Mwandosya yeye alitangaza nia mkoani Mbeya amekuja na vipaumbele vyake kumi ambavyo wengi wamevikubali hususani kuendelea kilimo pale anapoishia rais Kikwete.Mwandosya hakuwa na msisimko mkubwa sana jukwaani wa kumpinga kama ilivyokuwa kwa Lowasa kwa mijadala mingi ya Mwandosya ilikuwa kimya isipokuwa kambi ya Lowasa wao walikuwa wanambeza kwa kumuhofia kuwa atakuja kuwa kikwazo kwao. Sababu kubwa ya mijadala ya Mwandosya kuwa kimya na kukosa upinzani kwawapinzani wake hawana cha kumsema juu ya ufisadi wala rushwa kashfa na tuhuma yeyote ile kama wagombea wengine badala yake wanasemea tumboni.
Mwandosya anazungumzia Uchumi imara unajengwa hasa pale panapokuwa na lengo la kitaifa.Lengo katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ni Tanzania kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Lengo hilo liliwekwa mwaka 2000 kwamba ifikapo mwaka 2030 Tanzania iwe nchi za juu zenye kipato cha kati(High Middle Income),na kwamba ifikapo 2050 Tanzania iwe nchi iliyoendelea.
Tunawezaje kuyafikia malengo hayo? Tunawezaje kukuza uchumi na ukuaji huo uwe endelevu?Hili ndilo swali. Na haya ndio majibu ya Mwandosya na vipaumbele vyake
1.Kilimo cha kisasa na cha kisayansi kupitia matumizi zaidi na bora ya mbolea; kuendeleza utafiti kwa kuboresha miundombinu,vifaa,na kuendekeza rasilimali watu;kuboresha mifumo na aina ya mikopo kwa wakulima wadogo;kuboresha barabara za vijijini; kuendeleza ujenzi wa maghala kwa ajili ya kutunza nafaka;kuwa na migumo ya uhakika ya masoko ya mazao;na kuhakikisha kiwanda cha kimkakati cha mbolea itokanayo na gesi asilia kinajengwa haraka iwezekanavyo.
2.Kuanzisha na kuendeleza viwanda,kwa kuanzia viwanda vinavyoongeza thamani ya mazao na rasilimali asili
3.Kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa chakula.
4.Kuendelea kusimamia kutengemaa kwa uchumi mpana
5.Kuondoa vikwazo vinavyozuia uwekezaji wa ndani na kutoka nje
6.Kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa ipasavyo kwa kufungua fursa nyingi za utalii wa ndani na utalii katika sekta ya kusini.
7.Kuongeza tija katika utendaji wa kazi kwa kuthamini kazi(kufanya kazi kwa bidii,kwa uadilifu,na kwa kujituma), kusimamia kanuni,maadili na miiko ya utumishi wa umma na kuufanya utumishi wa umma usiwe wa mazoea tu bali wa ushindani unaopimika katika kutoa huduma kwa wananchi.Hii itakwenda sambamba na kulinda haki na kuboresha msilahi ya wafanyakazi.
8.Kuchukia,kuzuia na kupambana na ufisadi na rushwa. Kuondoa vikwazo vinavyoonekana kuwepo kwa matabaka mawili ya wananchi; wale wanaoshughulikiwa na takukuru moja kwa moja,na wale ambao kibali kinahitajika kuwashtaki,kwa kuipa Takukuru uwezo wa kisheria kufanya kazi bila kuingiliwa na chombo chochote,wakati huohuo kuhakikisha haki za wananchi wema zinalindwa kupitia chombo cha kusimamia malalamiko (ombudsman).
9.Kuendeleza na ikibidi kuimarisha uhuru wa Benki Kuu na uhuru wa vyombo vya udhibiti wa huduma za kiuchumi,mifuko ya jamii,bima.
10.Serikali kuwa injini ya ukuaji wa uchumi lakini kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi,mtu mmoja,vikundi vya wajasiriamali,saccos,na kampuni binafsi kuchochea ukuaji wa uchumi.
Uchumi unapokua,basi serikali itakuwa katika nafasi nzuri ya kutekeleza vipaumbele katika maendeleo ya jamii: Elimu,maji safi na salama,afya, na miundombinu. Kuhusu elimu,anasema ataboresha mitaala ili iendane na matumizi ya sayansi na teknolojia katika ngazi zote;kuhakikisha kila mtanzania ana nafasi sawa ya kujiendeleza kielimu kuanzia ngazi ya awali mpaka elimu ya juu; kuendeleza elimu ya ufundi na kilimo; kuandaa na kutekeleza mipango kwa hatua kuifanya elimu ya msingi ifikie kidato cha pili, cha nne na hatimaye kidato cha sita;kuongeza wingi wa udahili wa wasichana katika katika ngazi ya elimu ya juu;kuboresha hali na ari ya utendaji wa kazi kwa walimu,ikiwa ni pamoja na ujenzi nyumba za kuishi na kuongeza ujira.
Katika maeneo mengine ya huduma za kijamii, Prof: Mwandosya anasema lengo la serikali litakuwa ni kutekeleza sera zilizopo na kuhakikisha malengo yanatekelezwa na yanapimika.Katika kuleta afya bora kwa wananchi lengo litakuwa ni kuweka mizania katika kuzuia na kupambana na magonjwa.
Uchumi hauwezi kukua pasipokuwa na amani na utulivu. Amani usalama na utulivu ni tunu.Waasisi wetu wametujengea msingi wa tunu hii. Viashiria vya kupotea kwa amani vinaanza kuonekana kutoka ndani na nje.Hali inahitaji kuimarisha vyombo vyetu vya usalama katika maeneo yote hususan mafunzo,vitendea kazi,vifaa, miundombinu na silaha za kisasa.Hatimaye ulinzi wa nchi unaanzia mwananchi mwenyewe.
Mwandosya amwataka watanzania kuwa uzalendo na upendo kwa nchi. Ansema kumekuwa upungufu wa uzalendo na unajionesha katika kuenzi tamaduni za nje, kubeza juhudi za maendeleo yaliyopatikana, viongozi kutoa matamshi yanayo kebehi nchi wakiwa nje ya nchi,kutojivunia historia yetu iliyojikita katika michango ya mashujaa wetu.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments