From: Novatus Kambota <novakambota@gmail.com>
Date: Thu, 13 Nov 2014 12:05:07 +0300
Subject: Mapinduzi ya umma Yataendelea Kushamiri barani Afrika
To:
Kuelekea 2030 serikali nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara zitang'olewa
Na Nova Kambota, 0712 544237
Alhamisi, 13 Novemba,2014
Dar es salaam, Tanzania
Habari kubwa hivi sasa barani Afrika ni mapinduzi ya umma
yaliyofanyika Burkinafaso, makala haya ni mtazamo wangu kuhusu
kitakachojiri kusini mwa jangwa la sahara kuelekea 2030, mtazamo huu
umejikita katika kutathimini matukio yanayoendelea kusini mwa jangwa
la sahara na hali ya kisiasa kwa ujumla, fuatana nami katika maandishi
haya ya kusisimua;
Kusini mwa jangwa la Afrika si salama
Dalili za wazi zinaonyesha kuwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la
Sahara zipo katika hali mbaya zaidi ya nchi za kiarabu zilizopinduliwa
kama Misri na Tunisia , halikadhalika kwenye mataifa hayo ya kusini
mwa jangwa la sahara kuna ukosefu mkubwa zaidi wa ajira hivyo kufanya
idadi kubwa ya vijana kuwa wazururaji kuliko Burkinafaso ambayo
imepinduliwa hivi karibuni. Sasa ikiwa hali iko hivi kwanini viongozi
wa mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara hawachukui tahadhari?
Kwanini wanazidi kujisahau?
Viongozi wengi wa kusini mwa jangwa la sahara wanategemea kuudhibiti
upinzani kwa msaada wa vyombo vya dola mfano mzuri ni hujuma kubwa
dhidi ya viongozi wa upinzani kwenye baadhi ya mataifa yanayounda
jumuiya ya Afrika Mashariki. Tatizo kubwa la marais hawa nikule
kudhani kuwa vyombo vya dola vinaweza kuudhibiti umma, wanapaswa
kujifunza kwa makini maana halisi ya nguvu za umma na athari zake kwa
muktadha wa siasa za taifa lolote ulimwenguni, yatosha kuzingatia kuwa
umma haujawahi kushindwa.
Vyama vingi tawala vitakataliwa
Kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wake kwa wananchi vyama vingi
tawala vitakataliwakatika mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara.
Kuanzia miaka ya 1990 vuguvugu la vyama vya upinzani limeweza
kuving'oa vyama tawala kadha wa kadha mifano ya UNIP Zambia, KANU
Kenya na PDS Senegal hapa pia usisahau kuangushwa kwa chama cha UMD
cha Fredrick Chiluba huko Zambia kilipopoteza kwa Michael Satta wa PF.
Angukohili la vyama tawala halikwepeki hasa kwa kuzingatia udhaifu wa
vyama hivyo katika kushughulikia shida za wanyonge ikiwamo bei za
mazao, ajira na kupanda kwa gharama za maisha, utegemezi mkubwa wa
nchi za kiafrika kwa wawekezaji kutoka nje ,uwekezaji ambao umeshindwa
kuondoa umasikini una kila dalili mbaya kwa vyama vya ANC Afrika
Kusini, FRELIMO Msumbiji na CCM Tanzania, kuelekea 2030 vyma hivi
vimezidi kupunguza idadi ya kura huku upinzani ukizidi kushika kasi
kwenye nchi zao.
Marais ving'ang'anizi watang'olewa kabla ya 2030
Mwanahistoria Jovitus Mwijage katika kitabu chake "Major Events in
African History" akielezea kushindwa kwa viongozi wengi waliotwaa
madaraka kwa njia za mapinduzi mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzano
mwa miaka ya 1990 , katika ukurasa wa 308 anasema "Under the auspices
of the constitutions made by them (African dictators), the ballots
could not change the existing leadership; therefore, the barrel of the
gun eventually became answer to those political puzzles. Even the
constitutions made after the coups could not attend to the interests
of the masses.The leaders of the coups made the constitutions, which
were to ensure that their evil interests were fulfilled. Such
constitutions appeared in Uganda, Sudan, Angola, Congo, Zimbabwe,
Gabon, Togo and Rwanda".
Hali hii ya viongozi kadhaa wa kiafrika ambao awali walionekana kuwa
wawakilishi wa kweli wa wananchi lakini polepole wakazivunja miguu
katika za nchi zao ili waendelee kutawala hivyo kugeuka
ving'ang'anizini sababu nyingine itakayopelekea mapinduzi kwa nchi
hizo. Iwe ni mapinduzi ya umma ama vinginevyo lakini marais
ng'ang'anizi kama Yoweri Museveni wa Uganda na mwenzake Paul Kagame wa
Rwanda wamekalia kuti kavu kwani wananchi hawataki ufalme ama usultani
bali wanataka demokrasia inayozingatia ukomo wa madaraka. Ikiwa
watawala wa mataifa haya wataendelea kukaa madarakani basi joto
kisiasa halitawaacha salama, wimbi la mabadiliko litawafagia mmoja
baada ya mwingine kuelekea 2030.
Nova Kambota ni mchambuzi na mwandishi wa siasa, hii ni sehemu ya
maoni yake ya hivi karibuni kuhusu mapinduzi ya umma na mwelekeo wa
siasa katika mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara. Nova Kambota
anapatikana jijini Dar es salaam, simu +255712 544237, barua pepe;
novakambota@gmail.com , Blog; http://novakambota.wordpress.com
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CABkmAOLSG3ySTSQ1Df0q1VErqKLsw9c9CRBqV43_KwwoLvNTEw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments