozopo katika kuingiza masuala ya jinsia na demekrasia kwenye katiba mpya.

Akifafanua zaidi juu ya mafunzo hayo, mmoja wa watoa mada, Geoffrey Chambua alisema washiriki wanatoka katika ngazi ya jamii; yaani katika asasi za kiraia, vikundi vya kijamii, asasi za kidini, wajasiliamali na makundi maalumu wote kutoka katika  mikoa ya Morogoro, Lindi, Pwani pamoja na Dar es Salaam yenyewe. Chambua alisema mafunzo kama hayo pia yanaendelea katika kanda anuai.

Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments