[wanabidii] Alichofanyiwa Slaa kimewaumiza wengi sana katika mitndao ya kijamii

Tuesday, August 04, 2015
(Hiki ndicho alichoandika mdau mwenzetu wa mitandao ya kijamii mara baada ya kusikia kuwa Dr Slaa kajiuzulu na kujivua uanachama wa CHADEMA)

Kiukweli itanichukua muda mrefu hadi kurudi katika hali yangu ya kawaida ili niweze kuamnini kinachotokea nyakati hizi ndani ya chama langu CHADEMA/UKAWA...Labda tu niwe muwazi kuwa bado sijaelewa mantiki hasa ya mwenyekiti wangu MBOWE kuchukua uamuzi huu....Bado najiona mwenye hatia ndani yangu maana niliamni kuwa LOWASA ndiye adui namba moja wa uchumi wa TANZANIA kwa ufisadi wake....niliyaamini haya kupitia kwa viongozi wangu wa CHADEMA katika kufichua maovu ndani ya chama tawala bila woga na ujasiri wa hali ya juu.....

Tena tukaambiwa kuwa huyo mtu anapaswa afungwe jiwe kubwa na atupwe baharini au kama vipi achomwe moto...maana kumweka jela pekee yake haingetosha kutibu madhira aliyowasababishia wananchi kwa ufisadi wake....ujumbe huu ulipelekea chama tawala kutikisika na hatimaye kuamua kujivua magamba kwa madhumuni ya wale waliokuwa na tuhuma za ufisadi wajiondoe wenyewe au waondolewe,....sote kwa pamoja tukapongeza juhudi za Dk Slaa na CHADEMA kwa ujumla kwa ujasiri wao......

Na naweza kusema hata maamuzi ya kulikata jina la LOWASA yaliyofanywa na kamati kuu ya CCM yalipata msukumo kwa kiasi kikubwa na kelele za upinzani kuhusiana na kashfa za ufisadi za LOWASA.......Huku tukimshudia Mbowe akisema kuwa endapo CCM itampitisha LOWASA kuwa mgombea wao basi itakuwa imeipunguzia kazi ya kufanya UKAWA kwani mgombea huyo ni mchafu na hasafishiki hata kwa jiki.......Huku Dk SLAA akiiponda safari ya matumaini ya LOWASA kwamba WATANZANIA wamechoka kuishi kwa matumaini katika nchi yenye utajiri wa kutosha wa rasilimali badala yake wanataka safari ya uhakika.....ambayo yeye ataianzisha..........

Sasa iweje leo wana CHADEMA TUAMBIWE KUWA MTU HUYO NI MSAFI isipokuwa tu mfumo ndio mchafu...na sisi tushangilie tu....tunatakiwa kujiuliza kuwa huo mfumo unaundwa na nani kama sio watu....huo mfumo unaendeshwa na wakina nani kama sio watu....sasa hao watu ni wakina nani??? kama sio hao hao mliotuaminisha kuwa ni mafisadi na wanapaswa kuwa magerezani na sio uraiani.....Nitakuwa nimekosea kwa kuwaita viongozi wa CHADEMA walioshiriki kumkaribisha LOWASA kuwa ni MANDUMILAKUWIRI...???......... ...WATANZANIA WENGI WAPENDA MABADILIKO TUNA IMANI NA SLAA NA SIO HUYO LOWASA..........
 

Share this :

Related Posts

0 Comments