[wanabidii] PRESS RELEASE: KINONDONI TALENT SEARCH. KIPAJI CHAKO. AJIRA YAKO

Tuesday, March 31, 2015
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WILAYA YA KINONDONI
Anwani ya Simu:
2170169/2170183

Unapojibu tafadhali Taja

OFISI YA MKUU WA WILAYA KINONDONI
1 MTAA WA MINAKI,
S. L. P. 9583,
14881 DAR ES SALAAM.
24 Machi, 2015

PRESS RELEASE: KINONDONI TALENT SEARCH. KIPAJI CHAKO. AJIRA YAKO

IMETOLEWA NA: MKUU WA WILAYA – KINONDONI

TAREHE: 31.3.2015 SAA 4 ASUBUHI.

Mnamo tarehe 28 mwezi wa pili nilipokabidhiwa rasmi ofisi, nilitangaza mambo niliyoyaona yanafaa kupewa kipaumbele ambayo yaligawanyika katika maeneo matatu; Kwanza, utekelezaji wa shughuli za kila siku za serikali yaani: Administrative duties, pili, ufuatiliaji wa masuala ya usalama wa raia na mali zao (security) na tatu, maendeleo ya makundi yote ya kijamii (social-economic development affairs). Katika kutekeleza mambo haya matatu yapo mambo niliyoyaona ni vyema kuanza nayo, ikiwemo kushughulikia migogoro ya ardhi, ujenzi wa maabara na barabara, PF3, usafi, michezo, maji na mambo kadha wa kadha ambayo katika mpango wangu wa tarehe 28 yanajieleza kwa kina. Leo nimewaita kuongelea habari moja muhimu, kwani naamini kama serikali upo umuhimu wa kutilia mkazo vipaji, kwani katika karne hii ya 21 asilimia mia moja ya maisha ya watanzania na dunia kwa ujumla, yanaendeshwa na ubunifu unaozaliwa katika vipaji, na kwa kutumia ubunifu ama vipaji tuna uwezo kabisa wa kupunguza ama kufuta tatizo la ajira nchini.

Sasa basi, katika kutambua na kutekeleza adhima hii ambayo katika ngazi ya kitaifa imekuwa ikisimamiwa na kuhimizwa vyema na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ofisi yangu inayofuraha kuwataarifu vijana wote wa Kinondoni juu ya ujio wa Kinondoni Talent Search. Kinondoni Talent Search ni mpango wenye lengo kuu la kuwatambua vijana waishio kwenye Wilaya ya Kinondoni wenye vipaji vya kuimba, kucheza na kuchekesha ambao wengi wao wapo katika mazingira magumu ya kiuchumi jambo linalowafanya kushindwa kuonyesha vipaji vyao mwisho ndoto zao kufifia. Hivyo, lengo kuu la mpango huu ni kuwawezesha kupata njia za kutimiza ndoto zao kupitia uwezo wao. Kwa ufupi ni kwamba, Kinondoni Talent Search inalenga kwanza, kuwatengenezea nafasi za mafanikio vijana wenye vipaji, kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na wadau muhimu waliopo kwenye sekta zao. Lakini kubwa zaidi, kutoa hamasa kwa vijana wote wa Wilaya ya Kinondoni na Tanzania kwa ujumla juu ya umuhimu wa kuendeleza vipaji vyao, kuepuka mambo yanayoweza kuviua na kuharibu malengo yao ya baadae, mfano matumizi ya dawa za kulevya, ngono zembe na vitendo vya uporaji. Bila kusahau kuwakumbusha vijana wote kuwa ukimiliki kipaji unakuwa unamiliki ajira, ni kujua tu namna ya kukitumia ili kikufae na kukufikisha utakapo, na ndio maana kauli mbiu ya mpango huu ni: kipaji chako, ajira yako.

Leo kupitia mkutano huu na waandishi wa habari ndio rasmi nitakuwa nimezindua mradi huu wa Kinondoni Talent Search, ambapo, ili kuhakikisha mradi unafanikiwa kwa kiwango cha juu na kufikia lengo, nimetengeneza kamati maalumu yenye wajumbe kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya wasanii ambao wana uzoefu zaidi katika Nyanja ambazo tunazigusa kwenye mpango huu. Kwa ufupi, kamati itahusisha:-

• Afisa utamaduni-Manispaa ya Kinondoni.

• Afisa habari – Manispaa ya Kinondoni

• Peter msechu Mwanamuziki wa Bongofleva.

• Jokate Mwegelo – Mwimbaji/mbunifu.

• Mc-pilipili - Mchekeshaji.

Kinondoni Talent Search itatumia jumla ya mwezi mmoja na nusu toka kuanza kwake mpaka kumalizika. Na muda huu utajumuisha: shughuli za utafutaji vipaji ambapo tutaanzia kwenye ngazi ya Kata, kutoka kwenye jumla ya Kata 34 tulizonazo, mafunzo kwa washiriki, kuwapa nafasi washiriki ya kukutana na wadau wakubwa na muhimu kutoka kwenye taasisi mbalimbali zinazofanya mambo yanayoendana na fani zao, na mwisho kwenye kufunga zoezi tutafanya tukio kubwa lenye hadhi ya kimataifa litakalowapa vijana wote nafasi ya kuonyesha vipaji vyao mbele ya Mabalozi wa nchi mbalimbali kama sehemu ya mkakati wa kuwasogeza wasanii wetu kwenye anga za kimataifa kwenye kazi zao, wasanii wakubwa waishio Wilaya ya Kinondoni, wafanyabiashara wakubwa kutoka Wilaya ya kinondoni na vyombo vyote vikubwa vya habari kutoka hapa nchini na nje ya Tanzania.

Mwisho lakini si kwa umuhimu, niwaombe sana ushirikiano wenu wa karibu katika mchakato wote huu, kwani ninaamini waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika kuwaunganisha wananchi na Serikali hasa katika masuala muhimu yenye maslahi ya nchi kama hii, kwani jaribu kufikiria tu, ukivumbua vipaji vipya, utakuwa umevumbua biashara mpya za sanaa na utakuwa umevumbua ajira mpya kwa vijana na mwisho utakuwa umeimarisha uchumi wa kijana mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kupitia kodi watakazolipa.

Imetolewa na:
Mh. Paul Makonda
Mkuu wa Wilaya Kinondoni.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments