[wanabidii] ANTHONY KOMU AMTISHIA SIRAHA LEMA, AMABAYE NI KATIBU WA MKOA KILIMANJARO CHADEMA KISA KUSHINDWA KATIKAKURA ZA MAONI CHADEMA

Thursday, August 20, 2015
ANTHONY KOMU AMTISHIA SIRAHA LEMA, AMABAYE NI KATIBU WA MKOA KILIMANJARO CHADEMA KISA KUSHINDWA  KATIKAKURA ZA MAONI CHADEMA

Mkurugenzi wa  Fedha na Utawala wa, Anthony Komu, amedaiwa kumtisha kwa silaha katibu mkuu wa chama hicho mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema.

Tukio hilo lilidaiwa kutokea jana baada ya  Chadema makao makuu, kudaiwa kuamuru kurudiwa kwa uchaguzi wa kura ya maoni, ambao awali ulimpa ushindi Mbunge wa Viti maalum, Lucy Owenya, baada ya kuwashinda wagombea wengine tisa kwa kura 266, akiwemo Komu aliyepata kura 25.

Akizungumza na Nipashe, Lema alidaiwa kutishwa kwa bastola na Mkurugenzi huyu saa 6:00 mchana eneo la Kibosho baada ya kutaka kujua taratibu zilizotumika kuhamisha mkutano halali wa uchaguzi uliofanyika eneo la Garden kata Kiboroloni manispaa ya Moshi.
"Ni kweli amenitisha kwa silaha na sasa hivi nimetoka kituo cha polisi Moshi mjini kumshitaki. Wamenipa hati yenye namba MOS/RB/829/2015".

"Kimsingi mimi nilikwenda kujua wajumbe waliopelekwa pale ni halali, kama amabavyo niliagizwa na kaimu na kaimu katibu mkuu (Salum…. Mwalimu) hata hivyo, huo mkutano haukufanyika, lakini mkutano halali Garden umempitisha Lucy kuwa mgombea" .

Hata hivyo, Komu alisema: "Sijawahi kushika silaha wala similiki silaha. Nilishika mara ya mwisho nikiwa JKT (Jeshi la Kujenga Taifa).Iweje  nimtishe Lema kwa wakati Sina ugomvi nae?... yeye kaja kasema amekuja kuvunja mkutano, tukamwambia hapana ni Moshi vijijini, tulifanya uchaguzi wetu hata hivyo kulitokea rabsha na vijana wake aliokuja nao wa ulinzi wakatofautiana na kupigana".

CHANZO NIPASHE, 19/08/2015, UKURASA 3

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments