MAWAZO 'MGANDO'... TRADITIONAL THINKING..!
ERIC SHIGONGO aliwahi kuja kuongea na vijana kanisani kwetu tarehe 3 April, 2011 siku ya Jumapili na mimi nikawa miongoni mwao (Huwa tuna Intellectuals Gathering kanisani kwetu kila Jumapili ya kwanza ya kila mwezi.) Alipomaliza kuzungumza wakati watu wanaomba contact zake mimi nilimfata nikaomba asaini kwenye diary yangu na aniandikie ujumbe wowote. Nilitaka kubaki na ukumbusho wa maandishi kutoka kwa mtu adimu kama yeye! Kila nikisoma ujumbe ule nazidi kuona huyu ni mtu adimu.
'Kila mtu' anaifahamu story ya Shigongo. Lakini nimejifunza kitu kikubwa kwake kuwa ni mtu asiye na mawazo mgando! Ametoka katika familia duni mno kama ilivyo kwa wengi wetu wewe ukiwa mmojawapo ingawaje unajitutumua Instagram na picha za Merrybrown au Century Cinemax, na "Xoxo" nyingi wakati wazazi wako kijijini mara ya mwisho kunywa Soda ilikuwaa Krismas ya mwaka 98 ukiwa darasa la tatu! Uongo?? Sasa umeshamaliza Degree yako CBE na umepata kazi hapo MICROFINANCE basi kila siku instragram na TECNO yako TECNO yenyewe N- Series. Pshuuu..
Sasa yeye alichagua kutowaza mawazo yaliyopitwa na wakati.
Alichagua bidii badala ya malalamiko. Yeye alichagua kuona mbali badala ya kupumbazwa na maisha ya mjini hususan wanayoishi "wasomi".
Wasomi wengi wana mawazo mgando sana...
Wanawaza bila kupata ka-masters maisha hayawezi kwenda.
Wanawaza bila AJIRA maisha hayawezi kwenda mbele!
Wanawaza bila kufoji safari na risiti maisha hayawezi kwenda mbele!
Wanawaza bila kutembea na bosi maisha hayawezi kwenda mbele!
Wanawaza bila kukopa gari huwezi kupata hela ukanunua mwenyewe!
Wanawaza bila kajiriwa mafanikio hayawezi kuja!
Wanawaza lazima kazi ufanye Vodacom au NBC au Barrick ili uheshimike hapa mjini! (Siku hizi nasikia Serikalini ndo dili)
Na sasa wanawaza piga ua lazima waingie kwenye siasa ili wapige hela!
Wanawaza ili kufanikiwa kwenye biashara lazima usome CBE au IFM uwe na degree ya hayo mambo.
Nauliza tena: Kwani Shigongo ana degree ya CBE? Na siku mkisikia CBE wanataka kumpa Degree ya Heshima mtaanza ooh kwa nini.. Ooh wanapendelea sisi tunalia na SUPP yeye kwa nini apate bure.. Pshuuuu!
Hivi ushakaa na Shigongo hata dakika mbili kuongea? Sasa kati yako wewe mwenye degree ya CBE umeajiriwa tu hapo Microfinance mwaka wa nne sasa hivi hata Vitz tu huna na yeye asiye hata na nusu ya Elimu yako na ana miliki biashara kubwa, ni mwajiri wa wenye degree kama wewe, na anatembelea Range nani alistahili hicho cheti?? Upo tu Microfinance kazi yako kupigia simu wanaodaiwa wakati we mwenyewe unadaiwa kuanzia Bodi ya mikopo, hapo kazini kwenyewe, huko Kimara ulikopanga ndo kuanzia mangi dukani mpaka muuza genge wanakudai, upo tu Microfinance na T-shirt yako ya Microfinance sijui nini nini microfinance. Umekuwa tu bango la kutangaza Microfinance njiani. Ukiitwa na wenzako wasio na mawazo mgando njoo tukutane bana tuongee kidogo kuhusu mawazo ya biashara unadai uko busy.
Uko busy na Account yako Benki nayo iko busy kuingiza hela?? Ooh sina muda. Kaa tu hapo.
Kiti unachokalia si chako! Ni cha mwenye mawazo yasiyo mgando.
Meza na computer vyote si vyako.
Mpaka kalamu unayoandikia si yako ni ya mwenye ofisi yake. We cha kwako hapo ni kitambaa cha kufutia jasho (maana hata AC zimekufa ofisini) na kimkoba chako ambacho hakina kitu cha maana huko ndani zaidi ya chenchi ya daladala uliyorudushiwa asubuhi na space ya kuwekea hiyo TECNO. Mungu kila siku anakuletea watu wanataka kukushauri mambo muhimu wewe ooh boyfriend wangu alishakataa mi nisikutane na wavulana. Excuse me! Boy-whaaat???
Pshuuu..
Mkaka naye akiambiwa aisee njoo tuonane kuna fursa za biashara huko mikoani, hataki hata kusikia! Yeye anataka umwambie biashara ya kufungua banda la chipsi city centre. Basi! Au umwambie kuna fremu Mwenge anataka auze chaji na cover za simu na kuchajisha simu. Fremu laki 5 kwa mwezi. Kwa mwaka milioni 6! Sasa hivi watu wana power bank hivi nani atakuja kuchajisha simu kwako na atakulipa sh ngapi?
Enyi "WAGALATIA" hivi nani amewaloga?? Mbona elimu mnazo?
Sasa SHIGONGO siku hiyo tarehe 3.4.2011 alisema maneno yafuatayo:
(Uyaandike na wewe. Mi nisingeandika ungeyapata?)
1. MANY INTELLECTUALS HAVE OUTDATED TRUTH (Jamani kweli si kweli? Hapa siongei pima mwenyewe)
2. MANY INTELLECTUALS HAVE WALLS AROUND THEM (Wasomi wamezungukwa na kuta. Anachokijua yeye ndo hichohicho. Usimletee habari zako sijui una wazo la nini, NO! Ukimwambia tu Unajua Robert Kiyosaki anasema...yaani kabla hata hujamaliza utasikia "Aah ushaanza sasa")
3. LEARNING IS AN ENDLESS PROCESS EVEN UNTO DEATH - EVEN THERE YOU HAVE TO LEARN HOW TO DIE
(Unasikia maneno hayo?)
4. SPECIALIZATION IS FORMAL EDUCATION'S WAY OF PUTTING YOU IN A CORNER OUT OF WHICH YOU CANNOT OPERATE (Mnaosomea special fields. Yaani we hutajua kitu kingine zaidi ya hicho afu wanakuita mtaalamu. Mbwembwe tu)
5. DON'T BE COMPLACENT. COMPLACENCY KILLS. (Unatafuta dictionary? Yaani hii point ndo inawaua wasomi)
6. Sasa sikia hii: NOTHING GOOD WILL HAPPEN TO YOU IF YOU DON'T GET TIRED OF WHAT YOU ARE. LIVE A LIFE WITH AN IMPACT. ASK YOURSELF: WHAT MORE CAN I BECOME? (We umekaa tu hapo. Yaani hakuna cha maana unachosubiri kwa hamu hapa duniani sasa hivi kama simu ya fundi cherehani akupigie kukwambia kuwa gauni lako la kuendea kitchen party ya rafiki yako liko tayari! Hivi Mungu akiamua akuchukue utakataa?)
7. WHEN YOU GET A CHALLENGE IT IS NOT TIME TO LOOK FOR TRUTH. IT'S TIME TO APPLY IT (Jamani jamaa kichwa au siyo kichwa?)
8. ALWAYS TELL YOURSELF: I AM NOT THERE YET, I AM ABOUT TO GET THERE. ALWAYS (Sasa mwenzetu unajiona umeshafika)
9. DO THE RIGHT THING EVERY SINGLE DAY. NO MATTER HOW SMALL IT IS
Na hii ifuatayo sasa usipoielewa basi imekula kwako:
10. RICH PEOPLE MAKE THEIR MONEY BETWEEN 5PM AND MIDNIGHT.
Hivi kati ya saa kumi na moja jioni hadi saa sita usiku huwa unafanya nini cha maana.
Boooy! Huyo ndo ERIC SHIGONGO sasa.
Jamani ni kichwa adimu au nakosea?
Sasa na wewe huwa unaongeaga point mbele za watu? Au wewe ukiongea watu wanawaza hiyo degree uliipataje!
Una chochote cha maana ulichoongea mwaka huu toka umeanza zaidi ya kuongelea Escrow hiyo nayo hata huielewi. Upo tu hapo! Maneno muhimu maishani mwako yamekuwa maneno ya konda wa daladala saa mbili usiku anapouliza "KIMARA MWISHO?" Na wewe unaitikia: "SHUSHAAA!"
Acha mawazo mgando ndugu yangu.
Acha kujitumua Instagram. Kubali mawazo mapya!
Msalimie bosi wako wa hiyo MICROFINANCE.
Peace!
ANDREA MUHOZYA
DAR ES SALAAM, TANZANIA.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments