9 MACHI 2015 SIKU YA MWISHO YA NOTISI KANISA KANISA LISILO RASMI KUHAMA KAWE
Siku 30 za notisi zimetimia Mchungaji Josephat Gwajima Kufunga virago Kawe!
Kanisa la lisilo rasmi la mchungaji Mchungaji Josephat Gwajima lililokuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe,wilaya ya Kinondoni,jiji Dar limeamuriwa kuondoka mara moja na kuwacha eneo hilo wazi kwa ajili ya maendeleo ya watu wa kawe. Kanisa hilo ambalo kwa muda mrefu lemekuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu na kusababisha usumbufu na kero kubwa za makelele kwa wakazi wa maeneo hayo. Katika Barua iliosainiwa na Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa shirika la nyumba la Taifa imesisitiza kwamba pamoja na kutambuliwa umuhimu wa kanisa hilo kuendesha shughuli zake lakini shirika hilo halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo kuendelea kufanya mahubiri katika viwanja hivyo,kwani shirika hilo limeshaanza kutumia Viwanja hivyo kwa maendeleo ya wananchi wa KAWE ikiwa ni ujenzi wa makazi n.k Bw Masika ametoa siku 30 tu ambazo leo 9 Machi 2015 Mchungaji Gwajima anatakiwa kufunga virago na kuwacha viwanja hivyo wazi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Mchungaji Josephat Gwajima afunge virago
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments