TAMKO LA VIONGOZI WA KIROHO KUTOKA MKOA WA MBEYA KUHUSU MUSTAKABALI WA TAIFA LETU.
Ndugu wana habari:
Habarini za asubuhi:
Bwana Yesu asifiwe:
Tulio mbele yenu ni wachungaji na viongozi wa kiroho kutoka mkoa wa Mbeya.
Awali ya yote tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uzima na kutukutanisha nanyi leo hii.Ninyi ni watu muhimu katika jamii na tunawashukuru kwa kuitikia wito wetu.Tunatoa pongezi za dhati kwenu kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuelimisha jamii kupitia kalamu zenu.
Lengo la uwepo wetu hapa leo hii ni kuwaomba ninyi vijana wetu mtufikishie maoni yetu juu ya suala Zito lililopo mbele yetu Mwaka huu.
Kama mnavyofahamu Mwaka huu ni Mwaka wa uchaguzi,tumeona ni vema tukatumia nafasi yetu kama viongozi wa kiroho kutoa maoni yetu pamoja na kuwaomba Watanzania wote waendelee kuiombea nchi yetu ifanye uchaguzi kwa amani.
Ni ukweli usiofichika kuwa taifa letu linapita katika majaribu mazito katika kipindi hiki mfano Migogoro ya Kidini,Kukithiri kwa rushwa katika secta mbalimbali na maeneo muhimu ya utoaji huduma kwa jamii.Taifa letu linapita katika kipindi kigumu kilichogubikwa na mmomonyoko wa maadili kwa viongozi pamoja na kushika kwa kiwango cha elimu.
Ndugu wana habari,sisi viongozi wa kiroho Tunaamini njia pekee ya kuondokana na matatizo yote haya ni kumtanguliza Mungu mbele ili aweze kutupatia ili aweze kutupatia viongozi wenye hofu ya Mungu.Viongozi wasiokuwa na ubaguzi wa kidini,kikabila ama kikanda na zaidi viongozi watakaoweza kuwaonganisha watu wote.
Taifa letu linahitaji mtu msafi asiyekuwa na chembe ya mashaka macho ni na masikioni Mwaka Wa tanzania.Huyu Ni kiongozi anaechukia rushwa na mwenye uwezo wa kuikemea hadharani pasipokuogopa hata marafiki zake.
Ndugu wanahabari,sisi viongozi wa Kiroho kutoka mkoa wa Mbeya tunaunga Mkono na tunaipongeza ASASI YA UTAFITI WA KIELIMU (TEDRO) kwa kuona umuhimu wa ushiriki wa vijana katika siasa na namna ambavyo jamii inavyowapokea.
Ndugu wanahabari,kwa mujibu wa maandiko matakatifu Biblia inatuambia mdogo atamtawala mkubwa,kwa mfano Yakobo na Esau ambapo Yakobo alichukua nafasi ya Esau ambae alikuwa mkubwa.
Pia hata mfalme Daudi ambae alikuwa kijana mdogo,shujaa,hodari na aliyekuwa amesahaulima katika watoto wa Yese,ndiye aliyechukua nafasi ya ufalme licha ya udogo wake japo walikuwepo ndugu zake WA kubwa.
Ndugu wanahabari,sisi tu naamini kwamba Mungu hutumia wadogo kuleta mabadiriko kwamfano Mh MWIGULU LAMECK NCHEMBA,Naibu Waziri wa fedha kwamaneno yake na matendo yake pamoja na historia yake ya kukemea hadharani rushwa,ubadhirifu wa Mali za umma na matumizi mabaya ya madaraka amekuwa na misimamo wa pekee katika kusimamia kauli zake kwa maslahi ya umma..mfano sakata la ESCROW iliyosababisha upotevu mkubwa wa fedha za umma na kupelekea wananchi kukosa imani na serikali yao.Ni Mwigulu Nchemba ndani ya serikali aliyejitokeza hadharani kuamuru kukemea suala hili na kuamuru waliochota fedha hizo warudishe.
Vilevile kwasababu ya uzalendo wake na upendo wake kwa Taifa letu,hata maandiko matakatifu yanatuambia "Asiyependa wa kwao hafa kabisa kuliko yule asiyeamini".
Ndugu wanahabari mtakumbuka hata Hayati baba wa Taifa mwl JULIUS NYERERE katika umri mdogo wake aliweza kusimamia Mabadiriko makubwa katika Taifa letu.Ni katika umri wake mdogo mwalim aliweza kupiegania Uhuru wa nchi yetu na Uhuru wa nchi nyingine barani Afrika.
Ndugu wanahabari ifahamike ya kwamba kiongozi yeyote hakumbukwi kwa muda mrefu aliokaa madarakani bali hukumbukwa kwa matendo na matunda aliyoyaleta kwa muda mfupi.
Ikumbukwe Waziri mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine alikaa muda mfupi madarakani lakini aliyoyafanya ni makubwa na yanakumbukwa vizazi hadi vizazi.
Ndugu wana habari,sisi viongozi wa kiroho tunapenda kumtia moyo na kumuombea kwa mwenyezi Mungu aongeze jitihada katika kutetea haki za wanyonge. Pia tunaungana na watanzania wote wanaomshawishi na kumtaka agombee ukuu wa nchi kwa tunaamini Mungu huwainua wale wanaoonekana wadogo,Kama alivomuinua Mfalme Daudi.
Asanteni Sana kwa kutusikiliza.
Ni sisi
WACHUNGAJI
Gilbert Mwampiki- Kanisa la Baptist
Waziri Mwamwage-Kanisa la Nazareth
Nangisyaga Mwabulambo-Kanisa la Morovian
Amulike Kamendu-Kanisa la Pentecoste
Joseph Mwang'onda-Kanisa la TAG
Gastor Mwaihuti- Kanisa la Carvary
Emmanuel Mwalyego-kanisa la Huduma Tano.
Tar.11 February 2015
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments