FAIDA NA HASARA ZA LOWASA KUHAMA CCM NA KUHAMIA CHADEMA
Katika sakata hili la Lowassa kuhamia Chadema kuna vitu vya kuzingatia;
1. Mpaka sasa hakuna yeyote anayejadili sera ya kilimo, elimu , afya , miundombinu, uwekezaji , mambo ya nje, ulizi na usalama, michezo na utamaduni, hali ya hewa, nishati na madini, muungano na mambo mengine muhimu kwa taifa.
Hili ni kosa, lakini si kubwa sana kwa vile ilani za uchaguzi hazijaanza kutangazwa.
Hata hivyo, hapa tunajifunza kuwa ratiba ya kuchagua mgombea kabla ya kuwa na ilani sio sahihi. Inafanya mijadala ijikite kwenye personalities rather than real issues.
2. Kila upande unaweza kuathirika au kunufaika na maamuzi ya Lowassa kwenda Chadema kama ifuatavyo;
1. Mpaka sasa hakuna yeyote anayejadili sera ya kilimo, elimu , afya , miundombinu, uwekezaji , mambo ya nje, ulizi na usalama, michezo na utamaduni, hali ya hewa, nishati na madini, muungano na mambo mengine muhimu kwa taifa.
Hili ni kosa, lakini si kubwa sana kwa vile ilani za uchaguzi hazijaanza kutangazwa.
Hata hivyo, hapa tunajifunza kuwa ratiba ya kuchagua mgombea kabla ya kuwa na ilani sio sahihi. Inafanya mijadala ijikite kwenye personalities rather than real issues.
2. Kila upande unaweza kuathirika au kunufaika na maamuzi ya Lowassa kwenda Chadema kama ifuatavyo;
i) CCM
Faida
a) Kupunguza lawama za kuitwa chama cha mafisadi. Chadema na Ukawa wameshaanza kuondoa neno ufisadi na mafisadi kwenye kauli zao. Kauli yao mpya ni kubadili mfumo. Hata hivyo bado Chadema wana kibarua cha kuelezea wataubadili vipi mfumo kwa sababu mfumo sio chama cha siasa.
b) Kutoa fursa kwa wanasiasa wasio waaminifu kwa chama kukikimbia na kuacha wale walio tayari kukipigania chama. Rafiki wa kweli hujulikana kipindi cha changamoto.
c) Kupata fursa ya kuingiza wimbi kubwa la mamluki ndani ya upinzani kwa kisingizio cha kumfuata Lowassa. Hawa watapewa hero's welcome na kuaminiwa kirahisi.
Hasara
a) Siri zake za maandilizi ya uchaguzi zitafahamika kwa upinzani. CCM italazimika kufanya mabadiliko makubwa kwenye mikakati jambo ambalo litakigharimu chama.
b) Kupoteza baadhi ya watu ambao fundamentally wanaamini Lowassa ndio mtu pekee nchini mwenye uwezo na haki wa kuongoza. Ingawa kundi hili ni la watu wasioelewa maana ya chama lakini lipo. Hawa watamfuata Lowassa kokote anakoenda, wanasema "ulipo, tupo".
i) Chadema
Faida
a) Kupata mgombea tajiri ambaye ni high profile politician.
b) Kupewa siri za CCM.
c) Kupokea wafuasi wa Lowassa.
Hasara
a) Kujenga sura ya kuthamini umaarufu na pesa kuliko misingi ya Chama.
b) Kukiri de facto kuwa hawakuwa na uwezo wa kuishinda CCM. Hapa watahojiwa je mtu mmoja ndio amewaletea uwezo? Je , kama mtu huyo ana nguvu kubwa kuliko Chama, mtamdhibiti vipi akiwageuka huko mbeleni?
c) Kuwakatisha tamaa wanaojitolea kwa ajili ya Chama. Kitendo cha Slaa kukatwa na kutokusikilizwa kitawafanya watu kama kamanda Mawazo wakae chini na kutafakari kazi wanayojitolea inalenga kubadili nini? Wengi wa wanaojitolea kwa nia njema huongozwa na misingi na itikadi ya Chama. Chama kinapotoka nje ya misingi , kinahatarisha kupoteza au kuwavunja nguvu watu hawa.
d) Kupunguza kuaminiwa na wananchi. Sura iliyojengeka ni kuwa Chadema inacheza tu mchezo wa siasa na hailengi hasa kuboresha maisha ya mtanzania. Mtu yeyote anayewapa pesa za uchaguzi watamtukuza ilimradi tu washinde. Kauli hizi za Mbowe hazijapokelewa vizuri na watanzania.
e) Kutumia nguvu kubwa kusambaza ujumbe mpya. Siku zote inafahamika ujumbe wa chadema ni kupinga mafisadi. Sasa kuna mabadiliko, tatizo sio mafisadi ila mfumo. Hii itahitaji resources nyingi kuwaeleza watu mpaka waikubali. Kwahiyo muda wa kuzungumzia masuala mengine ya maisha ya kila siku utakuwa mdogo kuliko wa kufafanua mabadiliko haya ya msimamo. Hii inaatarisha Chadema kuonekana Chama kinachotafuta madaraka bila kuwa na mkakati wa kuongoza nchi na kuboresha maisha.
f) Iwapo Chama hakitashinda uchaguzi kitakosa misingi ya kukiendeleza. Kitabaki kuonekana chama cha wajanjawajanja. Watu wa Lowassa ambao wameahidiwa vyeo serikalini itabidi watake vyeo kwenye Chama. Chama kitachukuliwa na watu wasiokijua wala kukijali kwa dhati.
3. Pamoja na kwamba watu hudhani siasa ni mchezo, lakini siasa ni taaluma. Katika haya yanayoendelea, mwenye taaluma zaidi ndiye atayejipatia faida zaidi kuliko hasara.
4. Sisi kama watanzania tunachotakiwa kuomba ni Mungu aendelee kuilinda nchi yetu iwe na amani na umoja kama taifa
0 Comments