[Mabadiliko] Kisa Cha January Makamba..!

Monday, January 19, 2015


Ndugu zangu,

Nimetafakari kufanya uchambuzi wa kitabu nilichosoma chenye kumhusu January Makamba.

Lakini, kabla ya kuendelea kuifanya kazi hiyo, na baada ya kufikiri, nikakikumbuka kisa alichosimulia January pale Nkrumah Hall siku ile ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wetu. Nami nilialikwa kama mzungumzaji.

January alipopewa muda wa kuongea alianza na kusimulia:

" Jamani msituone wanasiasa tunakumbatiana mkadhani tunapendana sana. Tukivua mashati yetu na mkatazama migongo yetu, basi, mnaweza kuona makovu ya mishale tunayochomana huku tukikumbatiana!"- January Makamba.

Na mimi leo ninapotafakari kuyaweka kwenye maandishi yale niliyoyachambua kwenye maandiko ya Privatus Karugendo kumhusu January, kuna mawili nayaona;
Mosi, kwa vile nilishaweka wazi, kuwa nimeyaona makusudio mawili kwenye maandiko kumhusu January, kuwa la kwanza ni kuweka wazi kusudio lake la kuwania kiti cha Urais. Na la pili ni kujimbanua.

Hivyo, unapobaki hapo, na unapoziangalia ishara za nyakati na upepo wenye kuzisukuma. Nayaona matokeo mawili ya uchambuzi nitakaoufanya; Mosi, uwepo wa matumizi mazuri ya uchambuzi wangu, na pili, matumizi mabaya ya uchambuzi wangu. Na kosa langu litakuwa ni kushindwa kusoma ishara za nyakati. Mapokeo ya uchambuzi wangu kuhusiana na kitabu hiki, nikifanya sasa, yaweza kuwa na sura moja katika wakati huu tulio nao, na nifanya mwezi Juni, basi, yatakuwa na sura nyingine kabisa.

Maaana, kwenye maisha ya kisiasa, January ana marafiki na maadui. Yumkini, marafiki na maadui wa January kisiasa nao wameshakisoma kitabu hicho, pengine zaidi ya mara mbili. Kuna wenye kusubiri kwa hamu uchambuzi yakinifu unaotokana na fikra ' gombanishi' za Mwenyekiti wa kijiji cha Mjengwablog. Ili nao wazitumie ipasavyo kwenye kukidhi mahitaji yao ya kimkakati.

January ni jamaa yangu, na sina uadui na wote wengine wanaokwenda kushindana na January kwenye kinyang'anyiro cha Urais. Nisingependa uchambuzi wangu uonekane kuwa umechangia kwenye kumkandamiza January au kumbeba January.

Hivyo, kwa kipindi hiki nimechagua kuchambua ' Kimya Kimya..!'

Maggid,
Dar es Salaam.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye7qX-EgQ%2BZsu7EAs%3DrrHUmM5giE3wixM8y78ZphXtoDfQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments