[wanabidii] "Tusiache watu wazuri kwa kashfa zisizo na mashiko"

Thursday, November 13, 2014
Salama ndugu Mollel?
Nimekuwa nikifatilia hoja hii ya Mh.Ben juu ya mada tajwa hapo juu kwa muda sasa. Awali skutaka kuchangia ila kadri muda unavoyoyoma na michango inavyotolewa nimeona nijaribu kuweka maoni yangu kidogo hasa nikirejelea mchango wako.

Katika mchango wako hapa jukwaani umesema unadhani kauli ya Mr. Ben yaelekea inalenga kumwelezea Mh. Lowasa na hofu yako juu ya Ukawa ikiwa CCM itamuweka mtu mwingine tofauti na yeye.Sina lengo la kupingana na mawazo yako kwa kuwa kila mtu ana uhuru wa kujichagulia.Aidha kila mtu mwenye kufikiri kwa kina ni wazi anatambua fika utendaji wa Mh. Lowasa na wengine ndani na nje ya CCM kama makamanda wa chama na kama watumishi wa umma katika sekta/idara walizopata kuzitumikia.

Aidha, katika maelezo yako umeenda mbali kidogo na kueleza kuwa watu kama akina Edo Moringe Sokoine au JKN hawataweza kufit kwa kuwa eti ni wajamaa ukidai kuwa sisi wote siku hizi ni mabepari.Hapa mimi nakukatalia kwa kuwa nina imani kuwa bado tupo wengi tuliozaliwa na kuliona kama si kuliishi Azimio la Arusha ambalo kimsingi ndilo lililorasimisha Ujamaa na kujitegemea.Kimsingi binafsi ninaliishi na sitaliacha thats why kila nilipo huwa nipo na nakala yake na ninapopata nafasi kuwa nalisoma tena na tena. Hapa napenda nikukumbushe tu kuwa hata CCM bado kinaamini katika siasa ya Ujamaa na kujitegemea japo watendaji wake wanafanya kinyume kiasi cha kukufanya uamini kuwa wote ni mabepari. [Tazama Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2012 ukurasa wa 6 sehemu ya kwanza 5(3).]. Kwa mantiki hiyo nataka kusema kuwa mtu eyote atakayesimishwa na CCM kupambana na ukawa yampasa kuhakikisha anailinda na kuitetea katiba ya chama ikiwa ni pamoja na kutekeleza malengo ya chama kama yalivyofafanuliwa katika katiba hiyo.

Asante.
 
______________________________
Without "Ethical Culture" there is No Salvation for Humanity
______________________________
A D D R E S S
John J. Malata
Vikindu Teachers` Training College.
P.O  Box 16268
DAR ES SALAAM
TANZANIA 
Mobile:    +255 782366090
Blog:http://pengotz.blogspot.com/

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments