ZZK ni CHADEMA, ZZK ni CCM, ZZK ni ACT.
Kimenuka tena harufu imegusa mbingu, inawezekanaje mzalendo ZZK kama anavyojinasibu na washirika wake, aweze kuwa popo mwenye mabawa matatu?? Mzalendo haishi hata siku moja ktk hali ya sintofahamu kwa umma, si angeweka wazi kama kweli ni mkweli na mzalendo?
Fikiria CDM wanasema ni msaliti, dalali wa majimbo ya uchaguzi, muuzaji wa siri na harakati za chama, wakaonesha mara ngapi amekutana na CCM kufanikisha udalali wake, tukawekewa hadi namba za simu na majina ya watu aliokuwa akihujumu chama nao, akajaribu kutumia MM1, MM2 kuvuruga chama, CDM inasema ikamkamata. Hongera Shujaa Lema ambaye ulianza kwa kujilipua kunyanganga kwa nguvu za mungu hizi hizi za ndizi na nyama pale arusha ndg Mwigamba Samsoni.
Fikiria tena upanda mmoja Mkumbo kila mara anamshauri ajiunge na kugombea wenyekiti ACT, mara ACT wanadai hadharani ZZK ni mlezi wa ACT, mara makamu mwenyekiti anadai ZZK ndo mwanzilishi wa ACT, huo ni upande mwingine unaothibitisha bila kuacha shaka kuwa ZZK kama ambavyo CDM ilisema hapo juu ni msaliti na dalali.
Kwa upande wa CCM, ZZK amekuwa kijana mzuri, ameshinda bila taabu mihura mitatu, amekuwa mwenyekiti wa kamati nyeti za bunge, amekuwa akisafiri na JK kabla hajasitukiwa na upinzani na kupigwa chini na Ikulu, amekuwa akiongea na TISS mara zaidi ya kumi na moja siku ya uchaguzi hadi matokeo kutangazwa, uchaguzi mkuuu 2010. tangu 2008 hakuna hata siku moja ktk harakati za ZZK ambazo CCM imeonekana dhahiri kumkabaa kama inavyowakaba kina Slaa, Lissu, Mbowe, Lipumba, Msigwa, Wenje, Mr. II etc. ni kijana wao mtiifu wenye kuhadaa umma kuwa ni mpiganaji na mzalendo.
Ukiona anatumika sehemu kama ESCROW dili chafu ili aume na kupilizia, unakumbuka maneno yake mwenyewe eti alinongonezwa na Mwandosya, shame shame, mambo ya nchi unakubali kunong'onezwa na kuacha baadhi ya mambo?? Unakumbuka ZZK alivyounga mkono formulation ya Chenge na kuacha watu wakiuliza hata na wewe huku yuko kimya??? formulation ya Chenge hata mtoto mdogo angeomba dk 5 aliangalie sana, maana ni ya kutaka kuwanasua wenzake kama kawaida yao, ZZK alikubalije mapema hivyo kabla ya kujishutukia kuwa ameshutukiwa na kusema AKILI ZIMECHOKA, sio zilichoka siku hiyo, hapana zimechoka siku nyingi sana, ndo maana usaliti ndani ya CDM ulikamatwa kama wa kitoto.
Huyo ndo ZZK ambaye nchi inashawishiwa ni mzalendo, wasanii kwa faida yao kama Jokate watasifia ile hali lile ni pachaka kwa maneno ya EL hata kama maji yamejaa, yataisha tu maana pakacha shuruti kuvija.
Nawasilisha
==========================
Zitto atajwa bosi wa ACT
CHAMA cha Mabadiliko na Uwazi (ACT), kimetangaza rasmi kuwa muasisi wa chama hicho ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), ambaye kwa sasa bado anatambulika kuwa mwanachama wa Chadema.
Siri hiyo iliwekwa hadharani jana na Makamu Mwenyekiti wa ACT, Shabani Mambo, wakati akinadi kwa wananchi wagombea wa uenyeviti wa serikali za mitaa kupitia chama hicho kipya, katika mitaa ya Majengo pamoja na Nyasubi katika uwanja wa Lumambo.
Kutokana na kauli hiyo, gazeti hili lilimtafuta Zitto atoe ufafanuzi, ambapo alikataa kukiri wala kukanusha madai hayo ya ACT.
Hii si mara ya kwanza kwa Zitto kuhusishwa na chama hicho, ambapo Mei mwaka huu alipohojiwa na kituo cha redio cha Clouds Fm, kiongozi huyo kijana wa Chadema alikaririwa akisema hawezi kukubali au kukanusha kuwa mwanachama wa ACT, mpaka hapo kesi ya msingi dhidi ya uanachama wake Chadema itakapotolewa uamuzi mahakamani.
Aliulizwa swali hilo, baada ya kiongozi ambaye alitimuliwa Chadema pamoja na Zitto, Profesa Kitila Mkumbo, kumtaka rafiki yake Zitto kuhamia ACT na kugombea nafasi ya uenyekiti.
Profesa Mkumbo katika maoni yake kwa Zitto, alikaririwa akisema kiongozi huyo kijana hawezi kupata mafanikio zaidi ya kisiasa ndani ya Chadema, isipokuwa kama ataamua kuhama chama hicho.
Zitto alipohojiwa na Clouds kuhusu kauli ya Profesa Mkumbo, alisema yeye na Profesa Mkumbo wana mrengo wa siasa unaofanana, unaoamini katika maendeleo na maslahi ya jamii kwa ujumla na sio chama wala watu wachache.
Kampeni
Akiendelea na kampeni baada ya kueleza kuwa bosi wao ni Zitto, Mambo alidai watumishi wa Serikali iliyopo madarakani, wamekuwa na jeuri ya fedha kuliko wafanyabiashara hata kama wana mishahara midogo na kuongeza kuwa hali hiyo inatokana na ubadhirifu uliopo katika sehemu zao za kazi.
"Unakuta mfanyakazi mdogo wa halmashauri lakini unakuta anamiliki mali nyingi na huku mshahara wake ukiwa ni mdogo, ukiambiwa unaweza kushangaa hata mfanyabiashara mkubwa anaweza kutokuwa nazo sasa hebu fikiri mtu huyu anatoa wapi fedha hizo?" Alihoji.
Katika Mkutano huo Makamu Mwenyekiti huyo aliwanadi wagombea uenyekiti kupitia ACT kutoka katika ya Majengo Kati, Ali Shango pamoja na mgombea mwingine wa Mtaa wa Nyasubi, Idsam Mapande na kuongeza kuwa chama hicho ambacho ni kipya kimejipanga kuhakikisha kuwa kinashinda viti hivyo. Chanzo:Habarileo
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en ---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to
mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to
mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit
https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACChgVTyk79XzgQ0bucchnvGfq00aNb7__AfMWffFw1auRQbvQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
Share this :
0 Comments