[Mabadiliko] Neno Fupi La Usiku: Kushoto Na Kulia Ni Itikadi...

Wednesday, December 10, 2014


Ndugu zangu,

Kusimama kwenye Ujamaa ni Kusimama kushoto kiitikadi. Kuna tuliozaliwa kwenye Ujamaa, tumekulia kwenye Ujamaa, na tutakufa Wajamaa.Itikadi ni Imani pia. Ndio maana ya kusemwa, kuwa Ujamaa ni Imani.

Na kwenye siasa, unapozungumzia Kushoto na Kulia ina maana ya political distiction. Kwenye lugha ya kiimani na hususan Ukristo, Kulia ni Nzuri na Kushoto ni Mbaya.

Inasemwa, kuwa Bwana alimweka kondoo Kulia kwake, na mbuzi Kushoto kwake. Kondoo ameahidiwa nchi takatifu, wakati mbuzi mahali pake ni kwenye moto usiokoma.

Na Yesu alikaa kulia kwa Mungu, kama ilivyo kwa Malaika wa Mungu, nao walikaa kulia mwa altani yenye kufuka moshi.

Lakini, kwenye lugha ya siasa, tangu zama za Mapinduzi ya Ufaransa, hali hiyo ni kinyume. Kushoto, kwa maana walio kwenye mrengo wa kushoto, wao, kwenye Bunge la Taifa, walikaa Kushoto kwa Spika wa Bunge.

Kwa ufupi kabisa, kinachotofautisha Kulia na Kushoto kwenye itikadi ni mtazamo juu ya Usawa. Tulio kwenye mrengo wa Kushoto tunaamini, kuwa Kutokuwepo kwa Usawa katika jamii ni jambo lenye kudhalilisha na lisilopaswa kuwepo. Walio kwenye mrengo wa Kulia wanaamini, kuwa Kutokuwepo kwa Usawa katika Jamii ni jambo lisiloepukika.

Walio kwenye mrengo wa kulia wanahofia sana mrengo wa Kushoto, wakati, tulio kwenye mrengo wa Kushoto tunaamini, kuwa tuko kwenye njia sahihi katika kuipata jamii yenye Usawa. Maana, Amani na utulivu haviwezi kupatikana kwenye jamii isiyo na Haki na Usawa. Hivyo, kutokuwepo kwa Maendeleo.

Na kwa vile, kwenye jamii kama ya kwetu, pengo la walio nacho na wasio nacho linazidi kupanuka, basi, itikadi ya mrengo wa Kushoto inahitajika kuliko wakati mwingine wowote. Hivyo basi, uwepo wa misingi thabiti ya itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea uliofanyiwa mabadiliko ya kimsingi.

Ni Neno Fupi La Usiku.

Maggid,
Iringa.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye7dv4kn%3Du5J8Gk6gwWiOJ1_9V1xM5zfizFp_1M0kUUJOg%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments