[wanabidii] Naomba msaada wako nifanye nini?

Sunday, December 14, 2014

Naomba msaada wako nifanye nini?

Mimi ni mke wa mtu, na mume wangu tunapendana sana. Juzi
niliondoka kwenda kazini nikamuacha mume wangu ana angalia TV. Sikufika mbali gari likazima ghafla. Nikalazimika kutembea kwa miguu kurudi nyumbani nikamwambie mume wangu anisaidie.

Nilipofika nyumbani sikuamini macho yangu baada kumkuta mume wangu na binti wa jirani yetu. Nilimkabiri mume wangu na kwa bahati nzuri kakubali makosa kuwa uhusiano wao una mwaka sasa, lakini cha ajabu amesema atalazimika kumuacha huyo binti pole pole ili asimchanganye kisaikolojia kwa kuwa bado mdogo.

Je hii ni sawa? Nifanye nini? Naomba
ushauri ndugu yangu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments