Hofu yatanda kambi ya Halima Mdee Ndani ya Jimbo la Kawe.
Baada ya Janeth Rite kutangaza kutaka kugombea Ubunge
Halima na kambi Yake wanajua atawashinda kwenye kura za maoni za CDM sasa waanza kuandaa zengwe.
Wenyewe wanazani wanamchafua kumbe wanamng'arisha.
Hii ndiyo meseji ambayo timu ya Halima inasambaza ikiongozwa na mtu ambaye ameandaliwa kugombea udiwani Kata ya Kunduchi
"UBUNGE WAIVURUGA CHADEMA KAWE.
Diwani wa Kunduchi jimbo la Kawe na mtamani ubunge wa jimbo hilo kupitia Chadema bi Janeth Rithe kuingia katika mgogoro mkubwa na mbunge wa jimbo hilo kupitia Chadema Halima mdee.
Kwa mujibu wa Janeth, kabla ya nia hiyo ya ubunge aliwahi kugombea uenyekiti Bawicha lakini jambo la kushangaza Mbowe alimtumia walinzi ili wamfungie ndani asishiriki uchaguzi ule uliyempa ushindi Halima.
Camera zetu zilimfuatilia Janeth kwa umakini tangu tupate habari hizi, siku ya jana camera zilimnasa akiingia ofisi za chama cha ACT na kukaa kwa muda kidogo.
Moja kati ya watu wa ACT makao makuu walituelezea lililompeleka Janeth pale ni kuomba uanachama na ikiwezekana apewe ridhaa ya kugombea Kawe.
Mwandishi wetu alipotaka kuyajua hayo toka kwa Bi Janeth, mwenyewe alikiri kutaka kuhamia ACT na sio yeye pekee bali nusu ya madiwani wa jimbo la Kawe.
Halima alipoulizwa alidai Janeth ni muoga wa demokrasia na anategemea ushindi wa kupewa kitu ambacho hakiwezekani.
Joyce Mbikirwa ni moja kati ya viongozi wa Chadema jimbo la Kawe wanaoaminika kuwa tayari kuambatana na Janeth kujiunga ACT kwa sababu ya uongozi mbovu wa Chadema jimboni hadi makao makuu.
Mwandishi Huru
Kawe.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments