[wanabidii] Maswali 25 kwa Mheshimiwa Edward Lowassa

Friday, January 16, 2015
Maswali 25 kwa Mheshimiwa Lowassa
Watanzania wengi tumepata kuwaelewa japo kwa uchache na kuwajadili wanasiasa wengi katika waliojitokeza kuonyesha nia ya kutaka kiti cha Urais wa awamu ya tano kutokana na michango yao mbali mbali bungeni na mahojiano ya hapa na pale. Lakini inapokuja kwa Mheshimiwa Edward Lowassa ambae ni moja ya wanaotajwa na waliojitaja kuwa wanautaka Urais wa Awamu ya tano wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania, tumekuwa tukimsemea mambo mengi kwa kuwa zaidi ya harambee mbali mbali, amekuwa kimya kwenye kuchangia bungeni, au kutoa misimamo yake kwenye vipindi mbali mbali vya radio na Tv vinavyojadili siasa. Natamani siku anipe ruhusa nimuulize maswali haya yafuatayo ili tumsikie yeye mwenyewe maoni yake na misimamo yake tupate "reference" badala ya kuishi kwa maoni na maono yetu sisi kuwa lowassa ana msimamo huu na ule..

1. Kwanza ningependa kujua wasifu wako binafsi na kama baba wa familia yako

2. Unaweza mtambua mtu kwa kuangalia Rafiki zake waliomzunguka, Je mheshimiwa Lowasa marafiki zako wa karibu ni akina Nani

3. Nje ya siasa Je una biashara nyingine unafanya? Je kwa kupitia kipato chako kuna uwekezaji wowote umefanya Watanzania wakapata ajira?

4. Je kipato chako na matumizi yako ni matunda ya mishahara na marupurupu ya kuajiriwa serikalini?

5. Kipi unachoweza jivunia baada ya kuwa waziri wa maji kwa muda wa miaka 5, kuna mabadiliko yoyote uliyafanya?

6. Je wewe ni muumini wa Mwalimu Nyerere?

7. Una maoni gani juu ya azimio la Arusha?

8. Umeshakuwa waziri mwenye dhamana wa maendeleo ya makazi ya watu na baadae waziri mwenye dhamana wa Umaskini, Je ni kipi cha kujivunia katika uongozi wako huo uki"reflect" na hali iliyopo sasa?

9. kwa nini Urais? Je mabadiliko unayotaka kuyafanya hayawezekani wewe ukiwa mwanajamii, mbunge, na waziri?

10. Je unakubaliana na maoni ya wengi kuwa kwa miaka 50 sasa serikali ya CCM Imeshindwa tatua tatizo la maradhi na umaskini? Kama ndio wewe kama kiongozi ndani ya CCM uliyeanza madaraka tangu miaka ya mwisho wa 80 mpaka leo unayo nafasi ya kulaumiwa? 

11. Wasifu wako unaonyesha tangu umeingia serikalini, ni wizara 1 tu umekaa kwa muda wa miaka mitano, zingine zote hikumaliza miaka 3, ukahamishwa au ukajiuzulu, kwa mfano AICC mwaka 1, sheria na mambo ya bunge miaka 3, ardhi na maendeleo ya jamii miaka 2, mazingira na umaskini miaka 3 na mwisho uwaziri mkuu miaka 2 na nusu, ufupi huu unatokana na Utendaji wako, imani ya muajiri wako, au ni mikataba ya kazi ambayo hupewa?

12. Tumemskia mara nyingi ukisema nchi hii inakosa kiongozi mwenye Maamuzi magumu, ukitumia mifano michache tuelezee maamuzi magumu ni yapi kwenye kuwaletea maendeleo Watanzania

13. Je unazichukuliaje kamati teule za bunge na ripoti za kazi walizotumwa

14. Kama Wewe Lowassa ungekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania leo hii baada ya ripoti ya Escrow kutolewa na "kamati" ya Bunge ungemchukulia hatua gani waziri Mhongo na waliohusishwa kwenye kashfa ya Escrow na je ungekuwa na Maamuzi tofauti na yale aliyoyafanya Rais wa sasa?

15. Je unaikubali ripoti yakamati ya PAC? Kama ndio, kwa nini si kamati ya Mwakyembe

16. Mwaka 1995 Mwalimu Nyerere kwa Maoni yake binafsi alikuengua kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Urais, miaka 10 baadae, Rais kikwete akakuteua kuwa waziri mkuu, kuonyesha kuwa Mwalimu hakuwa sahihi wabunge wakakupitisha kwa kishindo kwa kura 312 kati ya 314, swali ni je, kwa nini miaka mitatu kasoro baadae wabunge walewale wamtuhumu mtu waliyempitisha kwa kishindo kwa sababu ambazo wewe unasema si za msingi. Nikikunukuu "tatizo ni huu uwaziri mkuu", kwa nini wakugeuke kutaka uachie uwaziri mkuu? Na je Nyerere aliona mbali?

17. Moja ya matatizo makubwa ambayo Watanzania wanalia nayo na ndio yaliyotufikisha hapa ni Rushwa na Ufisadi, Je ipo record yoyote kuwa kuna sehemu yoyote hapa Duniani ulishawahi tamka kukemea Rushwa?

18. Na je unapinga Rushwa na Ufisadi? Katika msimamo wako wa Maamuzi magumu, tukikupa nchi unahisi ni vipi wala Rushwa na Mafisadi utawatambua na vipi utawahukumu ( swali la msingi ni kuwa ipi itakuwa mbinu yako ya kupambana na Rushwa na Ufisadi)

19. Je kwa maoni yako, mikataba ya gesi asilia, mafuta, madini na nishati inafaa iwekwe wazi au iwe siri

20. Kuna minong'ono ya hapa na pale kuwa ipo sehemu ulitamka kuwa ulijiuzulu kumficha Richmond mwenyewe na kuna mtu alikuwa anaijua Richmond, kwa kuwa Wewe unajinadi kuwa ni muumini wa kufanya Maamuzi Magumu, Je Unaweza fanya maamuzi magumu sasa kwa kumtamka hadharani aliyekuwa anaijua Richmond na aliyeilinda Richmond pale ulipotaka vunja mkataba? Kama huwezi sasa kwa nini tukuamini mpaka tukupw nchi ndo utaweza?

21. Kwa kauli zako Ajira kwa vijana ni Bomu, Mheshimiwa ni Rahisi kuonyesha udhaifu kuliko kuuondoa, je ni Ipi mbinu yako au maoni yako unahisi ni njia sahihi ya kuongeza ajira kwa vijana kuzuia bomu lisiripuke

22. Wakati wa kuukaribisha mwaka 2014 ukiwa kijijini monduli ulisema "tulihudhunika pamoja, tutacheka pamoja" je wakati tuliohudhunika pamoja ni upi? Miaka 53 baada ya uhuru, awamu ya Kikwete au ulipojiuzuru uwaziri?

23. Upi msimamo wako katka idadi ya serikali? Moja, mbili au Tatu?

24. Tukirejea hotuba yako ya kujiuzulu uwaziri Mkuu mwaka 2008, ni sahihi kusema mtazamo wako ni chama kwanza Watanzania baadae?

25. Nini msimamo wako kuhusu ndoa za jinsia moja

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments