[wanabidii] Kauli mbiu yake ya "Tanzania ni yetu, Tusimame"

Sunday, June 07, 2015

Nami leo nakwea katika eneo hili hapa Namfua, ili kupitia Singida niongee na watanzania wenzangu nchi nzima, sababu saa ya uhuwisho wa Tanzania, Saa ya Tanzania kupiga hatua kubwa zaidi, saa ya watanzania viongozi wa kizaizi kipya kukimbia kwa mbio zaidi imewasili.

Watanzania wenzangu, Mungu ameniruhusu kusimama mbele yenu leo, lakini ameniruhusu kwa saa na wakati kama huu, wakati wa kihistoria mabayo naiona imewadia, na sisi sote leo tumejaliwa kuwa katika sehemu ya historia hii ambayo inaanza katika Namfua hapa Singida.

Aidha nirudie kuwashukuru tena wana Singida kaskazini, Kwa kunipa imani na kunipa fursa ya kuweza kuliongoza jimbo la Singida kaskazini kwa miaka 15 nikiwa kama Mbunge wao. Nakumbuka tuliimba Mapinduzi ungali bado kijana mdogo, nimepewa nikulee upate makamo, uweze kukua, uweze kufundishwa ukafundishika.

Saa imefika baada ya miaka 15 ya kuwa mbunge wa wana Singida kasikazini, ni heshima iliyoje, Nimesimama mbele ya taifa niweze kuomba ridhaa katika mioyo ya watanzania na mioyo ya wanachama wa chama cha CCM, kama mkiona vyema, mniruhusu niingie malangoni mwenu.

Waliandika katika vitabu zamani, wengine watataja farasi, na wengine watataja magari, lakini sisi tutalitaja lile jina ambalo linatuunganisha sisi watanzania wote. Tutalitaja mapenzi yatokanayo kwa Mungu, tutataja imani ya watanzania, kwakuwa mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema chama ni imani, imani ambayo inatuunganisha watanzania ndani ya CCM kikaendelea kubaki kuwa chama kikubwa katika Afrika chama kilichowaunganisha wazanzibar na Wabara, chama kilichouwenzi Muungano wetu lakini chama ambacho ndo kinaiongoza Afrika kuelekea umoja unaotarajiwa wa mataifa ya Afrika

Naomba nichukue fursa hii kwa mara nyingien tena, Nimshukuru kwa kipekee, Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wa kitaifa, na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, DK. Jakaya Mrisho Kikwete, kwanza kwa kuniruhusu na mimi niingie katika malangoni pake , akaniteuwa kua msaidizi wake mkuu kwenye dhamana ya kusimamia rasilimali zinazoongozwa na Wizara ya maliasili na utalii. Katika kuifanya hii, moja nimeona moyo wa rais wetu, nmeyaona mapenzi yake ya dhati kwa watanzania, nmeona imani yake, nmeona akisimama wakati uliomfaa na usiomfaa, akilitetea akifanya kazi kuisimamia tanzania, sijaona katika maisha yangu, mzee mwenye stamina anayaweza akafanya kazi asilale zaidi Mh Rais Jakaya Kikwete.

Chini ya Uongozi wa Jakaya, nikiwa msaidizi wake katika wizara ya maliasili na utalii, Utalii sasa unaliingizia pato taifa letu kama ni pato linaloongoza kuingizia taifa letu pesa za kigeni, utalii sasa mchango wake Unazidi robo ya jumla ya pato kuu la Taifa, utalia unatoa ajira za moja kwa moja zaidi ya laki tano, lakini watanzania zaidi ya mil mbili wanaendelea kunufaika na biashara hii ya utalii.

Hivi karibuni nalitangaza katika bunge la Tanzania kwamba Tanzania sasa imetajwa kwa mara ya kwanza ndo nchi ya kwanza barania Afrika ambayo ina mvuto, haiba, utashi ya kwanza ikifuatiwa na Taifa la Botswana kwa mataifa na wanadamu kukimbia kuja kutembea katika nchini mwetu.

Kama Waziri mwenye dhamana ya maliasili na utalii, na kwa kuzingatia matakwa ya ilani ya uchaguzi yACCM ya mwaka 2010 hadi 2015, fursa hii imenipa kushiriki moja kwa moja katika katika kutatua changamoto za ulinzi wa lasilimali za taifa letu. Hususani kuepo na kuendelea kuwepo kwa lasilimali ya wanyamapoli katika nchi yetu. Na vilevile nimepata fursa ya kushiriki moja kwa moja katika kutatua migogoro inayo wakatibir wakulima na wafugaji, sabau naamini, Tanzania bila migogoro inawezekena. Na namshukuru sana rais Kikwete, kunipa fursa kuwa mmoja wa askari wake wa mwamvuli.

Chini ya uongozi wa urais wa Kikwete nikiwa msaidizi wake, Kwa mara ya kwanza Tanzania imefanikiwa katika vita dhidi ya ujangili, hawa ni wezi, hawa ni watu ambao wanaionea husda nchi yetu, hawa ni watu ambao wanapaswa kushindwa na kulegea hawa ni watu ambao hawana fursa hapa Singida, Songea, Mbeya Zanzibar au popote Tanzania. Ni watu wabaya.

Kwa mala nyingine tena Tanzania kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa za Tembo za mwaka 2014 nilizozitua pia Arusha wiki iliyopita, kwa mara ya kwanza Tanzania kupambana na tatizo kubwa la Ujangili chini ya Uongozi wa Kikwete nikiwa Msaidizi wake, Mfumo wa Mbuga ya Serengeti, wameongezeka Tembo kwa asilimia 98.

Kazi kubwa nliyo nayo sasa ni kuhakikisha Tembo wapo salama na wananchi wanozunguka mbuga wapo salama. Mfumo wa Tarangile na Manyara, Tembo wameongezeka kwa asilimia 66. Mwaka 2013 tembo walitingisha dunia kutoka elfu50 hadi elfu 13. Sasa hivi wameongezeka ndani ya mwaka mmoja kutoka tembo elfu 13 hadi elfu 15.

Mwaka 1958 Mwalimu Nyerere, Alisema Tanzania itapandisha mshumaa katika mlima Kilimanjaro, na mshumaa huo utatoa na kusambaza mianga ya upendo, matumaini na amani na kwamba itaisambaza nchi nzima pande nne za Tanzania na nje ya mipaka yetu. Wakati tunapata uhuru watoto waliimba wakisema Tanzania nakupenda kwa moyo wote. Taifa la Tanzania lilisimama katika misingi ya Udugu, umoja, imani matumaini kwa wananchi. Hatua za miguu yake ya alizokua anazipiga, akasema kuwepo muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, akasema kuwepo Upendo mahali palipo na chuki, Nuru palipo na giza amani palipo vita ama mashaka, kuwepo haki palipo dhuluma. Mimi hatua hizo kama walivo zikanyaga marais walionitangulia, nazitazama hizi hatu wazi, Mungu anisaidie/atusaidie watanzania tuzipige hatua hizi alikuipeleka nchi yetu hatua inayo fuata.

Naamini sisi kama taifa kwa umoja wtu wa kusimama kama taifa umefika. Na mimi naomba kusema tena, Tanzania ni yetu na sisi sote tusimame kwa kuwa saa ya kuhuishwa upya taifa la Tanzaia imefika. Kazi na upokeo wa uongozi tunaoupokea tunaupokea kwa heshima kubwa lakini hatua ya pili ya Tanzania ni kuihuisha nchi hii itoke hapa ilipo iende hatua moja kubwa zaidi.

Anasema katika Uwaziri wake ameweza kudhibiti Ujangili wa tembo ambapo hivi sasa tembo wanaongezeka baadala ya kupungua.

Anasema tusimame pamoja kama taifa tuwashangaze majirani.

Anasema kubwa kuliko yote ni upendo

Anasema yeye atawekeza katika rasilimali watu

Anataka jamii yenye maono na ujasili na njia pekee ni kuwashirikisha wananchi uwezo

Atapiga ubaguzi na chuki baina ya vyama vya siasa. kwani chuki ya kwenye siasa huhamia kwenye jamii

Taifa letu linahitaji sera ya kuendeleza mema yote aliyo yaanzisha Kikwete

Tutlitazama swala la ardhi, usalama na kuhakikisha umoja na Mshikamano unadumu.

Ndimi zetu sisi tunaochukua fomu zijaliwe kusema vizuri, kuongeza umoja na mshikamano kwani siku ya mwisho atachaguliwa mmoja tu.

Nawashukuru wasisi wetu kuanzia TANU Kwa kazi nzuri kutoka bara hadi visiwani.

Tusimame kwa dakika moja kuwakumbuka waasisi wetu waliotuunganisha

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments