Wizara ya Fedha imewashtukia wawekezaji wanaobadili majina ya kampuni kwa lengo la kutaka kukwepa kulipa kodi baada ya kuamua kubadilisha sheria.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, (pichani) alisema hayo katika mahojiano na Redio One kwenye kipindi cha Kumepambazuka kuhusu mbinu zinazotumiwa na baadhi ya wawekezaji kukwepa kulipa kodi kwa kubadili majina ya kampuni.
Mwigulu alisema serikali ilishachukua hatua kwa kubadilisha sheria ambayo sasa haitoi fursa kwa wawekezaji kupata unafuu wa kodi anapobadili jina la kampuni.
"Kubadili jina haihusiani na badiliko lolote la jina la kampuni, akibadili jina kodi ipo pale pale, kwa hiyo wanaobadili majina ya kampuni wanajidanganya watatakiwa kilipa kodi kama kawaida kwa mujibu wa sheria," alisema.
Mwigulu alisema kutokana na mabadiliko hayo ya sheria mwekezaji au mtu yeyote akibadili jina la kampuni mmliki wa kwanza ndiye anakuwa bado anatambuliwa na akiuza hisa bado taifa itanufaika kwa kodi.
Alisema serikali imejipanga kuhakikisha kila mtu analipa kodi kwa mujibu wa sheria na kwamba serikali haitakubali kuona baadhi ya wawekezaji wanakwepa kulipa kodi na kuikosesha nchi mapato.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments