[wanabidii] CCM WANATUMIA SKANDALI YA ESCROW KUSHINDA UCHAGUZI!

Monday, November 24, 2014

Kuna kila dalili kwamba CCM wamelenga kuitumia skandali ya Escrow inayowaandama kama kete ya kushinda kirahisi uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Tathmini niliyoifanya tangu skandali hii ishike kasi hapa nchini inaonyesha kwamba vyama vya siasa na wanachi walio wengi wameelekeza macho na masikio yao kwenye skandali hii kuliko kujielekeza kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao. Hata UKAWA na wafuasi wao nao wameingia mkenge na kujikuta wakitumbukia kwenye mtego huu wa CCM.
 
Tathmini yangu inaonyesha kwamba hivi sasa CCM wanawatumia makada wao kwenye ngazi za Kata kujipanga kuchakachua matokeo ya uchaguzi huu kuanzia kwenye uandikishaji wa wapiga kura hadi siku ya kupiga, kuhesabu na kujumlisha kura. Leo nimetembelea vituo 15 vya uandikishaji wapiga kura na kati ya vituo vyote hivyo ni vituo 5 tu ambavyo nimekuta vina mawakala wa vyama vya siasa, na wengi wao ni wa CCM. Katika vituo hivyo 5 vilivyokuwa na mawakala ni kituo kimoja tu ambacho kilikuwa na wakala wa UKAWA. Hapa ndipo CCM itakapoanzia kuchakachukua idadi ya wapiga kura na hatimaye kushinda kilaghai. Wakati CCM wakiwatumia makada wao wa ngazi za chini kuchakachua uandikishaji, wanaUKAWA wote wameelekeza nguvu zao kwenye skandali ya Escrow.
 
Ndio maana CCM wanajitahidi kurefusha hili sakata la Escrow ili wazidi kuwazubaisha UKAWA wakati wao wakiendelea na uchakachuaji kama kawaida yao. Mawakala wa vyama vyote wanapaswa kuwepo kwenye eneo la uandikishaji ili kuhakikisha kwamba wanachi wanaoenda kujiandikisha wanatoka kwenye Mitaa, Vijiji, au Vitongoji husika. Kuna kila dalili kwamba CCM wamejipanga kuchomekea mamluki na kuwaandikisha kwenye maeneo ambayo hawahusiki ili kujiongezea kura haramu na kushinda viti vingi zaidi kuliko UKAWA. Nitoe wito kwa makada wote wa UKAWA, hasa wa ngazi za chini muwe makini na ulaghai huu wa CCM ili kudhibiti aina yoyote ya udanganyifu unaofanywa na CCM. Msipofanya hivyo sasa hivi na kuwaachia CCM kuchomekea mamluki wao kwenye daftari la wapiga kura, ikafika siku ya kupiga kura poliCCM watawasaidia CCM kufanikisha mamluki hao kupiga kura hata kama mtawagundua siku hiyo.
 
WanaUKAWA msikubali kusubiri hadi siku ya mwisho ndipo mawakala wawazuie mamluki kupiga kura. Mtakuwa mmechelewa sana na hamtafua dafu mbele ya poliCCM wenye silaha za moto na mabomu ya machozi. Ni bora kuziba ukuta sasa kuliko kujenga ukuta baadaye. Kila kiongozi wa UKAWA ajione anawiwa kuwahamasisha wananchi kwenye eneo lake waende wajiandikishe ili waje watusaidie kuwandoa hawa panya (CCM) kihengeni wasije wakatulaze njaa huku tunawachekea. Hakuna namna tunayoweza kujiokoa kutoka kwenye utumwa na UFISADI wa CCM zaidi ya kuwaondoa madarakani kupitia sanduku la kura. Tanzania bila CCM inawezekana, timiza wajibu wako wa kuwapigia kura wagombea wa UKAWA ili wawe viongozi wetu katika Kata, Vijiji na Vitongoji.
 
Nawasilisha.
 

Share this :

Related Posts

0 Comments