LUDOVICK WA CHADEMA: NILIKUWEPO IGUNGA.-GAZETI CHANGAMOTO.
Sehemu ya 3
Vyama vya CCM na CHADEMA vimekuwa vinatupiana lawama juu ya matukio haya mabaya kwenye siasa za nchi yetu. Mimi mwenyewe nilikuwepo hapo Igunga kwa muda wote nikiwa na kazi maalumu. Muda mwingi nikiwa na Lwakatare hasa kuratibu mfumo wa usalama na ulinzi. Tulikuwa tukiendesha mafunzo kwa Vijana wa Brigade waliokuwa wameitwa na chama toka sehemu mbalimbali za nchi. Katika mafunzo hayo tuliwapatia Brigade code names na kupanga uendeshaji wa maeneo ya kampeni kwa mfumo wa kijeshi tukiwa na RV kadhaa. Wakati fulani kuelekea mwisho wa Kampeni Lwakatare aliugua na kupelekwa Dar es salaam. HENRY KILEWO akawa ndiyo kiongozi wa ulinzi na usalama na mimi nikiwa msaidizi wake. Kutokana na mapambano kuwa makali na kuhofia usalama wetu, nilikuwa nalala mafichoni Nzega badala ya Igunga. Nilifahamu juu ya matukio ya kumwagiwa Tindikali kwa Mussa Tesha na niko tayari kutoa ushahidi mahakamani iwapo nitahitajika. Kwa kuwa jambo hili liko mahakamani hatuwezi kuliongelea hapa. Tulipoteza uchaguzi ule na Peter Kafumu kuwa mbunge wa Igunga. Baada ya tathmini haikuchukua muda tena tukaenda kwenye uchaguzi wa UZINI kule zanzibar, ambajo nako tulipoteza kwa RAZA. Kisha muda mfupi tu tukaenda ARUMERU Mashariki ambapo tulishinda uchaguzi na kumpata mbunge wa CHADEMA. kisha hapo tuliendelea na shughuli za kawaida za chama Dar es salaam na sehemu mbalimbali. Haina maana kuzieleza katika makala kama hii. Itoshe tu kusema tu kuwa zilikuwa shughuli nyingi na mbalimbali nyingine zikihatarisha maisha yetu na ya wengine. Wakati wa kufanya kazi hizi nilikuwa nikienda Lumumba ofisi ndogo za CCM mara nyingi sana kwa ajili ya kazi ya chama chetu.kwa waliokuwa wakiniona bila kujua nilikuwa nikifuatilia nini labda ndiyo hao waliojenga dhana ya mtu kuweza kutumiwa na CCM, japo hilo halikuwahi kuwa. Kwa sababu hiyo nilikuwa na mahusiano na baadhi ya viongozi wa CCM makao makuu. Ni ajabu kwamba wakati fulani kuna mbunge wa CHADEMA mwanamke alitoroka kikao cha kamati kuu na hakuwa ameaga. Nilipoambiwa kumtafuta nilikuja kugundua alikuwa hoteli moja chumbani akiwa na kiongozi mwandamizi wa CCM ambaye wakati ule alikuwa mjumbe wa kamati ya siasa na maadili. Ikiwa alikuwa huko kwa mambo ya unyumba ama kuuza siri za kamati kuu, hatuwezi kuandika hapa. Ni wakati huu pia ambapo, kutokana na kazi yangu katika mjengwablog nilipata kuwa ninakutana na wana habari katika masuala ya kihabari. Hata kama kuna ambao hawawezi kunifahamu, lakini mimi kuna ninaowakumbuka kutokana na kuwa tunakutana mara kwa mara katika matukio ya kihabari. Kama baadhi wanavyoweza kukumbuka nimekuwa nahusishwa kuwa na mahusiano na mengine yenye mashaka na baadhi ya watu katika vyama vya siasa na hata habari. Mojawapo ni kuwa nina mahusiano na Mwigullu Nchemba Naibu katibu mkuu wa CCM. nini mahusiano hayo yanalenga? ninamfahamu vipi Mh. Mwigullu Nchemba? Nitasimulia wiki ijayo.
Mawasuliano 0757 314961
--Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACMr6QjBSFMdRatAOqP6pnaObN4RidR9WuLKmhGpGMuhRf%3Dz4g%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments