Ndugu zangu,
Tangu nikiwa kijana mdogo wa Sekondari nimekuwa na ndoto ya siku moja kukutana na Dr Salim na kufanya nae mazungumzo ya kina na ya ana kwa ana. Fursa hiyo niliipata majuzi hapa.
Hakika, Dr Salim ni mmoja wa Watanzania waliotufanya, enzi hizo tukiwa shuleni, tutembee tukijivunia kuwa Nchi Yetu ni moja ya ' Mataifa Makubwa' kwenye siasa za dunia. Ni kupitia watu wa aina ya Dr Salim, Tanzania ilikuwa na sauti ya kusikilizwa duniani.
Na hakika, mazunguzo niliyoyafanya na Dr Salim hivi karibuni ni moja ya mazungumzo muhimu niliyopata kuyafanya ya kuweka kwenye kumbukumbu. Ilikuwa ni kama mwanafunzi aliyekutana na mwalimu aliyekuwa akimtungia maswali, na sasa mwalimu na mwanafunzi wanatafsiri kwa pamoja maana ya majibu ya maswali yale.
Ndugu zangu,
Naweza kabisa kumwelezea Dr Salim kwa maneno manne; Kiongozi, Mzalendo, Mwanamapinduzi na Shujaa.
Ndio, ni Kiongozi mzalendo, mwanamapinduzi na shujaa wa Afrika. Nyongeza muhimu; ni mtetezi wa haki za wanyonge wa dunia. Aliyaanza mapambano ya kuipigania Afrika na wanyonge wa duniani akiwa na miaka 22 tu.
Am hakika amestahili kuwa na nishani ya utumishi uliotukuka si kwa Tanzania tu, bali kwa bara zima la Afrika.
Dr Salim alinisimulia mengi; sikiliza kidogo hapa kwenye kipindi cha ' Nyumbani Na Diaspora'
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments