[wanabidii] Viongozi wa UKAWA warejea CCM kwa utendaji wa Mgimwa

Sunday, November 16, 2014
VIONGOZI watatu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kata ya Lyamgungwe jimbo la Kalenga wamempongeza mbunge wa jimbo la hilo Godfrey Mgimwa kwa kutekeleza ahadi mbalimbali zilizoachwa na marehemu mbunge aliyepita Dk Wiliam Mgimwa kwa muda mfupi na kuwa katika kuonesha umoja wao wameamua kuunganisha nguvu zao kwa mbunge huyo kwa kuhama CHADEMA na kujiunga na CCM.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzao zaidi ya 20 ambao walikuwa nyuma yao kabla ya kujiengua CHADEMA na kujinga na CCM walisema kuwa sababu ya kujiunga na upinzani ilitokana na makundi ndani ya CCM na upendeleo wa uteuzi wa wagombea mbalimbali pamoja na wabunge waliotangulia kuonesha kutumia ubunge kulea familia zao badala ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo jambo ambalo mbunge Mgimwa amekuwa wa tofauti na wabunge wengine kwa kuonesha kuwajali zaidi wapiga kura wake.


Bw Mapinduzi Kalolo ambae alikuwa ni viongozi wenzake wengine waliorudi CCM ni pamoja na Katibu kata, Mwenyekiti na wajumbe na kuwa kujiunga kwao CHADEMA ni baada ya mambo ndani ya CCM kutokwenda vizuri ila kwa sasa mbunge wao ameendelea kuwaunganisha wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama.

Pia alisema walipotoka CCM kwenda CHADEMA walikuwa wameahidiwa mambo mengi na viongozi wa CHADEMA jimbo hilo la Kalenga ila baada ya kujiunga utekelezaji wa ahadi walizotoa ikiwemo ya kufungua ofisi ilionekana ngumu na chama hicho hata kuwajali kilishindwa na hivyo kuishia kuonekana si chochote katika kata hiyo zaidi ya kutumika kama karai na CHADEMA.

"Kujiunga na CHADEMA kweli tulikuwa tumepotea ila kwa sasa tumeona ni vema kurudi kwa baba na mama CCM baaba ya maisha ya kuishi kama mwana mpotevu kutushinda ....hivyo tunakuhakikishia mheshimiwa mbunge Mgimwa wewe ndio umetushawishi kuhama CHADEMA na kujiunga na CCM kutokana na kuonyesha mfano katika kutekeleza ahadi zao kwa wananchi ...Kalenga hatujapata kuwa na mbunge ambaye amefanya mambo makubwa kama wewe ndani ya miezi minne ...haya uliyofanya wewe wabunge wengine walikuwa wakishindwa kuyafanya kwa kipindi cha miaka 5 ya ubunge."

Hata hivyo Kalolo alisema kuwa ni matumaini makubwa kwao kuwa kazi iliyofanywa na mbunge Mgimwa kwa kipindi kifupi cha miezi minne ama cha mwaka mmoja wa utawala wake ni imani tosha kwao kwa kuendelea kumchagua zaidi kwa miaka mingine 10 mbele ili kuliwezesha jimbo hilo kuwa la mfano zaidi.

Hivyo alikitaka CCM kuacha tabia ya viongozi wake wa wilaya kuwaruhusu baadhi ya wana CCM kuzunguka kuwavuruga wapiga kura kwa kubeza jitihada zinazofanywa na mbunge Mgimwa na kuwa kufanya hivyo ni kukaribisha upinzani katika jimbo hilo.

Kalolo alisema iwapo viongozi wa CCM ngazi ya wilaya na mkoa watashikamana na mbunge Mgimwa upo uwezekano wa upinzani kufutwa kabisa katika jimbo hilo ambalo halijapata kuwa na historia ya kuongozwa na upinzani.

Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa jimbo la Kalenga kupitia CHADEMA, Dk Salum Kalolo alisema kuwa kuondoka kwa viongozi hao CHADEMA na kujiunga na CCM kutokana na utendaji wa mbunge huyo Mgimwa hawajakosea kwani kwa mtazamo wake kazi inayofanywa na mbunge huyo jimboni inapaswa kuungwa mkono na kila mwananchi bila kujali itikadi ya chama chake.

"Wengi walijua kuwa kutokana na ujana wake mambo ya maendeleo yasingeweza kusonga mbele ila mimi si CCM mimi ni CHADEMA kutoka sakafu ya moyo wangu ninampongeza munge Mgimwa amekuwa mbunge wa mfano katika kutuletea maendeleo Kalenga"

"Zipo changamoto mbali mbali ambazo iwapo atapewa muda wake wa kipindi japo kimoja cha miaka 5 kuanzia mwakani 2015 tungependa atusaidie kutatua ni pamoja na adha ya maji na uboreshaji wa shule za msingi ambazo nyingi hazipo katika hali nzuri."

Hata hivyo mbunge Mgimwa alisema malengo yake ni kuweka rekodi nzuri ya ubunge katika jimbo hilo la Kalenga na kulifanya kuwa jimbo lenye maendeleo makubwa ikiwa ni pamoja na kuona ndoto yake ya kuanzisha benki ya wananchi wa Kalenga inaanzishwa ili kusaidia kuwakopesha wakulima mitaji.

Kuhusu suala la maji alisema tayari katika baadhi ya maeneo ameanza kutekeleza ahadi ya maji safi pamoja na kupeleka umeme katika kata ya Mgama na Magulilwa ili kuchochea kasi ya maendeleo japo maombi yake kwa wananchi ni kuendelea kumwombea zaidi ili ndoto yake ya kuleta maendeleo ifanikiwe zaidi.


Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa kulia akipokea kadi ya CHADEMA kutoka kwa mmoja kati ya viongozi wa CHADEMA kata ya Lyamgungwe aliyehamia CCM


Mbunge Mgimwa akikagua miradi ya maendeleo jimboni kwake



Kada wa CHADEMA (kulia) akipongezwa na mbunge Mgimwa baada ya kujiunga na CCM


Mbunge Mgimwa akizungumza na wananchi wake baada ya kupokea wana chama wa CHADEMA

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments